Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

wakitaka niamini kweli, foremost wamfuate lowassa ! then wazee wa vyama mbalimbali maana nao wamo !
 
Hivi huyu mzee Hosea mbona ana utani wa reja reja.Ana uhakika ataweza kuwahoji watu hawa na kuwachukulia sheria,au anacheza ngoma za mchana barabarani,kauli zingine si za kuropoka tu,ili mradi watu wakuone.Mie napendekeza majina haya yafanyiwe kazi,
Mkapa,Sumaye,Balali,Lowassa,Manji,Mwinyi,Mahita,anzia na hawa halafu baadae utupe feedback,sio unarukaruka tu kama chura.
 
Hapo kuna watu wamelengwa,hii kitu itatumika kuumizana au kukomoana,hawa pccb ni watu hatari sana tena wakuogopwa kama ukoma,mtu atakaye kuwa agaist na watawala basi atatupiwa hawa mbwa wa pccb.Hapa tutakuja kuzusha vurugu maana sheria za bongo huwa zinachagua watu.
Amerudia tena kuwa maraisi wote hawaguswi na hii sheria sijui tunakwenda wapi.
 
Hiyo sheria ipo siku nyingi sana kama huwezi kuonyesha jinsi ulivyolipa kodi kutokana na mali uliyonayo. Haya maswali niliuliza wakati EL alipotoa 60 million kwenye charity kama alilipia kodi zile pesa.

Unafahamu hii sheria iko kama sikosei TRA nafikiri kwenye mapato n.k. Huyu TAKUKURU ni mbabaishaji mwingine tu anatumwa na serikali, kuna wezi wengi tu wanapeta, wanaleta danganya toto nyingine. UPUUZI HUU UTAISHA TU IKIWA HIZI TUME ZITAFANYA KAZI BILA KUINGILIWA NA WANASIASA.

Angalia Hapa wenzetu hata wakikukuta unaendesha gari la kifahari ambapo huwezi kuonyesha kodi uliyolipa na ulivyopata hiyo pesa wanakunyang'anya.
 
sikubaliani na hii ya kuchunguza watu kwa sababu wanamajumba makubwa au kwa sababu mtu anaendesha Range Rover Vogue Dar

Hiii ni witch hunt na sidhani kama matokeo yake yatakuwa mazuri. Hawa jamaa kazi yao ni kuchunguza wakipata ushahidi wenye kuonyesha wazi kuwa kuna rushwa ililika then wanapeleka majalada ya prosecutor wa serikali. Sasa mfano wataanza kuwachunguza akina RUPIA kwa sababu wana majumba mazuri Dar? Je akina SYKES watapona?

Hivi katika dunia ya leo hawa hawatompata mtu na kama wakos erious then inabidi ma civil servants waongezewe mishahara ambayo inaendana na hali halisi ya uchumi wa nchi
 
Nyumba ni kielelezo cha maendeleo bora hao wanaojenga hapa nchini kuliko wale wanaojenga ughaibuni.

Na pia wahindi wachunguzwe ni kwa nini hawajengi nyumba hapa nchini ?wao wakishachukua wanaenda kujenga kwao.
 
Nyumba ni kielelezo cha maendeleo bora hao wanaojenga hapa nchini kuliko wale wanaojenga ughaibuni.

Na pia wahindi wachunguzwe ni kwa nini hawajengi nyumba hapa nchini ?wao wakishachukua wanaenda kujenga kwao.

Wajenge kwetu???

Wabaguzi wakubwa! Tena hao kwa rushwa ndo wenyewe, na wasi wasi wangu ni kwamba, at the end, PCCB ndo watakuja kuwa wala rushwa namba moja kwa mwendo huu! make wakienda chunguza wanakatiwa yanaisha.. yaani ndo dili zenyewe hizo mwendo wa TRA, muhindi akipangiwa kodi halisi mil. 60, afisa tra anamwambia leta 10mil na ndo imetoka!
 
nadhani hawa wanataka kutuletea vurugu tu,i think wezi wametengenezwa ni mifumo ya wakati huo,the system wa loose.ukianza kuchunguza samaki wadogo ambao kwa kweli ndi tulio wengi,na kwa kipato chetu mfano mimi binafsi i cant explain nimejenga vipi,hata yeye mwenyewe Hosea hawezi akatuambia amejengaje nyumba yake.
Tatizo he is talking alot he has to perform then the public will rate him.
pia we had an experience toka kwa akina apiyo,ambae watu walimuona anavyolia kwenye TV ametelekezwa,do you think kuna mtu atataka afe njaa,that means if you do not create a system people will create it to fill in the empty.
leo ndo wanataka wapeleke muswaada bungeni wa mortgage financing,ili sasa watu wajenge kwa mikopo.bila hilo ndo maana bongo kila baadaa ya nyumba unakuta nyumba tofauti,the same street hapa ghorofa hapa nyumba fupi,hapa kigae hapa bati so what!
 
sikubaliani na hii ya kuchunguza watu kwa sababu wanamajumba makubwa au kwa sababu mtu anaendesha Range Rover Vogue Dar

Hiii ni witch hunt na sidhani kama matokeo yake yatakuwa mazuri. Hawa jamaa kazi yao ni kuchunguza wakipata ushahidi wenye kuonyesha wazi kuwa kuna rushwa ililika then wanapeleka majalada ya prosecutor wa serikali. Sasa mfano wataanza kuwachunguza akina RUPIA kwa sababu wana majumba mazuri Dar? Je akina SYKES watapona?

Hivi katika dunia ya leo hawa hawatompata mtu na kama wakos erious then inabidi ma civil servants waongezewe mishahara ambayo inaendana na hali halisi ya uchumi wa nchi

Hivi kama una biashara yako na your books are in order unaogopa nini? Labda wengine wana biashara za unga kutoka Brazil...............itabidi wajirekebishe kwa sababu nchi yoyote haiwezi kuendelea wakati wananchi wake hawataki kulipa kodi na ni wakwepaji wakubwa.
 
98257.jpg


Prevention & Combating of Corruption Bureau Director General Edward Hoseah (C) addresses a forum for editors in DSM on recent amendments to the PCCB Act 2007.He is flanked by MOAT Chairman Reginald Mengi (R)& Editors Forum Chairperson Sakina Dattoo.

Picture kwa hisani ya IPP Media.
 
Haya JF msishangae kuona kuwa kati yetu wenye midomo mikubwa wakaambiwa wana mali kuliko uwezo wao
 
MCL, IPP zaungana kupambana na rushwa
Na Mwandishi Wetu
Gazeti la Mwananchi

KAMPUNI za Mwananchi Communications Limited (MCL) na IPP Media zimekubaliana kuunganisha juhudi za kupambana na rushwa kwa waandishi wa habari.

Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa jana na pande zote kwenye Hoteli ya Movenpick ni kuhakikisha waandishi wa kampuni hizo hawapokei 'bahasha' kutoka kwa watoa habari.

Katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa, viongozi wa kampuni hizo walikubaliana kuwazawadia waandishi wao ambao watakuwa wanakataa fedha maarufu kama mshiko kutoka kwa watoa habari.

Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, alisema hatua hiyo inalenga kuweka mshikamano kwenye masuala yenye maslahi kwa taifa na kwamba kuanzia sasa hawatakubali mtu yeyote kuwagawa.


"Naona sisi IPP na MCL tuanze, sio kwamba tunawabagua wengine (vyombo vya habari), hapana. Wakitaka watatufuata, ila sisi lazima tuwe na mshikamano kwenye masuala yenye maslahi na taifa na kulinda hadhii ya taaluma ya habari inayozidi kuporomoka kila siku," alisema Mengi.

Mengi alisema katika ushirikiano wa aina hiyo wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji kama kusafirisha magazeti kwa kutumia usafiri (magari) wa pamoja ili kuimarisha mshikamano na mafanikio kwa makampuni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Sam Shollei, alisema iwapo suala la rushwa halitaanza kupigwa vita kwenye vyombo vya habari, taifa haliwezi kufanikiwa katika harakati zake za kupambana na rushwa.

Shollei alisema biashara ya vyombo vya habari Tanzania ni kubwa ikilinganishwa na Kenya na Uganda kwa idadi ya magazeti yanayochapishwa kila siku, lakini linapowadia suala la maslahi ya taifa kila chombo kinakuwa na msimamo wake.

"Ushirikiano wetu unaweza ukapanuka kwa kufanya mafunzo ya pamoja na suala la gharama za uendeshaji. Lakini taifa la kidemokrasia haliwezi kuwepo kama vita dhidi ya rushwa haiwezi kuanza kwenye vyombo vya habari," alisema Shollei.

Alisema waandishi wa habari wa kampuni hizo watakapotambua jukumu na wajibu wao kwa jamii, itakuwa rahisi kwa serikali kupambana na vita hiyo na kuongeza: " Tunatakiwa kuhakikisha tunajikinga rushwa isitugawe".

Mhariri Mtendaji wa MCL, Theophil Makunga alisema, makubaliano hayo yanaweza kubadili mwelekeo wa habari Tanzania.

Naye Mhariri Mtendaji wa This Day, Evarist Mwitumba, aliwataka waandishi wa habari kuwa na moyo wa kukataa rushwa ili waweze kupambana nayo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian, Kiondo Mshana, alisema rushwa ziko nyingi kwenye vyumba vya habari na kwamba, baadhi huwa zinaandaliwa taratibu.

Akatoa mfano kwa kuhoji kumbwa mwandishi anapogombea ubunge anakuwa ameanzia wapi?
 
MCL, IPP zaungana kupambana na rushwa
Na Mwandishi Wetu
Gazeti la Mwananchi

KAMPUNI za Mwananchi Communications Limited (MCL) na IPP Media zimekubaliana kuunganisha juhudi za kupambana na rushwa kwa waandishi wa habari.

Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa jana na pande zote kwenye Hoteli ya Movenpick ni kuhakikisha waandishi wa kampuni hizo hawapokei 'bahasha' kutoka kwa watoa habari.

Hizi ni bahasha kama zile alizotoa EL.
 
It is the begining, lakini sijui kama itawezekana. Wakati waliokuwa respectable Journalists kama kina Salva Rweyamamu wamenunuliwa na wana mtanadao na kutumiwa vya kutosha halafu soon atatupwa. Ukisoma habari nyingi kwenye Majira, Mwananchi unaona wazi kabisa kuwa watu wameacha maadili ya uandishi wa habari wanatumiwa kuweka habari za kijinga za Lowassa na wanamtandao. Habari ambazo hata hazina mbele wa nyuma. Kama aibu hii imeonekana ni vizuri, lakini je Mengi, Mwananchi wanafanya efforts gani kuwafanya wafanyakazi wake wasipokee bahasha? Na miezi miwili iliyopita wakati EL alipoita wahariri na kuwapa bahasha za laki tatu, IPP na MCL hawakuwepo? au ni kwamba wanajaribu kutuzuga?
 
Hii inabidi iwe pact kwa wahusika wa MOAT wote. Na si ma publisher wawili tu, hata hivyo ni mwanzo mzuri wa kuigwa.

SteveD.
 
RA si anashares huko MCL?

Miye sijui, sina uhakika, Maggid kesha ondoka huko hakuna maana tena, zilizobakia ni Aibu ndani ya Aibu hivyo sijui pa kuuliza!,

Icadon, btw, a pact is a pact; shares cannot circumvent a treaty! Well, at least to my opinion.

SteveD.
 
Back
Top Bottom