Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Toka sakata la Bandari lianze nimepitia na kusoma sheria nyingi sana. Nikasoma na sheria mbalimbli za nchi nyingine. Nikagundua nchi haina sheria ya Uongo na upotoshaji wa umma.
Kwa nchi ya Tanzania unaweza kwenye vyombo vya habari ukasema uongo tu ambao si wa kichochezi na usiwajibike popote.
Kidogo serikali inajilinda na sheria ya Uchochezi. Kwa Tanzania ni ruksa kundanya Umma bila kuwajibikaji. Mtu anaweza kuhojiwa kuwa na mahusiano na mtu ambae hawajawahi kuonana bila kuwajibika. Akamletea madhara pamoja na msongo wa mawazo bila kuwajibika kwa lolote.
Kiongozi wa Umma anadanganya Umma tu bila wasiwasi wowote bila kujali madhara yake.
Kuna nchi za Ulaya hata ukigundulika una kimada unawajibika kabisa. Uongo kwenye mahusiano utaleta changamoto za kisaikolojia kwa na kupelekea uvunjifu wa sheria pamoja na mauti.
Nawashauri wadau wa sheria waje na hii sheria ili kulinda maadili ya jamii na kuepusha madhara ya kimwili, kiuchumi, kifedha kisiasa, na kijamii.