TANESCO
Official Account
- Jul 12, 2014
- 5,172
- 2,733
- Thread starter
- #9,961
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)Tangu jana mnaonekana mna shida kwenye kununua luku. Baada ya ucheleweshaji nimepata token. Ila napoingiza umeme hauingii. Je hii itakuwa ni shida gani?
TANESCO
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU KWA BAADHI YA WATEJA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.
Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.
Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya kijamii
Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu
Facebook Tanesco Yetu
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Mei 18, 2021.