TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri


TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
1,680
Points
2,000
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
1,680 2,000
tanzania_electric_supply_company-tanesco-_logo-png.498143
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;

LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.

NAMBA ZA SIMU ZA MADAWATI YA DHARURA YA TANESCO MIKOA YOTE

1. Ilala

0222133330/ 0784 768586/ 0715 768586.

2.Kinondoni Kusini (Magomeni)

0784271461/ 0715271461

3. Kinondoni Kasikazini(Mikocheni)

0784 768584/ 0716 768584

4. Temeke

0222138352/ 0732 997361/ 0758881055/ 0712 052720

5. Pwani
078 5122020/065 7108782/023 2402386

6. Mbeya
0759 777781/0787 023422


7.Arusha
0758174343/
0622612501/
+255 27 2506110

8.Tanga
0658 122 412/0687 677 667/ 027 2646 779

9. Kilimanjaro
0765 397 925/0682 771 310/ (+255) 272 755 007/8

10 Manyara
0689 795 599/ 0627938951

11. Mwanza
0759 777 786/0687 910 202/
(+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

12. Geita
0744 085 696/(+255) 28 2520330

13.Kagera
078 5 787 898 / 075 3 120 701/(+255) 282 220 061

14.Mara
0788 950 688/
028 262 2020/
0762 165 087

15.Simiyu
+255 282 700 180/0626383440/0745044072

16. Dodoma
0782 161 643/(+255) 262 321 728

17. Morogoro
068 4889272 /065 4829046/ (+255) 232 613 501/2

18 Singida
071 4 477 445 /0732 960 924 / 0689 373 757/(+255) 262 502 133

19. Tabora
0786 558 510 /0763 162 868

20. Shinyanga
0754 521 070/(+255) 28 2762120 /
0783 521 070

21. Kigoma
078 3720598/(+255) 2988226

22. Katavi
0688345200

23. Rukwa
0252161120/0768879813
24. Songwe
0684 611716/0763 430381.

25. Ruvuma
0252602281/0763 194 979/0787 758 986

26. Njombe
0744703988

27. Mtwara:
0789 999942/023 2333902

28. Iringa 0262702019/0739203015

29. Lindi
0752518247/0685692786


Kituo cha Miito ya simu/Call Centre Makao Makuu

0768 985 100/0222194400

Facebook
www.facebook.com/tanescoyetu

Twitter
www.twitter.com/tanescoyetu

Tovuti
www.tanesco.co.tz

Barua pepe
Customer.service@tanesco.co.tz

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
tinkanyarwele

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Messages
1,220
Points
2,000
Age
47
tinkanyarwele

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2016
1,220 2,000
Tanesco jamani mimi nimenyoosha mikono kupata umeme kwenu imekuwa ngumu sana siku nikipata nauli itabidi niwafuate huko Darisalama
 
Code Breaker

Code Breaker

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
1,010
Points
1,500
Code Breaker

Code Breaker

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
1,010 1,500
Habarini za kazi, katika kijiji cha Munjebwe, Rulenge Ngara, nguzo za umeme HT zimepita upande wa pili wa barabara approx. 150 m, na upande wa pili ambapo Kuna nyumba za wahitaji wa umeme hakuna nguzo za usambazaji na tunaambiwa REA wameshamaliza kazi katika eneo Hilo hivyo tuwafuate Tanesco na nyinyi bei ya kuweka nguzo ni kubwa kuliko uwezo wa wananchi, je, mnawasaidiaje wananchi hao?
Hakuna mgao mpendwa mteja wetu bali ni hitilafu zinazotokea na hatua stahiki huchukuliwa
 
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
1,680
Points
2,000
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
1,680 2,000
Habarini za kazi, katika kijiji cha Munjebwe, Rulenge Ngara, nguzo za umeme HT zimepita upande wa pili wa barabara approx. 150 m, na upande wa pili ambapo Kuna nyumba za wahitaji wa umeme hakuna nguzo za usambazaji na tunaambiwa REA wameshamaliza kazi katika eneo Hilo hivyo tuwafuate Tanesco na nyinyi bei ya kuweka nguzo ni kubwa kuliko uwezo wa wananchi, je, mnawasaidiaje wananchi hao?
Kuna awamu mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya REA hivyo wateja wanaokusa kwenye awamu moja tunawaomba wasubiri awamu ya pili
 
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
1,680
Points
2,000
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
1,680 2,000
Habarini za kazi, katika kijiji cha Munjebwe, Rulenge Ngara, nguzo za umeme HT zimepita upande wa pili wa barabara approx. 150 m, na upande wa pili ambapo Kuna nyumba za wahitaji wa umeme hakuna nguzo za usambazaji na tunaambiwa REA wameshamaliza kazi katika eneo Hilo hivyo tuwafuate Tanesco na nyinyi bei ya kuweka nguzo ni kubwa kuliko uwezo wa wananchi, je, mnawasaidiaje wananchi hao?
Kuna awamu mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya REA hivyo wateja wanaokusa kwenye awamu moja tunawaomba wasubiri awamu ya pili
 
M

miss lulu

Member
Joined
Dec 25, 2014
Messages
56
Points
125
M

miss lulu

Member
Joined Dec 25, 2014
56 125
Mimi ni mteja mwenye mita namba 54151170302 kimara mwisho. Mtaani kwetu nyumba kama sita hatuna umeme ikiwemo ya kwangu . Jana ijumaa ulikatika siku nzima ukarud usiku saa tatu na leo jumamosi ni umekatika asubuhi mpaka mida hii haujarudi. Je kuna tatizo gani ktk hizi nyumba chache kupelekea kukosa umeme ???
 
Zeus1

Zeus1

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Messages
3,171
Points
2,000
Zeus1

Zeus1

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2017
3,171 2,000
Msaada ,Mimi ni mteja mwenye namba 24211502166 naingiza umeme siku nzima mashine ina load na kujibu Error 00 msaada
 
Zeus1

Zeus1

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Messages
3,171
Points
2,000
Zeus1

Zeus1

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2017
3,171 2,000
Msaada ,Mimi ni mteja mwenye namba 24211502166 naingiza umeme siku nzima mashine ina load na kujibu Error 00 msaadatlk
 
D

DAD'S SON

Senior Member
Joined
Nov 18, 2015
Messages
141
Points
250
D

DAD'S SON

Senior Member
Joined Nov 18, 2015
141 250
TANESCO mjitathimini uendeshaji wenu wa shirika kwani ni miaka na miaka sasa imepita tatizo la kukatika umeme imekuwa kero utadhani ndo SERA YA TAIFA.

Ifike wakati tuache mazoea,umeme ndo kila kitu katika ukuaji wa uchumi wa nchi nyingi dunia kwan big investment zinategemea sana umeme lakini pia hata watu wa kawaida wanategemea umeme kuingiza kipato na kipato kinavyoingia kwa mtu mmoja mmoja ndio uchumi unakuwa lakini pia stability ya umeme inavutia wawekezaji.
Naomba niwakumbushe Rais wetu alisema hii ni Tz ya viwanda je na nyinyi mnalijua hili?? Ukizungumzia kiwanda unazungumzia na umeme.

Kwa kuhitimisha tuache mazoea kazini,tuwe wabunifu and tutumie elimu zetu kwa ndugu zetu wa Tz kwa mustakabali wa taifa hili linaloendelea.
 
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2018
Messages
554
Points
1,000
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2018
554 1,000
Tanesco Kibaha pwani.
Kongowe barabara ya Soga hakuna umeme siku ya nne leo. Je mna habari?
 
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
1,680
Points
2,000
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
1,680 2,000
TANESCO mjitathimini uendeshaji wenu wa shirika kwani ni miaka na miaka sasa imepita tatizo la kukatika umeme imekuwa kero utadhani ndo SERA YA TAIFA.

Ifike wakati tuache mazoea,umeme ndo kila kitu katika ukuaji wa uchumi wa nchi nyingi dunia kwan big investment zinategemea sana umeme lakini pia hata watu wa kawaida wanategemea umeme kuingiza kipato na kipato kinavyoingia kwa mtu mmoja mmoja ndio uchumi unakuwa lakini pia stability ya umeme inavutia wawekezaji.
Naomba niwakumbushe Rais wetu alisema hii ni Tz ya viwanda je na nyinyi mnalijua hili?? Ukizungumzia kiwanda unazungumzia na umeme.

Kwa kuhitimisha tuache mazoea kazini,tuwe wabunifu and tutumie elimu zetu kwa ndugu zetu wa Tz kwa mustakabali wa taifa hili linaloendelea.
*SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUKATIKA KWA UMEME*

*1. Utangulizi*
Kwa muda mrefu kumekuwa na uelewa kutoka kwa wateja wetu kuwa kila umeme unapokatika TANESCO WAMEKATA. Tumeona ni vyema tukatoa
Maelezo kwa ufupi ili wateja wetu waelewe sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi, zilizo ndani ya uwezo wa TANESCO na zisizo ndani ya uwezo wa TANESCO.

*2. Sababu za TANESCO Kukata Umeme*

TANESCO itakata tu umeme endapo kuna sababu zifuatazo *BILA* kuwataarifu wateja:-
a) Kuna mali inaungua (Mf. nyumba, kiwanda au mtambo)
b) Kuna mtu kanaswa na umeme.
c) Dharura _emergencies_ (imeelezwa hapo chini namba 4)

*3. TANESCO itakata umeme baada ya kuwataarifu wateja - _Planned Interruptions_ endapo:-*

a) Kuna matengenezo Kinga yaliyopangwa kufanyika ili kuimarisha miundombinu _Planned Preventive Maintanance_ (Mf. Kubadili nguzo zilizooza, kubadili waya chakavu, kubadili transfoma ili kuongeza uwezo wa umeme nk)
b) Matengenezo ya kila mara _Routine Maintanance_ (Mf. Kukata miti inayogusa line za umeme, kukagua vikombe na vifaa vingine kwenye line)
c) Kumuunga mteja mkubwa kwenye line ya msongo mkubwa wa umeme 11kV au 33kV

*4. SABABU zinazoweza kusababisha umeme kukatika kwa dharura _Emergency cases_* nyingi ni Unplanned Interruptions

a) Za kiasilia _Natural Calamities_ (Mf. Radi kupiga transfoma, mvua au upepo mkali kuangusha nguzo, kukata waya, miti au minazi au matawi ya miti kuangukia line, mafuriko, wanyama kama komba, nyani, nyoka, kunguru kunasa kwenye mifumo ya umeme nk.

b) Hujuma za kibinadamu _Sarbotage_
(Mf. Transfoma kuibiwa mafuta, kuibwa nyaya za umeme, nguzo kuchomwa moto na kuanguka, nguzo kubwa kuibiwa vyuma na kuanguka, magari kugonga nguzo za umeme na kuanguka, malori marefu kwenda juu kukata waya za umeme, wateja kukata miti ikaangukia kwenye line nk.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za msingi zinazoweza kusababisha umeme Kukatika. Hivyo ieleweke kuwa sio kila KUKATIKA KWA UMEME -TANESCO wamekata ni suala pana linalohitaji kujua sababu. Wakati mwingine kwa maelezo hayo hapo juu, Umeme unakatika hata TANESCO inabidi kufuatilia mifumo ili kujua sababu za kukatika.

*5. Hitimisho*
Tunajua jukumu la TANESCO ni kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika, pia ni ukweli kuwa mifumo mingi ya TANESCO ni ya muda mrefu hivyo inahitaji ukaratabati wa mara kwa mara na uwekezaji mkubwa ambao sote tumeona jitihada zinazofanywa na Serikali ili TANZANIA iwe na umeme wa uhakika.

Tunaomba umma uelewe sababu hizi na kuwa kama viongozi tunaamini hakuna mfanyakazi wa TANESCO anaweza kulihujumu Shirika kwa kukata umeme bila sababu au kukata umeme bila kufuata maagizo na utaratibu wa kukata line uliowekwa. Sio kila mfanyakazi au fundi anaweza kukata umeme. Upo utaratibu tena wakati mwingine wa kimaandishi unaompa fundi ruhusa, kabla ya kukata umeme. Kama yupo na anafahamika ( _Kama baadhi ya wateja wetu wanavyotuhumu_) tunaomba ushirikiano wenu ili tuweze kumshughulikia kwa taratibu za kisheria na tutakuwa tumelisaidia Shirika na serikali kwa ujumla.

TANESCO
_*Tunayaangaza Maisha Yako*_
 
sinajinasasa

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
1,740
Points
2,000
sinajinasasa

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
1,740 2,000
@ TANESCO utaratibu wa kuifungua meter mpya ukoje?
Maana nimefanyiwa installation na meter mpya, imewekewa Unit 10, nataka niongeze kwa kununua unit kwenye simu, inanikatalia.
20190512_190036-jpeg.1095714
 
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
1,927
Points
1,500
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
1,927 1,500
Hivi Tanesco mnafanyaje kazi Maofisini humu ndani ya utawala huu wa awamu ya tano?

Je mnatofautiana job description zenu Kati ya mkoa na mkoa? Nimefuatilia sana Suala la kupunguziwa matumizi kutoka makubwa kuja madogo, licha ya mizunguko mingi bado nilivumilia. Lakini mwisho mlichokitaka nikatimiza.

Suala la kubadilishwa kuja matumizi madogo inachukua Mwezi mzima? Sijapata kuona kutoka kwenu. Ofisi ya tanesco Kigamboni tangu inijazishe fomu ya kupunguza matumizi na kuahidiwa Kuwa Watakuja kukagua Vyombo vya umeme nilivyo navyo Leo ni Mwezi mzima umetimia, na wala hawajaonekana. Je huu utaratibu wa Mwezi mzima unatumika Dar tu? Inakuwaje mnatofautiana na mikoa mingine?
 
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined
Jul 12, 2014
Messages
1,680
Points
2,000
TANESCO

TANESCO

Verified Member
Joined Jul 12, 2014
1,680 2,000
Hivi Tanesco mnafanyaje kazi Maofisini humu ndani ya utawala huu wa awamu ya tano?

Je mnatofautiana job description zenu Kati ya mkoa na mkoa? Nimefuatilia sana Suala la kupunguziwa matumizi kutoka makubwa kuja madogo, licha ya mizunguko mingi bado nilivumilia. Lakini mwisho mlichokitaka nikatimiza.

Suala la kubadilishwa kuja matumizi madogo inachukua Mwezi mzima? Sijapata kuona kutoka kwenu. Ofisi ya tanesco Kigamboni tangu inijazishe fomu ya kupunguza matumizi na kuahidiwa Kuwa Watakuja kukagua Vyombo vya umeme nilivyo navyo Leo ni Mwezi mzima umetimia, na wala hawajaonekana. Je huu utaratibu wa Mwezi mzima unatumika Dar tu? Inakuwaje mnatofautiana na mikoa mingine?
Ndugu mpendwa mteja wetu sio kila anayeomba kubadilishiwa matumizi anabadilishiwa hapo hapo.kwanxa lazima akidhi vigezo pili tunaenda kumkagua nyumbani kwake.
 
Perimeter

Perimeter

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Messages
1,124
Points
2,000
Perimeter

Perimeter

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2015
1,124 2,000
ingekua mjibu comment ndio muingia front ningeelewa kitu ila hapa ni kutiana moyo kwa ushauri ila Ofisini tukija tunakuta watu wengine,shida bin shida
 

Forum statistics

Threads 1,294,032
Members 497,789
Posts 31,162,867
Top