Zakamwamoba
Senior Member
- Jul 28, 2016
- 177
- 609
Kutokana kifo cha JPM, leo nilipata muda wa kutafakari mambo kadhaa.
Tafakuri yangu imenipa jibu kwamba Tanzania tumevamiwa na maadui kila kona.
Kitendo cha taarifa nyeti za Ikulu kuvuja mitaaani kabla ya taarifa rasmi maana yake kwamba kuna mamluki wengi wamejaa Ikulu. Picha ya jeneza la JPM ilianza kusambaa kabla ya taarifa rasmi ya kifo, hii ni hatari sana.
Sasa hivi imekuwa kawaida sana taarifa za siri ndani ya Serikali kuonekana mtaani. TISS wa siku hizi kazi yao kuvaa suti nyeusi na miwani kama wachomelea mageti lakini wengi wao wanakiuka viapo vyao.
Zamani mtu wa TISS kumtambua ilikuwa ngumu, ila siku hizi hadi wanajitambulisha wenyewe mitaaani hii ni hatari. Ushauri wangu ili Mama Samia afanye kazi vizuri, ni vema Ikulu isafishwe, maafisa wale wa zamani wote waondolewe. Kuanzia macamera man hadi walinzi wa getini otherwise mama atafanya kazi kwa presha sana.