TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
2,030
Points
2,000

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
2,030 2,000
Tanzania_Electric_Supply_Company(TANESCO)_logo.png
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;

LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.

NAMBA ZA SIMU ZA MADAWATI YA DHARURA YA TANESCO MIKOA YOTE

1. Ilala

0222133330/ 0784 768586/ 0715 768586.

2.Kinondoni Kusini (Magomeni)

0784271461/ 0715271461

3. Kinondoni Kasikazini(Mikocheni)

0784 768584/ 0716 768584

4. Temeke

0222138352/ 0732 997361/ 0758881055/ 0712 052720

5. Pwani
078 5122020/065 7108782/023 2402386

6. Mbeya
0759 777781/0787 023422


7.Arusha
0758174343/
0622612501/
+255 27 2506110

8.Tanga
0658 122 412/0687 677 667/ 027 2646 779

9. Kilimanjaro
0765 397 925/0682 771 310/ (+255) 272 755 007/8

10 Manyara
0689 795 599/ 0627938951

11. Mwanza
0759 777 786/0687 910 202/
(+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

12. Geita
0744 085 696/(+255) 28 2520330

13.Kagera
078 5 787 898 / 075 3 120 701/(+255) 282 220 061

14.Mara
0788 950 688/
028 262 2020/
0762 165 087

15.Simiyu
+255 282 700 180/0626383440/0745044072

16. Dodoma
0782 161 643/(+255) 262 321 728

17. Morogoro
068 4889272 /065 4829046/ (+255) 232 613 501/2

18 Singida
071 4 477 445 /0732 960 924 / 0689 373 757/(+255) 262 502 133

19. Tabora
0786 558 510 /0763 162 868

20. Shinyanga
0754 521 070/(+255) 28 2762120 /
0783 521 070

21. Kigoma
078 3720598/(+255) 2988226

22. Katavi
0688345200

23. Rukwa
0252161120/0768879813
24. Songwe
0684 611716/0763 430381.

25. Ruvuma
0252602281/0763 194 979/0787 758 986

26. Njombe
0744703988

27. Mtwara:
0789 999942/023 2333902

28. Iringa 0262702019/0739203015

29. Lindi
0752518247/0685692786


Kituo cha Miito ya simu/Call Centre Makao Makuu

0768 985 100/0222194400

Facebook
www.facebook.com/tanescoyetu

Twitter
www.twitter.com/tanescoyetu

Tovuti
www.tanesco.co.tz

Barua pepe
Customer.service@tanesco.co.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
2,030
Points
2,000

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
2,030 2,000
Jana (10 June, 2019) tulinunua umeme wa luku (mita namba 43002630549) na kupewa units 16-kwa TZS 5900-badala ya 48 units za mwanzo kwa kuwa umepita mwezi na siku kadhaaa tangu tununue wa hapo awali. Sijajua tatizo ni nini?
Lakini pia, kila tukijaribu kuingiza token za unit 16 tulizopewa kwenye mita hiyo, inagoma kujibu na badala yake inaendelea kuandika unit 0.0
Je, sababu ni nini?
5397 8789 8197 1556 4421
 

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Messages
1,379
Points
2,000

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2013
1,379 2,000
5397 8789 8197 1556 4421
Yap! token ndiyo hizo, ila tuliwasiliana kwa kutumia namba yenu ya huduma kwa mteja na walirekebisha activation number ya mita ambayo ilionekana imekosewa. Tumefanikiwa kuingiza token hizo na mita sasa inasoma 16.6 units.
Sasa swali linabaki kwa nini tumepewa units 16.6 badala ya 48 kwa TZS 5900 kama ambazo tulikuwa tukipewa? Na tangu tununuwe umeme kabla ya Jana, umepita mwezi na siku kadhaa.
 

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
2,030
Points
2,000

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
2,030 2,000
Yap! token ndiyo hizo, ila tuliwasiliana kwa kutumia namba yenu ya huduma kwa mteja na walirekebisha activation number ya mita ambayo ilionekana imekosewa. Tumefanikiwa kuingiza token hizo na mita sasa inasoma 16 units.
Sasa swali linabaki kwa nini tumepewa units 16.6 badala ya 48 kwa TZS 5900 kama ambazo tulikuwa tukipewa?
Mtakuwa mmeshanunua zaidi ya unit 75 kwa mwezi
 

Mkiramussa

New Member
Joined
Feb 2, 2019
Messages
2
Points
45

Mkiramussa

New Member
Joined Feb 2, 2019
2 45
TANESCO mjitathimini uendeshaji wenu wa shirika kwani ni miaka na miaka sasa imepita tatizo la kukatika umeme imekuwa kero utadhani ndo SERA YA TAIFA.

Ifike wakati tuache mazoea,umeme ndo kila kitu katika ukuaji wa uchumi wa nchi nyingi dunia kwan big investment zinategemea sana umeme lakini pia hata watu wa kawaida wanategemea umeme kuingiza kipato na kipato kinavyoingia kwa mtu mmoja mmoja ndio uchumi unakuwa lakini pia stability ya umeme inavutia wawekezaji.
Naomba niwakumbushe Rais wetu alisema hii ni Tz ya viwanda je na nyinyi mnalijua hili?? Ukizungumzia kiwanda unazungumzia na umeme.

Kwa kuhitimisha tuache mazoea kazini,tuwe wabunifu and tutumie elimu zetu kwa ndugu zetu wa Tz kwa mustakabali wa taifa hili linaloendelea.
Umeme hapa moshi unakatika katika sana
 

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Messages
1,364
Points
2,000

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2013
1,364 2,000
aisee waheshimiwa hapa tegeta mivumoni kuna matatizo gani???? umeme siku ya tano leo ukikatika asubuhi ni hadi saa 12, SASA HAPA NAFANYAJE KAZI NA COMPUTER IMEISHA CHARGE??? YAANI MNANIKOSESHA HELA NYIE JAMAA MUNGU ANAWAONA NYIE.....
 

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2018
Messages
981
Points
1,000

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2018
981 1,000
Tanesco jana Jumanne tarehe 11 mwezi wa sita mwaka 2019 tulinunua umeme wa sh 5,000, nadhani utakua wa sh 4,900 maana hua wanakata sh 100, lakini kwa bahati mbaya ile karatasi tuliipoteza stend wakati wa kumpokea mgeni, tunaomba msaada wenu, namba ya mita 37210012797 jina Williamu Ole Mungaya.
 

kupukupu

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2016
Messages
399
Points
1,000

kupukupu

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2016
399 1,000
TANESCO huu uhuni mliotufanyia leo watu wa sumbawanga ukome, mnapata wapi ujasiri wa kutukatia umeme zaidi ya masaa 8 bila kutupa taarifa? Tena iwe mwisho, hii huduma ya umeme hamtupi bure tunanunua huu ujinga ujinga wa kukatia watu umeme bila taarifa ikome kuanzia leo.

Sisi watu wa sumbawanga hatujazoea huu ujinga ujinga mnaotaka kutuanzishia masaa 8 kwetu ni mengi mno hatujazoea hata kidogo, huo utoto wenu wafanyieni hao hao vijana wa dar maana wao hata mkiwakatia wiki hawawezi kufanya kitu.

Nasisitiza hili suala lisijirudie tena iwe mwisho leo, huo upuuzi wenu wafanyieni hao ambao mlishawazoesha.
 

Rchesse

Member
Joined
Apr 23, 2019
Messages
45
Points
95

Rchesse

Member
Joined Apr 23, 2019
45 95
Wilaya ya Tarime hivi kuna nini maana karibia mwezi wa pili huu umeme unakatika kila siku mara 3 hadi 4, na sio kwa muda mfupi ni kwa masaa. Mfano unawashwa kwa nusu saa, halafu wanakata kwa masaa 5 unarudi kwa dakika 20 unakatika kwa masaa 4. Na siku nyingine kama juzi na jana umekatika kwa siku nzima (masaa kama 20 hivi). Hata apa ninapoandika hivi hamna umeme. Kama ni hivi, nini maana ya kuwa na umeme si bora mngefungua hii mitambo yenu tujue kabisa hamna umeme wilaya ya Tarime. Hata taarifa hawatoi. Watu watafanyeje biashara kwa hii hali?.
 

Forum statistics

Threads 1,345,287
Members 516,220
Posts 32,852,267
Top