Nampongeza Rais Samia na Serikali yake Kudhibiti uvujaji wa siri na Nyaraka za Serikali

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu watanzania,

Kuna kipindi kulikuwa Kuna washangaza wazalendo wengi Sana juu ya Uvujaji na usambaaji wa Siri na Nyaraka za Siri za serikali, watu walikuwa wanaona fahari kuvujisha Siri za serikali na Nyaraka za serikali, ilikuwa Ni kawaida kukuta na kuona mitandaoni habari nyeti za serikali. Nilikuwa najiuliza ujasiri huo ulikuwa unatoka wapi wa kufanya hayo mambo pasipo kuhukumiwa na dhamira zao juu ya viapo vyao.vikali kimaneno.

Ndugu zangu Ili ushinde Vita ya aina yoyote Ile Ni lazima uwe msiri wa mambo yako,mipango yako,mikakati yako na mbinu zako za kimedani. Huwezi ukaishinda Vita kwa kuandika Siri za jeshi lako hadharani utafikiri pumba za mashineni, mataifa yaliyoendelea na yenye nguvu za kijeshi, kiuchumi, kisayansi, kiteknolojia, kijasusi na kiinterejensia yamefanikiwa katika suala la utunzaji wa Siri na kuzilinda Siri za mafanikio Yao kwa jasho na Damu, hawana mchezo katika suala la Siri za Taifa na Nyaraka za serikali au vyombo vya ulinzi na usalama na mipango yake.

Ifahamike kuwa kuvujisha Siri na Nyaraka za serikali ni hatari kiusalama. Ni kulivua Nguo Taifa kwa kuwa inatoa mwanya kwa maadui zetu na wapinzani wetu wa kiuchumi na hata maadui zetu kiusalama kuweza kupata mahali pa kuanzia na kujuwa udhaifu wetu ulipo, wanapata kujuwa udhaifu wetu wa kutunza mambo yenye maslahi kwa Taifa letu na hivyo kuwa Rahisi kutuhujumu kiuchumi na hata kiusalama.

Kwa bahati nzuri Tangia ameingia madarakani mama yetu mpendwa kipenzi Cha watanzania, mama imara na shupavu. Jasiri na mzalendo wa kweli Mama Samia Suluhu Hassan kumeonekana kupatiwa dawa kwa Tabia hii mbaya iliyokuwa inataka kumea hapa nchini kwa baadhi ya watumishi, kwa Sasa watu wanashindwa hata kubashiri ni nani anaweza kuteuliwa katika nafasi fulani hata Kama mh Rais akisema kuwa anataka kufanya mabadiliko mahali fulani kwa wasaidizi wake, iwe Ni kwenye chama aliko Kama Mwenyekiti au serikalini ambako Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu amedhibiti Sana Uvujaji Wa Siri za serikali Hali iliyoleta utulivu serikalini na kuondoa Taharuki kwa wananchi, imeondoa presha na hata sintofahamu iliyokuwa ikitokea na maneno maneno.

Mimi Mwashambwa nikiwa Kama mzalendo na mpenda nchi yangu nawapongeza Sana wale wote waliokula viapo vya kutunza Siri mahali pa kazi kwa kuwa waadilifu na wenye kuzingatia viapo vyao, Nawasihi Kuendelea na moyo huo kwa maslahi mapana ya Taifa letu, kila mmoja wetu aliyepewa dhamana ahakikishe anatunza Siri za serikali kwa Kiwango Cha juu, kusiwepo kuishiwa uvumilivu katika suala la kiapo, Taifa letu Ni muhimu kuliko kitu kingine chochote, Na kila mtu ajione mwenye hatia inayostahili adhabu Kali ya majuto na majonzi avujishapo Siri za serikali.

Rai yangu kwa wahusika Ni kuhakikisha kuwa maafisa wote serikalini wanazingatia viapo vyao, isitokee hata kwa bahati mbaya mambo ya serikali yanatoka nje na kuleta Taharuki na kutetemesha usalama wetu, kila mmoja aliyepewa dhamani Ahakikishe anakuwa msiri ikiwezekana hata kufa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa letu kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo.

Hongera Sana Rais wangu, Umethibitisha uimara na ushupavu wako, umetoa dira na muelekeo wa serikali yako, mausia na maonyo uliyoyatoa hadharani yamezingatiwa na sisi watanzania Tumeona matokeo yake. Tunakuamini sana Rais wetu, tunakuunga mkono, tupo bega kwa bega na wewe, tunakupigania mitaani na kukusemea kila mahali.

Tunaendelea kukuombea afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia wananchi wako, Songa mbele kwa nguvu maana tulio upande wako Ni wengi zaidi ya wale walio kinyume na wewe kwa maslahi yao binafsi, umefanikiwa Kuiteka na kuitawala mioyo ya watanzania kwa uchapa kazi wako, ndio maana unaona utulivu na Amani ukiwa umetamalaki hapa nchini.

Kazi Iendeleee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
..hiki ulichoandika ni UJINGA.

..yaani wananchi kutokujua serikali yao inafanya nini unaona ni jambo la fahari?

..umewahi kusikia kitu kinaitwa " WHITE HOUSE TAPES " na zilivyokuwa msaada mkubwa kubaini uhalifu aliofanya Raisi Richard Nixon wa Marekani?

..kwanini wakubwa wawe na siri dhidi ya wananchi kama hawafanyi uhalifu au ufisadi?
 
Zipo Taarif ambazo hazipaswi kutok kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ulishawahi kusikia kiapo Cha mawaziri? Umewahi kusikia kiapo Cha viongozi wa ngazi mbalimbali katika vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama?
 
Hili boga sijui ni la wapi?
(•‿•)(•‿•)(•‿•)😃😃😃😃
Unampongeza kudhibiti kuvuja kwa Siri za serikali ukilinganisha na awamu ipi ambapo Siri za serikali zilivuja saña? Bila shaka utazungumzia utawala wa jiwe! Tutajie angalau Siri nne zilizowahi kuvuja unazozifahamu!

Hapa hatuzungumzii mikataba feki na ya kifisadi ambayo bila kujulikana tusingejua chawa wanavyoinyonya NCHI yetu mathalani Richmond na Dowans na escrow. Hizo sio Siri

Siri za serikali ni classified information tena katika level ya classified classified na sio confidential!
Kama ulishawahi kula kiaponcha kutunza Siri za serikali utajua maanisha Nini Ila kama Umekaa ukavimbiwa maharage hutaweza kutofautusha classified na classified classified information na classified vs confidential!
Nitakupa mfano;
Mtihani wa taifa unakua classified information na sio classified classified kwanini?
Unakua Siri tangu unavyotungwa mpaka unapoingia katika chumba Cha mtihani na Baada ya hapo unakua public kwa watu Fulani (watahiniwa na wasimamizi ) Baada ya matokeo kutoka unakua completely public ndio mana wasahihushaji BADO wanakula kiapo Cha Siri!
Sasa kwa Sababu una ubongo wa ndege siwezi kuendelea kukufafanulia juu ya classified classified na confidential!
Ngumbaru wewe ashakum si matusi unataka kumgombanisha Rais na awamu zilizopita zionekana zilifanya kazi kizembe!
 
Ziliwahi kutoka wapi sasa ndio useme mama amefanikiwa kudhibiti which means zilikua zinavuja sasa toa mfano wa hizo Siri zilivuja wapi! Kufanikiwa maana alikua anatatua tatizo umamsifia kwa mafanikio! Je Hilo tatizo lilikua lilikuepo awamu zilizopita? Acha uchonganishi
 
Hili boga sijui ni la wapi?
(•‿•)(•‿•)(•‿•)😃😃😃😃
Unampongeza kudhibiti kuvuja kwa Siri za serikali ukilinganisha na awamu ipi ambapo Siri za serikali zilivuja saña? Bila shaka utazungumzia utawala wa jiwe! Tutajie angalau Siri nne zilizowahi kuvuja unazozifahamu!

Hapa hatuzungumzii mikataba feki na ya kifisadi ambayo bila kujulikana tusingejua chawa wanavyoinyonya NCHI yetu mathalani Richmond na Dowans na escrow. Hizo sio Siri

Siri za serikali ni classified information tena katika level ya classified classified na sio confidential!
Kama ulishawahi kula kiaponcha kutunza Siri za serikali utajua maanisha Nini Ila kama Umekaa ukavimbiwa maharage hutaweza kutofautusha classified na classified classified information na classified vs confidential!
Nitakupa mfano;
Mtihani wa taifa unakua classified information na sio classified classified kwanini?
Unakua Siri tangu unavyotungwa mpaka unapoingia katika chumba Cha mtihani na Baada ya hapo unakua public kwa watu Fulani (watahiniwa na wasimamizi ) Baada ya matokeo kutoka unakua completely public ndio mana wasahihushaji BADO wanakula kiapo Cha Siri!
Sasa kwa Sababu una ubongo wa ndege siwezi kuendelea kukufafanulia juu ya classified classified na confidential!
Ngumbaru wewe ashakum si matusi unataka kumgombanisha Rais na awamu zilizopita zionekana zilifanya kazi kizembe!
😆😆😆😆 Nacheka kwa kuwa umenitukana kuwa Mimi kichwa changu Ni Kama boga 🤣🤣🤣 kila Siku unanitukana tu humu,hata oksijeni ungekuwa unagawa bila Shaka ungeninyima ili nife
 
huna akili.
Ni boga la kutupwa porini! Uozo mtupu!
Serious na mods mnaona juu nao ni Uzi! Huyu anachonganisha serikali zilizotangulia na hii ya mama!
Ameandika ujinga wakee sasa ameenda kwenye state issue kesho ataandika kumsifia mama anavyoishi ikulu ya chamwino au ile ya magogoni! Au namna JWTZ inavyoendesha intelligentsia ya kulinda mipaka! Mjinga huyu ashakum sio matusi
 
😆😆😆😆 Nacheka kwa kuwa umenitukana kuwa Mimi kichwa changu Ni Kama boga 🤣🤣🤣 kila Siku unanitukana tu humu,hata oksijeni ungekuwa unagawa bila Shaka ungeninyima ili nife
Boga sio tusi ni chakula Cha nguruwe kama ni la porini na Cha Binadamu kama ni homesteads pumpkins!
 
jibu hoja yake, siri gani hizo ziliwahi kuvuja na sasa hazivuji?.
Hawezi kujibu hakuna tangible issues anaandikaga huyu jamaa ni nadharia tu na mapenzi yake havipo anavyoongea
Na msingi wa bandiko lake na kikao Cha mama na watunza nyaraka ambayo ni field yake kule Arusha akiwakunbusha umuhimu wa kutunza nyaraka na Siri za serikali! Over na sio kwamba NCHI hii ilikua na tatizo la kuvuja kwa Siri za serikali kama alivyoandika huo utumbo wa ngurue kwa page kibao hapo!
Leo hao anaowaandikia number za simu wakimuita aseme Siri zipi za serikali zimewahi kuvuja hataweza kutaja HATA moja kwa kipindi Cha miaka mitano iliyopita achilia mbali huko nyuma!
Anaona serikali ni kama boma ya baba Ake anweza kuandika ushubwada tu na akapata milage!
We ishia kwenye mbolea na bara bara tu. Kuchamba kwingi Mwisho ni kushika mavi na ngoma ikilia sana Mwisho inapasuka!
 
Ndugu zangu watanzania,

Kuna kipindi kulikuwa Kuna washangaza wazalendo wengi Sana juu ya Uvujaji na usambaaji wa Siri na Nyaraka za Siri za serikali, watu walikuwa wanaona fahari kuvujisha Siri za serikali na Nyaraka za serikali, ilikuwa Ni kawaida kukuta na kuona mitandaoni habari nyeti za serikali. Nilikuwa najiuliza ujasiri huo ulikuwa unatoka wapi wa kufanya hayo mambo pasipo kuhukumiwa na dhamira zao juu ya viapo vyao.vikali kimaneno.

Ndugu zangu Ili ushinde Vita ya aina yoyote Ile Ni lazima uwe msiri wa mambo yako,mipango yako,mikakati yako na mbinu zako za kimedani. Huwezi ukaishinda Vita kwa kuandika Siri za jeshi lako hadharani utafikiri pumba za mashineni, mataifa yaliyoendelea na yenye nguvu za kijeshi, kiuchumi, kisayansi, kiteknolojia, kijasusi na kiinterejensia yamefanikiwa katika suala la utunzaji wa Siri na kuzilinda Siri za mafanikio Yao kwa jasho na Damu, hawana mchezo katika suala la Siri za Taifa na Nyaraka za serikali au vyombo vya ulinzi na usalama na mipango yake.

Ifahamike kuwa kuvujisha Siri na Nyaraka za serikali ni hatari kiusalama. Ni kulivua Nguo Taifa kwa kuwa inatoa mwanya kwa maadui zetu na wapinzani wetu wa kiuchumi na hata maadui zetu kiusalama kuweza kupata mahali pa kuanzia na kujuwa udhaifu wetu ulipo, wanapata kujuwa udhaifu wetu wa kutunza mambo yenye maslahi kwa Taifa letu na hivyo kuwa Rahisi kutuhujumu kiuchumi na hata kiusalama.

Kwa bahati nzuri Tangia ameingia madarakani mama yetu mpendwa kipenzi Cha watanzania, mama imara na shupavu. Jasiri na mzalendo wa kweli Mama Samia Suluhu Hassan kumeonekana kupatiwa dawa kwa Tabia hii mbaya iliyokuwa inataka kumea hapa nchini kwa baadhi ya watumishi, kwa Sasa watu wanashindwa hata kubashiri ni nani anaweza kuteuliwa katika nafasi fulani hata Kama mh Rais akisema kuwa anataka kufanya mabadiliko mahali fulani kwa wasaidizi wake, iwe Ni kwenye chama aliko Kama Mwenyekiti au serikalini ambako Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu amedhibiti Sana Uvujaji Wa Siri za serikali Hali iliyoleta utulivu serikalini na kuondoa Taharuki kwa wananchi, imeondoa presha na hata sintofahamu iliyokuwa ikitokea na maneno maneno.

Mimi Mwashambwa nikiwa Kama mzalendo na mpenda nchi yangu nawapongeza Sana wale wote waliokula viapo vya kutunza Siri mahali pa kazi kwa kuwa waadilifu na wenye kuzingatia viapo vyao, Nawasihi Kuendelea na moyo huo kwa maslahi mapana ya Taifa letu, kila mmoja wetu aliyepewa dhamana ahakikishe anatunza Siri za serikali kwa Kiwango Cha juu, kusiwepo kuishiwa uvumilivu katika suala la kiapo, Taifa letu Ni muhimu kuliko kitu kingine chochote, Na kila mtu ajione mwenye hatia inayostahili adhabu Kali ya majuto na majonzi avujishapo Siri za serikali.

Rai yangu kwa wahusika Ni kuhakikisha kuwa maafisa wote serikalini wanazingatia viapo vyao, isitokee hata kwa bahati mbaya mambo ya serikali yanatoka nje na kuleta Taharuki na kutetemesha usalama wetu, kila mmoja aliyepewa dhamani Ahakikishe anakuwa msiri ikiwezekana hata kufa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa letu kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo.

Hongera Sana Rais wangu, Umethibitisha uimara na ushupavu wako, umetoa dira na muelekeo wa serikali yako, mausia na maonyo uliyoyatoa hadharani yamezingatiwa na sisi watanzania Tumeona matokeo yake. Tunakuamini sana Rais wetu, tunakuunga mkono, tupo bega kwa bega na wewe, tunakupigania mitaani na kukusemea kila mahali.

Tunaendelea kukuombea afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia wananchi wako, Songa mbele kwa nguvu maana tulio upande wako Ni wengi zaidi ya wale walio kinyume na wewe kwa maslahi yao binafsi, umefanikiwa Kuiteka na kuitawala mioyo ya watanzania kwa uchapa kazi wako, ndio maana unaona utulivu na Amani ukiwa umetamalaki hapa nchini.

Kazi Iendeleee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Mapinduzi Zanzibar picha za watawala waliopo madarakani zimetamalaki kuliko picha za John Gideon Okello na wenzake. Abeid Karume aliyekuwa DSM siku ya mapinduzi anaitwa shujaa.

Umeweza kukubali kuwa kuna Tanzania bara na Zanzibar wakati ukweli ni Tanganyika na Zanzibar hii mtawala wanataka kuficha.

Wameshindwa kueleza Rasilimali zetu zina faida gani. Unawekwa ujinga kwenye siri za watu kutaka kuongoza kwa ufisadi.
 
Back
Top Bottom