Tanzania hatupo salama, Maadui wamepenya hadi Ikulu

Zakamwamoba

Senior Member
Jul 28, 2016
166
1,000
Kutokana kifo cha JPM, leo nilipata muda wa kutafakari mambo kadhaa.

Tafakuri yangu imenipa jibu kwamba Tanzania tumevamiwa na maadui kila kona.

Kitendo cha taarifa nyeti za Ikulu kuvuja mitaaani kabla ya taarifa rasmi maana yake kwamba kuna mamluki wengi wamejaza Ikulu. Picha ya jeneza la JPM ilianza kusambaa kabla ya taarifa rasmi ya kifo, hii ni hatari sana.

Sasa hivi imekuwa kawaida sana taarifa za siri ndani ya serikali kuonekana mtaani. TISS wa siku hizi kazi yao kuvaa suti nyeusi na miwani kama wachomelea mageti lakini wengi wao wanakiuka viapo vyao.

Zamani mtu wa TISS kumtambua ilikuwa ngumu, ila siku hizi hadi wanajitambulisha wenyewe mitaaani hii ni hatari. Ushauri wangu ili Mama Samia afanye kazi vizuri, ni vema Ikulu isafishwe, maafisa wale wa zamani wote waondolewe. Kuanzia macamera man hadi walinzi wa getini otherwise mama atafanya kazi kwa presha sana.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,273
2,000
TISS imeingiliwa na wana siasa. haswa chama tawala. ukishakuwa kada wanakusukumizia huko.. hawajali kuhusu qualifications.

zamani TISS walikuwa wana recruit smart peoples tu. na kazi za weledi zilionekana.
lakin sasa hivi makada ndio usalama..nmatokeo yake tunapata watumishi wasio na weledi.

na huu ni mwanzo.tu.
 

Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
721
1,000
Hii idara tangu ndege iziuwe kule Bondeni, tangu mahindi yazuiwe tangu nisikie Rwanda wanatengeneza simu ilihali maligafi zinapita bandari ya DSM bila kutoa taarifa na analysis mapema ili kuzuia au kuweka figisu tusipatwe na mabalaa nikajua kazi yao ni kubeba maboksi yaliojaa kura zilizopigwa tayari.
 

lolypop

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,077
2,000
Mkuu haya ni mambo ya kawaida sana kwenye system ya watu wengi. Bush na Bush Jr walimtafuta Osama zaidi ya 10yr bila mafanikio kosa Lao kubwa lilikuwa ni kushirikisha usalama wa taifa. Obama alifanikiwa kumpata baada ya kushirikisha watu wawili tu na yeye ni wa3. Vijana wakaanza mazoezi bila kufahamu wana mission gani.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,198
2,000
Tecnojia ndio inafanya mambo yavuje haraka, zamani mambo mengi yalikuwa kwenye makaratasi.

TISS walizuia kabisa watu kupiga picha mwili wa Magufuli lakini leo kuna video inasambaa ikionyesha mwili wa Magufuli ukiwa kwenye jeneza.

Jamaa inaonekana alivaa kamera kwenye miwani ,kofia ama koti.

Tecnolojia imekuwa juu Sana Hadi USA wanalia Kila siku kudukuliwa na Urusi.
 

masaka kwetu

Member
Jun 6, 2020
38
150
Mkuu unakuwa mjinga kidogo.
Watu wasiporidhika ni vigumu sana kuwanyamazisha...
Mwamba ameongelea ethics za TISS za sasa zimebadilika sana??, Yaani mtu yupo Ubelgiji ndo anatoa taarifa za mjomba?? Ni ukweli usiopingika kuwa kuna kundi la watu hapo TISS ndo wamempa taarifa huyo jamaa wa Ubelgijj. Na hii yote ni kuwa TISS na huku ni mwana CCM.

Awe CCM kwa kazi maalumu tuu. Lkn siyo kuwa kindakindaki. Tunaitaji kuwa na Strong institution na siyo strongmen. Pumuzika kwa amani mwamba JPM! UlichokifanyaTz!

Kwa kila m tz wa kweli na mwenye machungu na nchi yake ni lazima akulilie kwa uchungu. Kazi umeifanya JPM! Umeiyachia Tz heshima hapa duniani na kwa familia yako kwa ujumla.
 

Zakamwamoba

Senior Member
Jul 28, 2016
166
1,000
Mwamba ameongelea ethics za TIS za sasa zimebadilika sana??, Yaani mtu yupo ubelgiji ndo anatoa taarifa za mjomba?? Ni ukweli usiopingika kuwa kuna kundi la watu hapo TIS ndo wamempa taarifa huyo jamaa wa ubelgijj. Na hii yote ni kuwa TIS na huku ni mwana CCM...
Hakika,hii ni taasisi nyeti sana,inahitaji watu makini.Zamani hawa jamaa tulikuwa tunaishi nao mitaani miaka kumi lakin huwezi jua ni mtu wa TISS,lakin hawa wa siku hizi aaah tunawajua kabisa na ndio wanaotoa taarifa za ndani za Serikali. Kwa vyovyote vile ukiona taarifa za ndani za Ikulu zinasambaa ujue hatuko salama.
 

Zakamwamoba

Senior Member
Jul 28, 2016
166
1,000
Tecnojia ndio inafanya mambo yavuje haraka, zamani mambo mengi yalikuwa kwenye makaratasi.

TISS walizuia kabisa watu kupiga picha mwili wa Magufuli lakini leo kuna video inasambaa ikionyesha mwili wa Magufuli ukiwa kwenye jeneza.

Jamaa inaonekana alivaa kamera kwenye miwani ,kofia ama koti.

Tecnolojia imekuwa juu Sana Hadi USA wanalia Kila siku kudukuliwa na Uruss.
Wasaidizi wa Rais wana vifaa maalumu vya kunusa hatari,Wanaweza kudetect devices.Kitendo cha mtu kupita pale na Camera wakati walikataza jua hawa jamaa hawako makini.Any time hata Rais angeweza kuvamiwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom