Ikitoka remote ya mita imeharibika kupata nyingine utaratibu wake uko vipi?
 
Habari TANESCO...naomba kujua gharama za kuweka mita za umeme zile za kusoma units...

Kuna nyumba ina share mita moja sasa imeonekana bora kila mtu awe na mita yake kuepusha lawama na kadhia hasa kwenye nyumba za kupanga hizi..kwaio naombeni kujua gharama.
 
Tanesco ndugu zangu sisi wakazi wa kigamboni vijibweni soweto tunawaomba tangu juzi jumatatu usiku paka leo hatuna umeme..tunaomba mtusaidie
 
Tanesco huduma kwa wateja tukipiga hizo number zenu mnatukata pesa wakati hata hatujaongea nanyi... Mnasema mnahudumia wengine.. kwanini mnatukata pesa bila ya kuongea na mtoa huduma!?
 
Mkoa wa pwani wilaya ya rufiji, eneo lote la ikwiriri,umeme hakuna tokea saa tano asubuhi na hakuna taarifa nini kinaendelea, panapokuwa na hitilafu toeni taarifa wateja wenu tujue
 
Mkoa wa pwani wilaya ya rufiji, eneo lote la ikwiriri,umeme hakuna tokea saa tano asubuhi na hakuna taarifa nini kinaendelea, panapokuwa na hitilafu toeni taarifa wateja wenu
 
Mimi
Karibu mgeni,
Ila mngeanzisha uzi maalum kwa matatizo mbali mbali
Mimi ni mteja mwenye Mita Namba 37154683611; niko mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Magu, Kata ya Isandula, Mtaa wa Ibidanja. Mita niliyoitaja ni mpya, baada ya ile ya zamani kuondolewa katika zoezi la kubadilisha mita.
Mita hiyo mpya ni ya kujazia token palepale kwenye mita; na tangu imewekwa haijasumbua chochote.
Pamoja na kutokusumbua kwake, aina ya MITA HIZI SIYO SALAMA kwa sababu kidirisha cha circuit breaker yake kinaweza kufunguliwa na umeme kuzimwa na yeyote hata asiyehusika. Hii ni hatari, HASA WAKATI WA USIKU; maana mtu mwenye nia ovu kama mwizi, jambazi n.k; anaweza kuzima umeme wa nyumba husika na akafanya uovu wake gizani, maana wenye nyumba wanakuwa hawana uwezo wa kuwasha taa.
Mita za aina hiyo mngefunga kwenye nyumba zenye usalama wa kutosha; nyumba zenye fence, gate na walinzi. Kwenye nyumba zisizokuwa na viwango hivyo, fungeni mita za kutundika kwenye nguzo/ bracket zibazotumia remote kujaza token. Mita hizi ni salama zaidi kwa Wateja na kwa shirika lenyewe (maana ni vigumu MTU ku-temper na mita iliyoko juu ya nguzo au kwenye bracket. Nawasilisha.
 
Ni wape hongera kwa kazi kwa wale wanaotimiza.majukumu Yao.Ningependa kujua kwanini maeneo ya Mbagala Kiburugwa tuna mgao kila siku ya Ijumaa mara tu ifikapo saa 2:30 usiku? Kwani hivi ni miezi miwili na nusu imepita mara tu ukifika muda nilioutaja Umeme unakatika kwa muda wa saa tatu.
 
Hakuna mgao mpendwa mteja wetu bali ni hitilafu zinazotokea na hatua stahiki huchukuliwa
 
Tumepokea ushauri wako mpendwa mteja
 
Sasa kwanini umeme ukatike kila siku ya Ijumaa muda huo wa saa 2:30 usiku? Kwa hiyo hitilafu unakuwa tu ifikapo Ijumaa saa 2;30 usiku? Kukatika kwa umeme eneo la Mbagala kiburugwa kwamba ni hitilafu sikubaliani na Maelezo haya. Hizi hitilafu zinasubiri ifike Ijumaa? Tunasubiri tena wiki hii tarehe 10/05/2019 saa 2:30 usiku umeme ukatike maana tayari hiyo tumeiweka kwenye ratiba ya kila ifikapo Ijumaa saa 2:30 usiku.
 
Mimi ni mkazi wa Jiji la mbeya kata ya Iganjo mtaa Ikhanga.mtaa huu hauna umeme mpaka leo naandindika ujumbe huu kwenu,tumeanza kufatilia umeme tangu 2010 tukaambiwa tusuke umeme tutaletewa lakini hatukupata,2017 mwezi wa pili ulikuja umeme wa REA ambapo zilifungiwa nyumba 20 tuu tatizo likaendelea.Nasisi wakazi wa apa tumetoa eneo la kujenga substation ya umeme lakini bado tupo gizani mpaka leo tukifuatilia tunaambiwa hatumo kwenye budget ya kuwekewa umeme kwa miaka yote hiyo.Naomba majibu yenu shirika mnampango gani na sisi wakazi wa Ikhanga
 
Tangu Pasaka eneo letu lina tatizo la umeme,umeme mdogo sana,kila siku tunawapigia Tanesco kibaha emergency wanadai kurekebisha ni zaidi ya week,fridge haziwaki.Jaribuni kuwa serious na matatizo ya wateja wenu.Tunaingia hasara ya kumwaga vyakula kwa ajili ya uzembe wenu.Au Ili nalo mnasubiri Rais afanye?
 
Kwanini wilaya ya tarime mvua ikianza tu, iwe manyunyu au kubwa umeme unakatwa?. Siku nyingine hadi masaa 24. Inamaana miundombinu yenu imejegwa kwa matope au?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…