John Kachembeho
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 560
- 389
- Thread starter
- #81
kwa hiyo kuruka na hizo parachute wanataka tuelewe nini hasa? Kwamba makomandoo wetu wapo fiti sana wanaruka kwa maparachute? Eti wanavunja mawe kwa vichwa, ili kumtisha nani? Hivi kweli waliyoyaonyesha yanatosha kujiridhisha juu ya ubora wao? Dunia ya sasa inaendeshwa kwa sayansi na teknolojia hivyo mbwembwe zote hizo ni kazi bure kama teknolojia ipo chini. sikatai umuhimu wa fitness kwa hawa mabwana ila tusiegemee huko zaid hakuna adui atakaye kuruhusu umsogelee daima atataka kukumaliza ukiwa mbali hivyo unapaswa kujipanga na kumkabiri akiwa mbali hivyo hivyo (teknolojia) wenzetu wana ndege zisizo na ruban ili kuhakikisha wanapambana na adui pasipo kuhatarisha maisha ya askar wao je sisi tuna kipi tunachotengeneza wenyewe? Tumeendeleza kwa kiasi gani yale magar tuliyokuwa tuna tengeneza?(nyumbu) Tuendeleze teknolojia yetu haya mambo ya kuruka na miamvuli kuwafurahisha raia hayana msingi ni sifa za kijinga. Wenzetu wanatuchora tu!
uko sawa tu pia!
Mara nyingi operations ambazo commandos wanakuwa assigned wanakuwa katika vikundi vya watu wachache sana, teknolojia inasaidia sana tu kukabiliana na adui ila huwezi ku-undermine human use kama vile ilivyo katika intelijensia huwezi kupuuza human intelligence (HUMINT) licha ya mahitaji ya teknolojia ya hali ya juu.
Chukulia mfano ulio wazi wa kukamatwa na kuuawa kwa Osama Bin Laden kule Pakistan, teknolojia ilitumika sana tu kufahamu alipo na nguvu around him lakini mwisho wa siku ni timu ya makomando iliyotumwa kwenda kutekeleza mission ya kumkamata/kumuua. Marekani licha ya kuwa na teknolojia ya juu mno (Drones etc) but still ina vikosi maalumu vingi tu vya ukomando.
Tusisahau pia pale uwanjani kwenye maonyesho lengo ni kutoa burudani, kuonyesha vitu interesting kufurahisha watu sio kutisha watu kwa kuua mtu pale!