Tanzania: Ukosefu wa maadili unakosesha nchi maendeleo

GUI1

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
3,761
4,816
Habari wana bodi.

Nimejaribu kutafakali kuwa moja ya sababu inayo kosesha maendeleo ya nchi hii ni maadili, kivipi?

Ukichunguza kwa makini utajua kila kitu kina hitaji maadili na uungwana, Tanzania hapa kwa sasa kila kona kuna ukosefu wa maadili kuazia kwenye familia una kuta wazazi wengi hawana tena Sauti juu ya watoto wao lakini pia wazazi wenyewe mda mwingine hawa wajibiki ipasavyo kwa mahitaji ya watoto wao sababu inayo pelekea watoto kuwa juu ya wazazi wao.

Tukija kwenye siasa huku kila mtu anajua, ukosefu wa maadili umepelekea viongozi wengi kuwa wabinafsi walio pitiliza kiasi kwamba maslahi ya umma yanakuwa nyuma baada ya maslahi binafsi.

Kwenye dini pia tunaona kinacho kuwa kipaombele ni michango na sio imani tena, maombi huendeshwa kwa kuangalia kipato zaidi kuliko imani waliyo nayo watu.

Sasa ni nini kama nchi inatakiwa kufanya ni kuwa kwasababu watu wa nchi wengi hawana maadili na ungwana ina takiwa kuja na sheria kali zenye kutekelezeka kikamilifu.

Mfano nionavyo mimi wa zungu wamendelea kwa kuwa na sheria kali kwa kiasi flani. Bala Asia wana maadili na sheria kali ndio maana wametuacha kwenye maendeleo.

Karibu tujadili
 
China ukifisadi mali ya umma wanaondoka na kichwa chako! Daaadeki! Marekani baba wa demokrasia duniani ina wingi wa magereza kuliko shule na mahosipitali! Daaadeki! Uingereza mwanamke anasikilizwa na kuaminika kuliko mwanaume!

Ukipishana kauli na mwanamke akakuvutia waya njagu wakatia kipira moja kwa moja rupango mpaka uje kutolewa umeishaumia! Uingereza wanaume wanaogopa wanawake sio poa! Daaadeki!

Sasa hapa bongo mvunja sheria anaonekana mjanja! Shwaini!
 
China ukifisadi mali ya umma wanaondoka na kichwa chako! Daaadeki! Marekani baba wa demokrasia duniani ina wingi wa magereza kuliko shule na mahosipitali! Daaadeki! Uingereza mwanamke anasikilizwa na kuaminika kuliko mwanaume! Ukipishana kauli na mwanamke akakuvutia waya njagu wakatia kipira moja kwa moja rupango mpaka uje kutolewa umeishaumia! Uingereza wanaume wanaogopa wanawake sio poa! Daaadeki! Sasa hapa bongo mvunja sheria anaonekana mjanja! Shwaini!
Hii ni changamoto sana na sisi tuna chukulia poa sana lkn huyu ndio mchawi wa maendeleo yetu.
Kwasasa watu wengi hatufungamani na mila na desturi zetu za makabila wala maadili ya kidini. Kilicho baki kwenda kwenye nyumba za ibada ni fashion tu na kuonekana.
 
Back
Top Bottom