*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO*

*TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU MKOA WA TABORA*
Shirika la umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Tabora, linapenda kuwataarifu wateja wake wote wa manispaa ya Tabora kuwa kutakuwa na kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya umeme siku ya jumanne ya tarehe 26/09/2017.

*MUDA* Kuanzia saa 3:00 asubuhi_11:00 jioni.

*MAENEO YATAKAYOATHIRIKA*
Bara bara ya Boma, Ofisi ya mkuu wa mkoa Tabora, Ofisi ya mkuu wa wilaya Tabora, Uhazili, VETA, Kwa Mrema, Majumba 40 JWTZ, Shule za wasichana na Wavulana Tabora, Kariakoo, Uwanja wa ndege, Cheyo A, Cheyo B, Malabi, Isevya, Bomba mzinga, Rada, Ipuli na bwawa la Kazima.

*TAHADHARI*Tafadhali usiguse, usikanyage wala usishike waya uliokatika maana ni hatari kwako.

*MAWASILIANO* Piga dawati la dharura:
0788 684535, 0786 558 810,
KITUO CHA MIITO MAKAO MAKUU: 0222194400/0768 985 100
*TOVUTI* www.tanesco.co.tz

*TANESCO INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA*

*IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO HUDUMA KWA WATEJA TANESCO MKOA WA TABORA.*
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEMEMKOA WA TEMEKE

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya matengenezo ya njia ya ya msongo mkubwa wa 132kv kutoka Kurasini-Mbagala iliyolenga kuimarisha ubora na upatikanaji wa umeme Siku ya Jumanne, tarehe 26Sept,2017 kuanzia saa 02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 jioni

Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Mbagala yote, baadhi ya maeneo ya yombo, Kimbangulile, Kiburugwa, kilungule, Kingugi, maeneo yote ya Chamazi, Mzambarauni,kijichi, Nyumba nyeupe, Mbande Kiponza, Mbande Bamia, Zakhem, Kizuiani, Rangi tatu, Mbande Kisewe, Nzasa, hospitali ya Rangi tatu, kiwanda cha Dar steel, kiwanda cha maji poa, ukumbi wa Darlive, Am steel, karibu textile mills, East afrc polybagy, avant industry, camel cement, SD plastic Epz ltd,

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400/0768 985 100.

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano kwa wateja
TANESCO-TEMEKE
 
Tanesco tanesco nimeshindwa kuwaelewa,,,au mnataka pesa?ni week ya pili sasa tangu waisimike nguzo kwaajili ya kunivutia umeme lkn hawajaniunganishia mini tatizo au niwape pesa?
 
Tanesco, huku Mtwara mbona katakata imekuwa nyingi sana yaani ndani ya masaa mawili umeme unakatika na kurudi zaidi ya mara tatu, na ukatikaji huwa siyo wa kistaarabu yaani umeme unaanza kwa kupungua nguvu kisha ndiyo unakatika.

Nini tatizo? Toeni hata matangazo basi tujue kinachoendelea.
 
Nipo Tabata dampo mkoa wa Dar es salaam wilaya ya ilala matumizi yangu ya umeme wastan kwa siku moja ni unity 1

Kwa mwezi ni unity 30 Sijawahi kufikisha hata unity 35 kwa mwezi tokea nimeanza kutumia umeme wa mita ya Luku huu sasa ni mwaka wa 2
TANESCO mnasema ukiwa huko chini ya unity 75 nenda ofisi ukaandike barua ya kubadilishiwa Tarif kutoka Tarif 1 kwenda tarif 4 kama ukikidhi vigezo utabadilishiwa

mimi nilikwenda ofisi za TANESCO Tabata Liwiti nikaandika barua ,mara ya kwanza meneja aligoma kupokea barua yangu alisema barua za maombi zipo nyingi sana
Nilitumia akili ya ziada nikaingia ofisi nikawasilisha maombi yangu
Yule mdada pale ofisini sijui alinizuga ,nimeona kabisa kawasha computer akaniambia swala lako tunalifanyia kazi
Tangu siku ile ni kimya kabisa mbaka nimekata tamaa

Kifupi swala la kubadilisha tarif kwa wale tunaotumia umeme chini ya unity 75 ni kizungu Mkuti ukisoma humu maneno yao watu wa TANESCO ni ya kukupa matumaini ila usithubutu kwenda ofisini kwao kulalamikia hili utapigwa sound tu,

Utekelezaji wake ni mgumu sana kwa sababu wao wanafanya biashara ya kutudhulumu sisi wananchi
Ukiwa tarif 4 sh elfu 10 ni unity 70 wakati ukiwa tarif 1 sh elfu 10 ni unity 28 unafikiri TANESCO watakubari kubadilisha tarif ili wapate hasara
Nawasilisha.
 
TANESCO mnasikitisha katika kutoa kipa umbele kwenye matatizo yanaporipotiwa. Nimekuwa mhanga wa kutoshughulikiwa tatizo langu mbali ya kutoa kwangu taarifa zaidi ya mwaka na nusu sasa.
Katika chuma ya juu ya paa langu la nyumba linalopokea umeme kuingiza ndani kuna loose connection. Hii inapelekea kila pakitisika kidogo na upepo umeme hukatika ama cheche kutoka. Zaidi ya mwaka na nusu nimetoa taarifa katika ofisi za wilaya ya Ilala pasi kupata msaada wowote.
Mimi sio fundi lakini nina hakika si jambo kubwa kurekebisha ila limekuwa na uzito tu katika kutekeleza. Kuna mpaka mmoja wa vijana wa TANESCO alidiriki kunambia nitoe kitu kidogo ili tatizo langu lishughulikiwe. Sasa nashangaa kidogo hicho nikitoe vipi katika jambo ambalo kila siku mnaimba kuwa ni bure.
Mita namba yangu ni 22132264494.

Mtaa Kilosa No. 6, Ilala Dar es Salaam.

0715 286 322.
 
Mkuu tunaomba radhi kwa hili, tatizo lako linashughulikiwa mara moja
 
Nipo Tabata dampo mkoa wa Dar es salaam wilaya ya ilala
matumizi yangu ya umeme wastan kwa siku moja ni unity 1
Kwa mwezi ni unity 30
Sijawahi kufikisha hata unity 35 kwa mwezi tokea nimeanza kutumia umeme wa mita ya Luku huu sasa ni mwaka wa 2
TANESCO mnasema ukiwa huko chini ya unity 75 nenda ofisi ukaandike barua ya kubadilishiwa Tarif kutoka Tarif 1 kwenda tarif 4 kama ukikidhi vigezo utabadilishiwa
mimi nilikwenda ofisi za TANESCO Tabata Liwiti nikaandika barua ,mara ya kwanza meneja aligoma kupokea barua yangu alisema barua za maombi zipo nyingi sana
Nilitumia akili ya ziada nikaingia ofisi nikawasilisha maombi yangu
Yule mdada pale ofisini sijui alinizuga ,nimeona kabisa kawasha computer akaniambia swala lako tunalifanyia kazi
Tangu siku ile ni kimya kabisa mbaka nimekata tamaa

Kifupi swala la kubadilisha tarif kwa wale tunaotumia umeme chini ya unity 75 ni kizungu Mkuti ukisoma humu maneno yao watu wa TANESCO ni ya kukupa matumaini ila usithubutu kwenda ofisini kwao kulalamikia hili utapigwa sound tu,
Utekelezaji wake ni mgumu sana kwa sababu wao wanafanya biashara ya kutudhulumu sisi wananchi
Ukiwa tarif 4 sh elfu 10 ni unity 70 wakati ukiwa tarif 1 sh elfu 10 ni unity 28 unafikiri TANESCO watakubari kubadilisha tarif ili wapate hasara
Nawasilisha.
Tunaomba mita namba na namba yako ya simu tafadhali
 
TANESCO habari, Mimi ni mkazi wa wazo ninatumia umeme wa Tanesco nilikua nahitaji kufunga mita ya pili kwenye nyumba yangu, je narusiwa kufanya ivo? naomba utaratibu kama inawezekana.
 
TANESCO habari, Mimi ni mkazi wa wazo ninatumia umeme wa Tanesco nilikua nahitaji kufunga mita ya pili kwenye nyumba yangu, je narusiwa kufanya ivo? naomba utaratibu kama inawezekana.
Inaruhusiwa bila tatizo, unafika ofisi ya tegeta na kupewa maelezo pamoja na fomu.

Gharama inakuwa ni ile ile 320,960 pamoja na Vat na unatikiwa kutengenisha mitandao ya umeme au wiring yako ili mita mpya iweze kujitegemea kwa main switch
 
Za mda huu,kama kichwa cha habari kinavyojieleza..

Watu wengi kwa namna moja au nyingine tunaishi maisha ya kupanga, kwa sababu unaweza kuwa na nyumba yako ila duka au kazini umepanga...

Kwa sababu hiyo mara nyigi huwa kunatokea mgogano wa ulipaji umeme hasa pale unapokuwa na watu wenye matumizi tofauti tofauti.mfano baadhi ya wapangaji wana-fridge zaidi ya moja na wengine hawana kabisa na wanatumia umeme kwa taa,redio na kuchaji simu,lakini bill inawataka kulipa kiwango sawa.

Kibaya zaidi mtu anaweka meter reader yake na anagundua umeme anaotumia haufiki hata robo ya anaolipa.hapo ndio kelele za wapangaji zinapoanza kuhusu umeme na akiwa mtu ni mkorofi anagoma kulipa hali ni zamu yake

Kwa sababu hizo ni bora TANESCO ikaweka utaratibu wa MTU kuwa na meter yake hata kama hana nyumba yake ili pale anapohama ahame nayo akatumie huko anakohamia hiyo itapunguza kero za umeme kwa wapangaji,maana wenye nyumba wengi hawezi kufunga meter kila chumba....

Naamini utalifikilia
 
kunakifaa cha kuonesha wewe unatumia umeme wa kiasi gani ili ulipe kutokana na unavyotumia waulize tanesco vizuri
 
Wakiweka meter kwa kila mpangaji basi wata double cost umeme wao mnaotumia..awamu ya 5 inataka kukusanya makwenje tu hawashauriki wala hawajaribiwi teh teh
 
kunakifaa cha kuonesha wewe unatumia umeme wa kiasi gani ili ulipe kutokana na unavyotumia waulize tanesco vizuri
Mku hicho kifaa kabala sijahamia kwangu kilikuwa shida maana wapangaji waliokimbia umande hawaelewi kitu wao wanaona umechezea. Na lazima pia uchangie. Mikataba ya wenye nyumba pia ni kero. Inasema huduma za umeme na maji zitachangiwa.

Imagine wewe ni bachelor unatumia ndoo moja ya maji kwa siku tatu, halafu mpangaji mwenzio ana familia halafu anatumia ndoo kumi kwa siku. Bili ya maji ikija mnachangia sawa.

Jikwamue Ujenge. Japo kujenga sio mwiaho wa kupangisha.
 
Back
Top Bottom