Mazungumzo ya Rais Samia na Rais Ruto, Ikulu Dar es Salaam Oktoba 10, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ampokea na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya William Somoei Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Oktoba, 2022.



Mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na;

Rais Samia Suluhu Hassan
  • Kukuza na kuimairisha uhusiano kati ya Tanzania na kenya.
  • Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya biashara.
  • Mkutano wa tume ya pamoja ya mashirikiano ufanyike na kufanyiwa hatua kwa haraka.
  • Kuangalia zoezi la kuimarisha mpaka wa kimataifa kati ya nchi mbili hizi.
  • Mradi wa bomba la gesi kusafirisha gesi asilia Dar kwenda Mombasa, Kenya.
  • Kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyovuka mipaka, kama madawa ya kulevya, uharamia, ujangili na biashara haramu ya binadamu.
  • Kushikiana katika maswala ya kikanda na kimataifa kwenye Umoja wa Afrika na Afrika Mashariki.

Rais William Ruto
  • Kuhakikisha misingi iliyoachwa na Uhuru Kenyata kuwa inaendelea kuijengwa na Rais Samia ili kupeleka nchi hizi mbili mbele zaidi.
  • Kuongeza mahusiano ya kibiashara mara mbili zaidi kati ya Kenya na Tanzania.
  • Mawaziri wa Kenya wakishathibitishwa kuanza kufanya kazi, kazi yao ya kwanza itakuwa ni kufanya kazi na wenzao wa Tanzania, kuondoa vikwazo vilivyobaki kibiashara, JCC ifanyike Disemba ili biashara ziendelee vizuri na kukua zaidi kwa manufaa ya Kenya na Tanzania.
  • Bomba la kupeleka gesi kutoka Dar hadi Kenya wale wanaoshughulikia jambo hili kuharakisha na kuhakikisha linaisha haraka, ambapo litasaidia kupunguza ushuru wa nishati kwenye viwanda, kibiashara na matumizi ya kawaida ya nadni ili kuboresha maisha ya wananchi wetu na kuimarisha ushindani wa kibiashara.
  • Mambo ya utalii kati ya Kenya na Tanzania kuboreshwa, vizuizi vinavyokwamisha utalii kufanya vizuri kuondolewa.
  • Makubaliano ya kuwa na mtandao mmoja kwenye mawasiliano kwa nchi za Rwanda, Tanzania, kenya, S.Sudan na Uganda na sasa imebakia kufanyiwa kazi tu jambo hilo. Kufanya hivi biashara na uhusiano mzuri utaongezeka. Ni muhimu kwa gharama za mawasiliano kuwa nafuu ili kufanikisha biashara na mawasilano kuwa mazuri na kufanyika zaidi.
  • Makubaliano ya kushirikisha vitengo vya nchi hizi mbili katika kupambana na mambo ya uhalifu ambayo yanatoa majina mabaya kwa nchi zetu na kuhakikisha tunapunguza athari mbaya zinazoletwa na mambo haya ya kihalifu.
  • Nawahikikishia watu wa Tanzania mko na ndugu na jamaa zenu kutoka Kenya, tunataka kufanya kazi na nyinyi na kuhakikisha nchi zetu zinakua. Historia ya zamani ya mabishano tumeyaweka nyuma yetu, tunataka kutengeneza uhusaiano ambao utanufaisha pande zote mbili, na umoja wetu kwa ujumla.
  • Misingi uliyojengwa na watangulizi wetu kuanzia kwa Hayati Julius Nyerere tutahakisha inakuwa imara ili tuzidi kwenda mbele.

Mgeni.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto Zawadi ya Picha ya kumbukumbu mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Oktoba, 2022.

Kikao.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto pamoja na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Oktoba, 2022.

Kuagana.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku 2 Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Oktoba, 2022.​
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpokea na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya William Somoei Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Oktoba, 2022


Hii Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam mbona looks like a disserted facility?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom