TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Shirika limejifia. Mnatutia hasara kati ka kazi zetu. Hata tukiseka ni maharage na January wamewapiga show bado itakuwa sio sababu. Achaneni na kuzalisha umeme mfanye mambo mengine.
 
Nahitaji kubadilishiwa mita kutoka mita ya zamani kuja hizi mita ndogo wakuu
 
Tanesco eneo la chanika (ILALA) Kuna shida gani? Mteja anafanyiwa survey then anakaa Zaid ya miezi miwil hamtoi control number kwa madai hakuna nguzo, je mna uhaba wa nguzo kiasi hiko?? Wateja wengi wanalalamika
 
Kuna taarifa kwamba Tarifu 4/D1 imefutwa na kila aliyekuwa analipia umeme kwa rate ya tarifu hiyo atapangiwa tarifu 1.
Tanesco je, hii taarifa ni ya kweli?
 
Kuna vijana wanajihusisha na uharibifu wa miundo mbinu yaTANESCO na TTCCL vijana hawa wanapatikana Nyerere road reli itokayo ghala la hifadhi ya chakula NFRA maarufu BODI katika uchunguzi wangu vijana hawa walichimba katika eneo lililo karibu na Toyota Tanzania baada ya kuchimba huvuka ngambo ya barabara na kuichoma hiyo miundombinu wenyewe huita Kopa Copper, nilipata majina yao kwa mama ntilie aliye karibu na hilo eneo majina yao ni kama ifuatavyo Kiongozi mkuu 1: Musa maarufu Muha Kidari, Mkurya maarufu Shamte, Zakayo, Sharo, White, nitaleta majina mengine kadri nitakavyofuatilia.
 
Back
Top Bottom