Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Icadon, btw, a pact is a pact; shares cannot circumvent a treaty! Well, at least to my opinion.

SteveD.

Tanzania kila kitu kinawezekana...labda huu ndio mwanzo tuwape muda tuone
 
HIVI RUSHWA IMEANZA LEO AU KWA KUWA MKUKI KWA NGURUWE.........JE WAASI WA RUSHWA KWA KUIITA MAJINA MATAMU KAMA VILE TAKRIMA, ASANTE, 10%, NA MENGINEYO WANAJIFIKIRIAJE?

na Dauson Harold--Tanzania Daima

MWENYEKITI wa Jukwaa la Uchumi, Idd Simba, amesema taifa letu hivi sasa limegubikwa na rushwa kiasi kwamba vyombo vingi vya utawala vinaendeshwa kwa rushwa.
Alisema imefikia hatua kwamba hata huduma za msingi hutolewa kwa rushwa na akasema mahakama na hospitali zinaendeshwa kwa rushwa, na elimu hutolewa kwa ubaguzi kwa sababu ya rushwa.

Iddi Simba, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alisema hivi sasa hakuna Mtanzania asiyefahamu rushwa ni nini na kwamba kila mtu anajaribu kufatuta mwanya katika utaratibu wowote, ili atoe rushwa, ama kudai au kupokea.

Mfanyabiashara na mwanasiasa huyo aliyepata pia kuwa mbunge wa Ilala, alisema hayo jana katika mkutano uliokuwa ukizungumzia masuala ya rushwa, utawala bora na umilikaji wa njia kuu za uchumi wa nchi yetu.

Alisema sasa imefikia wapiga kura ndio wanaodai rushwa, na akasema hivi karibuni tutasikia watoto wa shule nao wanadai rushwa kwa wazazi, ili wakubali kwenda shule.

“Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, matukio ndani ya nchi yetu yametudhihirishia mengi ambayo wengi wetu tumekuwa tukiyasikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hali ya uchumi ni mbaya sana.

“Tukiendelea na shughuli kama kawaida, tutafika mahali ambapo hatutaweza kurekebisha chochote, na taifa litaangamia. Tutakuwa tumewakosea watoto wetu na wajukuu wetu. Tutakuwa tumelikosea taifa.

“Hali ya uchumi ni mbaya kiasi kwamba idadi ya kutosha ya wananchi wamekwisha kusahau thamani ya maisha. Kuna Watanzania waliobanwa na ugumu wa uchumi mbovu kiasi cha kuuza uhuru wao wa kuchagua viongozi,” alisema Simba.

Alisema kuwa mwananchi aliyefikia hapo ni dhahiri hana tena matumaini ya kupata maendeleo kwa kutumia uhuru na haki yake ya kikatiba, na kwamba kuna vijana wengi walio radhi kuuza miili yao bila kujali kuambukizwa virusi vya ukimwi ilimradi apate kuishi maisha ya starehe, mafupi kuliko maisha aliyonayo sasa.

Aidha, alisema wananchi wamekwishaamua kwamba ziko dhambi ambazo si dhambi tena, bali ndiyo njia ya maisha. Viongozi wa dini wanaita dhambi za aina hii kuwa ni dhambi za mfumo.

Aliendelea kueleza kuwa Watanzania wamekubali kubweteka na kuingizwa au kujiingiza katika mfumo unaowalazimisha kutenda dhambi na kusema kwamba anafahamu kwamba viongozi wa dini sasa kazi zao zimekuwa ngumu.

Alisema wako katika mchakato mpya wa kujaribu kubadili nchi kwa kujipa matumaini mapya na malengo ambayo japo ni makubwa, lakini yanatekelezeka.

“Tunataka watu wetu wapate mwamko mpya wa kujikomboa katika utumwa uliokwishapata nguvu. Utumwa wa kuthamini mali kuliko watu. Utumwa wa kutumia binadamu wengine kupata na kupora rasilimali za taifa, badala ya kutumia rasilimali hizo kuongeza thamani ya maisha ya wananchi,” alisema.

Alisema maisha ya amani, furaha na utulivu yamekwishapotea na kwamba tunastahili kuendesha maisha yatayotuwezesha kuutambua utukufu wa Mwenyezi Mungu hapa duniani, maisha yenye urahisi wa kupata mahitaji muhimu.

Simba, alisema utumwa huu ni ule ambao umekuwa ukitukabili kwa karne kadhaa ukiitwa ubeberu, isipokuwa sura yake imebadilika kutokana na maendeleo ya kiteknolojia.

“Teknolojia inayoendeshwa na wale wale waliotutawala kabla ya uhuru. Lazima tujiangalie wenyewe tujitambue sisi binadamu ni kitu gain? Na Tanzania ni kitu gain?

“Je, ubinadamu wetu ni kitu gani na uzalendo ni kitu gain? Wengi wetu hawaoni viongozi wenye nyadhifa mbalimbali, lazima tujiulize tena ni nini maana ya kuwaongoza binadamu wengine. Je, utawala bora ni nini?” alihoji Simba.

Alieleza kwamba baada ya uzoefu walioupata kwenye uongozi, wameelewa makosa yao ya kushindwa kujenga taifa lenye furaha na ustawi, badala yake wamejenga taifa ambalo bado limegubikwa na umaskini, maradhi na ujinga.

“Machungu ya makosa haya ni makali sana kwa wananchi wote, lakini kwa ujasiri wetu wa kibinadamu tunaweza kutumia machungu hayo kuwa mafundisho yetu ya leo na kesho.

“Hivi leo tunatambua pia jinsi gani sera zetu zinavyoendelea kujenga tabaka kubwa mno la mamilioni ya wasionacho, na tabaka dogo sana la walionacho. Hii ina maana kwamba malengo ya milenia tunayodhamiria kuyafikia mwaka 2025 yatakuwa ni ndoto tu.

Tukiangalia nchi yetu miaka 52 baada ya Vita ya Pili ya Dunia, tunaona kwamba uongozi wetu wenyewe umetushinda kulipa taifa matumaini mapya.

“Wala hakuna ushahidi kwamba tukiendelea na sera za sasa za ubinafsishaji na wawekezaji kutoka nje, tutaweza kubadili hali hii ya kukatisha tamaa.

“Rasilimali asili kama vile madini, bidhaa za misitu, mazao ya kilimo, haviwezi kugeuzwa kuwa utajiri na mtaji wa kutukomboa wazawa wa nchi hii, basi kuingia kwetu kwenye mfumo wa ubepari umekuwa kazi bure,” alisema.

Kadhalika, alieleza kuwa yeyote anayefikiri au kuamini kwamba taifa letu linaweza kuendelezwa na kukombolewa na wawekezaji kutoka nje, anajidanganya na akasema ni lazima tuwe na mikakati madhubuti ya kuwamilikisha wazalendo uchumi wa nchi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen Kijo-Bisimba, aliyetoa mada ya utawala bora, alisema kuwa utawala bora ni ule unaoongozwa na sheria, kanuni na kufuata matakwa ya watu waliowachagua.
 
Idd Simba,umeongea mambo ambayo kila siku tunaimba kuhusu hali halisi ya nchi,pongezi kwa kuligundua hilo,labda watu kama nyie mkisema mambo kama hayo yanaweza kuwafikia akina muungwana.Naona watu wengi sasa wameanza kusoma alama za nyakati,na kila mtu anaona mwelekeo wa Tanzania si mzuri.Tanzania ya Mwl JK,na Tanzania ya Msanii JK zina utofauti mkubwa sana.

PM wa Japan alivyoshindwa kuongoza serikali yake kaachia madaraka taratibu,sasa Kikwete anasubiri nyingi,hakuna rais aliyevurunda ndani ya kipindi kifupi cha uongzoi wake kama huyu mshikaji.Anatupeleka Zimbabwe,maisha bongo hayaendi.
 
Huyu mzee aache kutuyeyusha. Kama anataka kuongelea rushwa basi kwanza aueleze umma wa watanzania ukweli wa ndani wa ule uchafu uliomlazimu kutoka serikalini. Bila ya hapo hawezi kuwa tofauti na wajanjawajanja wengine.

Nadhani tujenge tabia ya kuwalazimisha watu kama hawa kutoa ukweli wote kuhusu uozo wao wa zamani kabla ya kuanza kuwapa uwanja wa kujinadi kama wapinga rushwa na ufisadi.

Mwengine ni Mzee Mengi.....

Tanzanianjema
 
Very true, ila angalau yeye alipata kutoboa mambo hadharani au hata kujitoa serikalini
 
Rushwa yamliza Idd Simba

na Dauson Harold
Tanzania daima

MWENYEKITI wa Jukwaa la Uchumi, Idd Simba, amesema taifa letu hivi sasa limegubikwa na rushwa kiasi kwamba vyombo vingi vya utawala vinaendeshwa kwa rushwa.
Alisema imefikia hatua kwamba hata huduma za msingi hutolewa kwa rushwa na akasema mahakama na hospitali zinaendeshwa kwa rushwa, na elimu hutolewa kwa ubaguzi kwa sababu ya rushwa.

Iddi Simba, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alisema hivi sasa hakuna Mtanzania asiyefahamu rushwa ni nini na kwamba kila mtu anajaribu kufatuta mwanya katika utaratibu wowote, ili atoe rushwa, ama kudai au kupokea.

Mfanyabiashara na mwanasiasa huyo aliyepata pia kuwa mbunge wa Ilala, alisema hayo jana katika mkutano uliokuwa ukizungumzia masuala ya rushwa, utawala bora na umilikaji wa njia kuu za uchumi wa nchi yetu.

Alisema sasa imefikia wapiga kura ndio wanaodai rushwa, na akasema hivi karibuni tutasikia watoto wa shule nao wanadai rushwa kwa wazazi, ili wakubali kwenda shule.

“Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, matukio ndani ya nchi yetu yametudhihirishia mengi ambayo wengi wetu tumekuwa tukiyasikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hali ya uchumi ni mbaya sana.

“Tukiendelea na shughuli kama kawaida, tutafika mahali ambapo hatutaweza kurekebisha chochote, na taifa litaangamia. Tutakuwa tumewakosea watoto wetu na wajukuu wetu. Tutakuwa tumelikosea taifa.

“Hali ya uchumi ni mbaya kiasi kwamba idadi ya kutosha ya wananchi wamekwisha kusahau thamani ya maisha. Kuna Watanzania waliobanwa na ugumu wa uchumi mbovu kiasi cha kuuza uhuru wao wa kuchagua viongozi,” alisema Simba.

Alisema kuwa mwananchi aliyefikia hapo ni dhahiri hana tena matumaini ya kupata maendeleo kwa kutumia uhuru na haki yake ya kikatiba, na kwamba kuna vijana wengi walio radhi kuuza miili yao bila kujali kuambukizwa virusi vya ukimwi ilimradi apate kuishi maisha ya starehe, mafupi kuliko maisha aliyonayo sasa.

Aidha, alisema wananchi wamekwishaamua kwamba ziko dhambi ambazo si dhambi tena, bali ndiyo njia ya maisha. Viongozi wa dini wanaita dhambi za aina hii kuwa ni dhambi za mfumo.

Aliendelea kueleza kuwa Watanzania wamekubali kubweteka na kuingizwa au kujiingiza katika mfumo unaowalazimisha kutenda dhambi na kusema kwamba anafahamu kwamba viongozi wa dini sasa kazi zao zimekuwa ngumu.

Alisema wako katika mchakato mpya wa kujaribu kubadili nchi kwa kujipa matumaini mapya na malengo ambayo japo ni makubwa, lakini yanatekelezeka.

“Tunataka watu wetu wapate mwamko mpya wa kujikomboa katika utumwa uliokwishapata nguvu. Utumwa wa kuthamini mali kuliko watu. Utumwa wa kutumia binadamu wengine kupata na kupora rasilimali za taifa, badala ya kutumia rasilimali hizo kuongeza thamani ya maisha ya wananchi,” alisema.

Alisema maisha ya amani, furaha na utulivu yamekwishapotea na kwamba tunastahili kuendesha maisha yatayotuwezesha kuutambua utukufu wa Mwenyezi Mungu hapa duniani, maisha yenye urahisi wa kupata mahitaji muhimu.

Simba, alisema utumwa huu ni ule ambao umekuwa ukitukabili kwa karne kadhaa ukiitwa ubeberu, isipokuwa sura yake imebadilika kutokana na maendeleo ya kiteknolojia.

“Teknolojia inayoendeshwa na wale wale waliotutawala kabla ya uhuru. Lazima tujiangalie wenyewe tujitambue sisi binadamu ni kitu gain? Na Tanzania ni kitu gain?

“Je, ubinadamu wetu ni kitu gani na uzalendo ni kitu gain? Wengi wetu hawaoni viongozi wenye nyadhifa mbalimbali, lazima tujiulize tena ni nini maana ya kuwaongoza binadamu wengine. Je, utawala bora ni nini?” alihoji Simba.

Alieleza kwamba baada ya uzoefu walioupata kwenye uongozi, wameelewa makosa yao ya kushindwa kujenga taifa lenye furaha na ustawi, badala yake wamejenga taifa ambalo bado limegubikwa na umaskini, maradhi na ujinga.

“Machungu ya makosa haya ni makali sana kwa wananchi wote, lakini kwa ujasiri wetu wa kibinadamu tunaweza kutumia machungu hayo kuwa mafundisho yetu ya leo na kesho.

“Hivi leo tunatambua pia jinsi gani sera zetu zinavyoendelea kujenga tabaka kubwa mno la mamilioni ya wasionacho, na tabaka dogo sana la walionacho. Hii ina maana kwamba malengo ya milenia tunayodhamiria kuyafikia mwaka 2025 yatakuwa ni ndoto tu.

Tukiangalia nchi yetu miaka 52 baada ya Vita ya Pili ya Dunia, tunaona kwamba uongozi wetu wenyewe umetushinda kulipa taifa matumaini mapya.

“Wala hakuna ushahidi kwamba tukiendelea na sera za sasa za ubinafsishaji na wawekezaji kutoka nje, tutaweza kubadili hali hii ya kukatisha tamaa.

“Rasilimali asili kama vile madini, bidhaa za misitu, mazao ya kilimo, haviwezi kugeuzwa kuwa utajiri na mtaji wa kutukomboa wazawa wa nchi hii, basi kuingia kwetu kwenye mfumo wa ubepari umekuwa kazi bure,” alisema.

Kadhalika, alieleza kuwa yeyote anayefikiri au kuamini kwamba taifa letu linaweza kuendelezwa na kukombolewa na wawekezaji kutoka nje, anajidanganya na akasema ni lazima tuwe na mikakati madhubuti ya kuwamilikisha wazalendo uchumi wa nchi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen Kijo-Bisimba, aliyetoa mada ya utawala bora, alisema kuwa utawala bora ni ule unaoongozwa na sheria, kanuni na kufuata matakwa ya watu waliowachagua.

tape-1.jpg
 
Aende nyumbani kwake akapumzike, nadhani kwao ni Tanzania. Japo kuwa Baba yake inasemekana kuwa ni mhutu!
 
Tanzania kuna watu kama Kinana ambaye ni Msomali, Simba ambaye uraia wake una utata, Balali ambaye mbali na kuwa na uraia wa US kuna uwezekano kabisa kuwa si mtanzania, Mungai ambaye ni wazi kabisa baba yake alikuwa Mkenya, Jenerali Ulimwengu mbaye nae anasemwa kuwa mtusi and so on.......Je kuna watanzania nje ya nchi ambao wameshika nafasi za uongozi wa juu kwenye serikali za nchi jirani? Au sisi ndio wa kuongozwa tu na wengine? Maana nafahamu kuna jamaa mmoja amekuwa wazirikwenye nchi tatu tofauti sijui kama sisi watanzania tuna watu kama hao, au ndio bado tumelala.
 
Tunahitaji Uzawa ambao unaonekana kuwa mwiba mkubwa kwa CCM .
 
Tanzania kuna watu kama Kinana ambaye ni Msomali, Simba ambaye uraia wake una utata, Balali ambaye mbali na kuwa na uraia wa US kuna uwezekano kabisa kuwa si mtanzania, Mungai ambaye ni wazi kabisa baba yake alikuwa Mkenya, Jenerali Ulimwengu mbaye nae anasemwa kuwa mtusi and so on.......Je kuna watanzania nje ya nchi ambao wameshika nafasi za uongozi wa juu kwenye serikali za nchi jirani? Au sisi ndio wa kuongozwa tu na wengine? Maana nafahamu kuna jamaa mmoja amekuwa wazirikwenye nchi tatu tofauti sijui kama sisi watanzania tuna watu kama hao, au ndio bado tumelala.

Hivi Utanzania ni Kabila ama Utaifa? Huu ndio ubaguzi wenyewe. Tu-deal na Simba kama mtu aliyewahi kuhusika na rushwa na ufisadi lakini sio asili yake...

Tanzanianjema
 
Moja ya habari ambayo ilinivutia siku ya jumatano ya wiki hii ni hii ya kampuni ya mwananchi communications kuungana na the gardian kupambana na rushwa katika sekta nzima ya habari .

Kwa ujumla vyombo vyote hivi vya habari vimejizolea sifa kibao sio tu kwa watanzania bali hata nje ya mipaka ya Tanzania , na sasa hivi zinasomwa zaidi kupitia katika mitandao na hizo tovuti zao kwahiyo haya ni mafanikio makubwa .

Kila mtu anakubaliana na mimi ninaposema hakuna sehemu yenye rushwa zaidi kama mamlaka za habari na taarifa , huku ndio kwenye kila kitu , mwandishi wengi sikuhizi wamefikia hatua ya kuandika habari wanazopenda wao na sio zile ambazo zitapendeza wengi na kufanya wengi waweze kuchangia .

Nimeupongeza uamuzi huu lakini pia nimeshangaa kidogo kuhusu magazeti mengine au vyombo vingine binafsi vya habari viko wapi kwanini havijaamua kuja kuungana na pamoja na magazeti haya ?

Labna kampuni ya mwananchi na nipashe hawakuamua kuwashirikisha kutokana na sababu kadhaa ambazo nahisi hata mimi naweza kuzitaja , ingawa sina uhakika nazo kwa asilimia zaidi ya 100 .

Mfano gazeti la Tanzania Daima , hili ni gazeti mali ya CHADEMA la chama cha siasa , sasa inawezekana sera za CHADEMA hazirhusu Tanzania daima kupigana vita ya rushwa hata hivyo fremedia ni kampuni changa haijajitanua sana sidhani kama inaweza kupimana ubavu na hizi mbili .

Pia kuna magazeti kama Daily News , Uhuru na kadhalika ambayo yanahusiana na serikali zaidi , inasemekana watu wengi walio serikalini ndio wanaongoza katika kutoa hongo haswa wakati wa uchaguzi na wakati mwingi kununua waandishi wawaandikie makala nzuri nzuri .

Kuna magazeti ya udaku kama HOJA , Mwanahalisi , UWAZI , RISASI , SANI , KIU na mengine mengi magazeti haya habari zao ni tegemezi wananunua kutoka kwa watu haswa habari za picha , haya magazeti ya udaku na waandishi wake ni rahisi sana kuhongeka au kuhonga katika kutoa au kupokea habari za matukio na picha

Mfano wakati wa uchaguzi mwaka jana waandishi wengi wa Habari Cooperation walinunulia ili waandike makala nzuri nzuri kwa ajili ya kuremba viongozi Fulani Fulani mmoja wao ni Majid Mjengwa , Muhigo na wengine wengi ambao wanaheshimika katika uchambuzi .

Na mwisho kabisa nafikiri maamuzi haya ya kuungana yaliyakiwa yakutanishe wamiliko wote wa vyombo vya habari , vya serikali na watu binafsi , mashirika na kadhalika ili kuweza kuweka usawa na uwajibikaji katika sekta nzima ya habari
 
vizuri lakini ipp kupambana rushwa ???? mengi na wewe kwanza lipa madeni unayodaiwa na serikali then mengine yatafuata !
 
Habari Corporation has shares in Mwananchi Communications.
Lakini anayepigana vita na rushwa ni Media Solutions Limited (kulikoni na this day), sio IPPMEDIA. The right candidate for Mwananchi kuungana nae ni Media solutions ambae ameshavianza vita kwa kasi. Media solutions, mengi made a smart move to make it as separate entity and brought in heavy weights wengine kama kina iddi Simba n.k
 
Mchambuzi
KUna developments zimetokea hapa Tanzania zinafurahisa sana. INaonekana PCCP wameanza kuwashughulikia wala rushwa na watoa rushwa wadogodwadodo CCM, what is your take? Mungai, Mangula, Arusha huko kina Laizer.......hii inatueleza nini. what will it be like in 2005
 
Kwa mtazamo wangu, hiyo kazi PCCP wataifanya vizuri sana as long as haiwahusu watu wa mtandao, atleast for a start. Chama chini ya mwenyekiti wake kinajua fika kwamba kuna tatizo la rushwa na wananchi wamekodoa macho kuangalia chama kinafanya nini kuhusu suala hilo. matokeo yake ndio hayo ya hao wabunge arusha.

Mungai kuanguka ni bahati mbaya tu. huyu mbunge kwa miaka mingi amekuwa na matatizo kuhusu background yake ni mkikuyu etc. Hili suala sio geni na limem cost hata ubunge on and off kwa miaka mingi. ingawa yeye ni mtu wa mtandao, mwamuzi wa mwisho katika suala la NEC iringa walikuwa ni wana ccm wa pale mkoani. Prof Msolla ametumia vizuri weakness hiyo ya mungai ambayo ipo for decades. Mungai angeenda kugombea viti vya NEC taifa na hata angeanguka kule, wanaoanguka ni wengi.

Mangula alikuwa ana kazi ngumu sana Iringa na on him mtandao haukuwa na kazi kubwa kumwangusha. This was abvious. Angekuwa na busara na kumwiga sumaye kugombea NEC taifa na huku angepita tu kama sumaye atakavyopita.

What will it be like in 2015 you meant? CCM haitakuwa CCM ya leo bali ile nyerere aliyotabiri kwamba upinzani wake wa kweli utatokea ndani ya ccm. Kina mangula hawatakuwa na influence yoyote, all eyes should be on mwandosya na Lowassa au any other ccm shot ambae atakuwa groomed na mtandao. Rais 2015 hatatoka nje ya baraza la mawaziri wa sasa.
 
Mchambuzi, hii ni kutishia upinzani au mjumuisho wa takwimu zako kutoka kwa Watanzania wote kuwa upinzani hautashinda 2015?!... Au ndiyo hivyo tena, mabox ya kura yalisha jazwa tayari na wagombea kutoka CCM?... fafanua tafadhali. Ahsante.

Rais wa Tanzania 2015 bado atatoka CCM. Wakijitahidi sana upinzani, wataweza ambulia kupata umakamu au uwaziri mkuu kutokana na nguvu yao kama wataipata kwenye majimbo na pia kura za urais. lakini that is too too far from being fetched. Wapinzani wameanza vizuri na kina kabwe, slaa lakini kete ya kushinda uchaguzi wa rais Tanzania haupo just on kufichua rushwa na wezi kwa sababu hata ndani ya ccm, that can be done if worse comes to worse. Kete ya kushinda urais Tanzania ipo kwenye masuala mengine ambayo yanawagusa wananchi moja kwa moja, mfano kuboresha maisha ya wakulima na wafanyakazi in the context of maintaining amani na utulivu na kuweka bayana mikakati yote towards that objective. So far, ccm has candidates for that, na sio lazima wana ccm wa mtandao.
 
Back
Top Bottom