TANESCO inasikitisha sana kuwa mnachukulia kwa wepesi sana kero za wateja.
Mimi ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar. Mnamo tarehe 14 kuamkia tarehe 15 mwezi huu, kulitokea hitilafu ya umeme kupelekea kukatika umeme eneo lote. Ila baada ya kurudi umeme, kwangu pekee kulikuwa hakuna umeme.
Ikanilazimu kwenda Ukonga Madafu ofisi za Tanesco, hapakuwa na mtu isipokuwa mlinzi alienipa namba ya Emergency. Nilipopiga niliongea na mtu anaitwa
Zuhura, alinipatia
Reference Number 3626 na kunambia mafundi watakuja. Ni kweli mafundi wa 3 walikuja na kusema mita yangu yenye namba
24218573269 imeungua hivyo itabidi kubadilishwa. Ikae kwenye rekodi kuwa mita hii ni ya pili kuungua.
Mafundi walinambia wanapeleka ripoti ofisini na itakuja kubadilishwa. Baada ya kuona kimya, nikapiga tena Emergency number na kuzungumza tena na Zuhura, akanambia tatizo langu linashughulikiwa. Izingatiwe hapo pote mpaka muda huu sina umeme, naishi kwenye giza.
Nikajaribu tena kupiga Emergency number na safari hii muhudumu akaniambia nitapigiwa na mtu kutoka makao makuu. Na kweli nikapata simu kutoka kwa mtu anaitwa
Lucas Mwala, lakini kwa mujibu wa Bw. Mwala ni kuwa ripoti waliyokuwa nayo ni kuwa tatizo langu limekwisha hivyo nifuatilie upya kwa mafundi.
Sasa
TANESCO hamuoni mnaofanya ni huduma mbovu? Ninaishi bila ya umeme kwa takriban siku 6 sasa na hakuna jibu la maana ninalopata. Je tunapaswa tufuatilie wapi ili matatizo yetu yatatuliwe? Ikiwa ni kweli mafundi wenu wanatoa ripoti batili, je tunapswa kuwa na imani nao wakija kuangalia matatizo?
Kama kuna muhusika hapa tafadhali naombeni msaada maana sasa imeshakuwa adhabu.
Ahsante
0784 366 654
0784 416 504