Je mlitoa taarifa?mkapewa namba ya taarifa ngapi na namba yako ya simu
Aisee mie niliomba kufanyiwa survey mwezi wa nne mpaka leo ni dana dana tuu na nililipia fomu sh elfu 15, Cha ajabu Eng alienda mwezi uliopita afu kaniambia eti umeme single Phase kwa distance ya 1km haufiki. haikuniingia akili kabisaa
 
"BRAVO 2 ZERO, post: 24490990, member: 157159"]Ni lini hii huduma yenu itafika hapa, na wakati mji wa mbele ya maili 35 una umeme? Pia ni lini na tutajuaje kuwa ndo mnaleta umeme. Au sisi wananchi tufanye nini ili mlete hii huduma kwa haraka hapa maana ni shida tupu[/QUOTE]

Tafadhali tunaomba maelezo fasaha, kwanza fomu haikuwahi kuwa bei unayosema fomu ilikuwa tsh 5900 na sasa imeshafutwa. Ulilipa wapi hiyo na risiti ulipewa?

Aisee mie niliomba kufanyiwa survey mwezi wa nne mpaka leo ni dana dana tuu na nililipia fomu sh elfu 15, Cha ajabu Eng alienda mwezi uliopita afu kaniambia eti umeme single Phase kwa distance ya 1km haufiki. haikuniingia akili kabisaa
 
Naomba kujibiwa umeme Goba Kinzudi ubalozi wa Lipira, tunateswa sana na kitendo cha umeme kukatika katika na kuwa na low voltage. Kwa nini mnatufanyia hivyo jamani, tumewakosea nini?

Hatuna majenereta na inakuwa ngumu sana kuishi bila umeme. Tusaidieni please muongeze nguvu ya umeme
 
TANESCO,
Nawapongeza kwa ubunifu(creativity), tuliyoyaomba yanaonekana hata kama mtakuwa na matatizo lakini tusaidiane tujenge nchi.

Mimi nina ushauri na maswali yafuatayo:

1)Nashauri muweke number ya simu ya WhatsApp kwa sababu mimi niko nje ya nchi lakini nikijibiwa kwa whatsApp ujumbe nitaupata na nyinyi ni gharama nafuu hata kwa muda wenu.

2)Mimi nikiwa nje ya nchi mita ya Luku iliharibika-eneo la Kijitonyama,mafundi wakashindwa kuitengeneza lakini baada ya week 2 nikapewa nyingine ikiwa kwenye jina la mteja mwingine, je kuibadili kuna gharama?Na je naweza kupata mita ya luku mpya?maana hii tuliichukua lakini ilikuwa na tatizo la button moja.

3)Kwa mfano kwenye case mteja wenu kama alinunua nyumba ambayo kwa bahati mbaya muuzaji wa nyumba alimndanganya na hakumueleza kuwa TANESCO wanamdai umeme wa zaidi ya million 3.Je kuna utaratibu wa kumsaidia huyu mteja mpya kama ameshindwa kumpata huyo muuzaji na yeye anataka umeme?

Ahsanteni na kazi njema,
Rakey,

katabazi@hotmail.com
 
tengenezeni mfumo ambao mtu anaweza nunua umeme kwa njia ya mpesa, airtelmoney, tigopesa, halotelmoney n.k na ukaingia moja kwa moja kwenye mita yake kama ninavyoweza nunua vocha
 
TANESCO,
Nawapongeza kwa ubunifu(creativity), tuliyoyaomba yanaonekana hata kama mtakuwa na matatizo lakini tusaidiane tujenge nchi.

Mimi nina ushauri na maswali yafuatayo:
1)Nashauri muweke number ya simu ya WhatsApp kwa sababu mimi niko nje ya nchi lakini nikijibiwa kwa whatsApp ujumbe nitaupata na nyinyi ni gharama nafuu hata kwa muda wenu.
2)Mimi nikiwa nje ya nchi mita ya Luku iliharibika-eneo la Kijitonyama,mafundi wakashindwa kuitengeneza lakini baada ya week 2 nikapewa nyingine ikiwa kwenye jina la mteja mwingine, je kuibadili kuna gharama?Na je naweza kupata mita ya luku mpya?maana hii tuliichukua lakini ilikuwa na tatizo la button moja.
3)Kwa mfano kwenye case mteja wenu kama alinunua nyumba ambayo kwa bahati mbaya muuzaji wa nyumba alimndanganya na hakumueleza kuwa TANESCO wanamdai umeme wa zaidi ya million 3.Je kuna utaratibu wa kumsaidia huyu mteja mpya kama ameshindwa kumpata huyo muuzaji na yeye anataka umeme?

Ahsanteni na kazi njema,
Rakey,

katabazi@hotmail.com
1.tuna whatsApp group kwa kila eneo linalohudumia wateja wa eneo husika mfano Tegeta, Mikocheni, Mbezi nk ni ngumu kuwa na whatsApp ya Nchi nzima kwani namba ya members haizidi 256.

2.Mita ikabadilishwa inafungwa na jina la mwanzo la mteja labda aombe libadilishwe.kwa maandishi.

3.kununua nyumba yenyr deni maana yake umenunua na deni.hivyo ni wajibu wa mteja aliyenunua nyumba hiyo kulilipa kwani TANESCO haihusiki na makubaliano binafsi ya kuuza au kununua nyumba la msingi ni meter ambayo ipo kwenye nyumba.mita hiyo inakuwa kwenye uangalizi wa mteja mpya hivyo uharibifu wowote au deni lolote linuhusu mmiliki aliyenunua
 
Naomba kujibiwa umeme Goba Kinzudi ubalozi wa Lipira, tunateswa sana na kitendo cha umeme kukatika katika na kuwa na low voltage. Kwa nini mnatufanyia hivyo jamani, tumewakosea nini? Hatuna majenereta na inakuwa ngumu sana kuishi bila umeme. Tusaidieni please muongeze nguvu ya umeme
Tumelipokea kwa hatua zaidi
 
Naomba kuuliza inachukua mda gani mtu akilipia ili aingiziwe umeme kwenye nyumba ya kuishi? Mbeya mjini
 
TANESCO imekuwa ni kawaida kwa wakazi wa Pugu, kigogo, kipawa, buyuni, chanika, kukosa umeme mara kwa mara, ni kama tuko ktk mgao wa muda mrefu, Umeme unakatika kuanzia asubuhi na unarudi jioni,na wiki hizi umeme umekuwa unakatika usiku wa maneno mara kwa mara, tatizo ni nini haswaa?

Mbona kuanzia jeshini mpaka gongo la mboto umeme unakuwepo?
 
TANESCO imekuwa ni kawaida kwa wakazi wa Pugu,kigogo,kipawa,buyuni,chanika, kukosa umeme mara kwa mara, ni kama tuko ktk mgao wa muda mrefu,Umeme unakatika kuanzia asubuhi na unarudi jioni,na wiki hizi umeme umekuwa unakatika usiku wa maneno mara kwa mara,tatizo ni nini haswaa? Mbona kuanzia jeshini mpaka gongo la mboto umeme unakuwepo?
Ndugu mpendwa mteja
Taarifa imekuwa ikitolewa mara kwa mara dhidi ya eneo lako
 
Niawauliza Tanesco tumewakosea nini maeneo ya Buzuruga, Nyakato, Mwananchi ambapo umeme unazimwa kila siku saa mbili asubuhi mpaka saa moja jioni. Hii kweli nchi itakuwa nchi ya Viwanda?.
 
Huu ni mgao live hata wakikataa. Ukiwepo mchana usiku wana kata. Mkibahatika wakate mchana usiku wanarudisha. Hapa nilipo wamekata saa 12:30 jioni maana mchn hawakukata.
 
Naomba nisianze na salamu niende moja kwa moja kwenye mada husika kwasababu nina hasira sana.

Kiukweli kwa saivi tanesco mnaboa hii imeniuma sana na ninaomba kama wahusika wapo hatua kali zichukuliwe kwa viongozi wa eneo lote la kisarawe na kanda jirani hadi maeneo ya Pugu. Ikiwemo hata adhabu ya kupiga mnada nyumba zao.

Ni kitu kinaudhi na kuboa ati kwa siku umeme unakatika zaidi ya mara sita. Yaani naomba muelewe sio kukatika mara moja ni mara sita yani kata na kurudisha.


Hivi mnajua hasara mnayoisababisha au huwa mnakata tu kwa kujua kuna manyani yanaishi huku hayana hata friji. Na hata tukikata hayatufanyi kitu. Mnajua mmeshaniunguzia vitu vingapi mpaka saivi?.
Computer yangu ndio maisha yangu naitumia kuandikia report mbalimbali afu naitumia direct from Power source Sasa swali ni moja mnapokata mnahisi kila mtu ana power saver. ? Naomba mnijibu maana msilete masihara
leo mmeniunguzia kabisa computer yangu mpaka saivi haiwaki na kesho natakiwa niwasilishe taarifa officini.
Hivi kuna boss atakubali nikimwambia umeme ulikatiaka asee.

Hebu kueni na heshima wakati mwingine kateni umeme kistaarabu mnakata mara sita mpaka kumi kwa mchana tu Sasa na usiku sijui inakuwaje.

OK OK. Basi mkiwa mnakata toeni taarifa kabla kuwa kesho kaeni macho umeme utakatika mara saba hadi nane. Msiwashe TV wala chombo cha umeme asee ingesaidia kidogo. Sasa mnakurupuka tuu huko sijui mmenyimwa posho mnaambizana leo tuwalipizie tukate mara nane tuwakomeshe.

Aaaah jamani hatuendi hivyo aseee.

Hebu kumbukeni ule mwaka umeme ulipokatika pale U. K kwa dakika 8 .jinsi shirika lilivyoingia hasara ya kulipa fidia ya mamilioni ya shilingi kuwalipa fidia wananchi waliopetelewa na mali zao.
Huo ni mfano mmoja tu mnatakiwa mjifunze na mfanye vitu vyenu kwa heshima za watu.

Naamini wenyewe mmenisikia na naamini kesho hamtakata kama leo.
 
Back
Top Bottom