Nimelipia kuunganishiwa umeme tangia tarehe 04/06/2018 nguzo zimesimikwa trh 26/10/2018 kwa sasa ni mwezi zimesimikwa nguzo lkn sijaunganishiwa umeme mpaka sasa sijui tatizo nn na niliambiwa siku 90 za kazi nitaunganishiwa umeme msahada wenu tafadhari nipo Geita mjini.
 
Umelipa kwa jina gani?tarehe na eneo gani tafadhali
DHAMBI YA KIBURI

"KIBURI" ni kati ya dhambi ngumu sana kujigundua kama unayo au la.

Na kwa sababu ya ugumu wa kujigundua, ndio maana imemaliza watu wengi na hata watumishi wazuri wa Mungu...

"Naweka hapa mambo kadhaa TUJIPIME SOTE KAMA TUNA DALILI ZA KIBURI AU LA"

1. Ukiona, KILA UKIONYWA UNAKASIRIKA NA KUNUNA AU KUSUSA, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.

- Yaani unaona karipio au onyo badala ya kuona tatizo lako, au hata ukiona tatizo lako huwezi kujizuia KUKASIRIKA AU KUNUNA UKIONYWA.

2. Ukiona, KILA MKIKOSANA NA MTU, HUONI KOSA LAKO, UNAONA MAKOSA YA MWINGINE TU, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.

- Kiburi siku zote NI KIDOLE KUKUONYESHA KOSA LA MWINGINE.

- Nilichojifunza, kwenye kila kwenye wawili au zaidi kukosana na kutokuelewana, kila mmoja ana mahali pa kujirekebisha, hakuna asiye na jambo la kujirekebisha

3. Ukiona, KILA UNALOFANYA, UNATAKA KUJILINGANISHA NA WENGINE, AU KILA WANACHOFANYA UNAJILINGANISHA NAO, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.

- Kiburi siku zote KINATAKA WEWE UJIONE UKO JUU YA WENGINE....
Wewe mzuri zaidi ya wengine... Msomi zidi ya... Una pesa zaidi ya... Unafundisha zaidi ya... Unahubiri zaidi ya... Unaomba zaidi ya...

Siku zote "Wahesabu wengine kuwa bora..."

4. UKIONA, KILA UNALOFANYA UNAFANYA KWA LENGO LA KUSHINDANA.

- Unafanya jambo zuri ndio, lakini Adhma (Motive) yako ni mashindano, hata kama hujasema hivyo...

- Unafanya ili kumshinda fulani hata kama fulani hajui, yaani utoshelefu wako wa ndani sio kutimiza jambo fulani, bali ni kugundua KWA KUTIMIZA HILO UMEMSHINDA FULANI

5. Ukiona, UNAPENDA KUSIFIWA KWA KILA UNALOFANYA, kwa lugha nyingine kuwa RECOGNIZED AND APPRECIATED.

- Kutambulika na kushukuriwa (to be recognized and appreciated) si jambo baya kabisa, lakini ukiona ukikosa hicho kitu unakosa amani kabisa na unatumia gharama yoyote utambulike na kushukuriwa, HICHO NI KIBURI KINAKUSUKUMA.

6. Ukiona, KILA ZURI UNALOLIFANYA SIRINI, UNATAKA LIJULIKANE NA WATU HATA KAMA SI MUHIMU KWAO na si kwa lengo la KUJIFUNZA, hiyo ni dalili ya KIBURI.

- Ukiomba, hauridhiki mpaka watu wajue uliomba, UKIFUNGA, mpaka watu wajue ulifunga au huwa unafunga, UKIFANYA JAMBO ZURI KWA MUNGU WAKO, mpaka watu wajue ndio unasikia kuridhika... Kinachokusukuma ndani ni KIBURI.

7. Ukiona, HAUKO HURU (COMFORTABLE) KABISA KUTUMIA LUGHA YA PAMOJA (tuta.., tume..) UNAPENDA ZAIDI KUTUMIA LUGHA YA BINAFSI (Nita.., nime.. ) UNAPOONGELEA MAMBO AU UMILIKI WA VITU, hiyo yaweza kuwa dalili ya KIBURI.

- Hupendi kutumia lugha kama, vitu vyetu, jambo letu, huduma yetu... Sisi... nk unapoongelea jambo ambalo na wengine wana mchango hata kama ni mdogo sana, hasa kama mwewe ni muanzilishi wa jambo au una mchango mkubwa juu ya jambo.

Kumbuka "KIBURI HUTANGULIA ANGUKO"

Lakini pia, "KIBURI HUTANGULIA MAUTI"

EE MUNGU UTUPONYE NA DHAMBI YA KIBURI.

NATUMAI UMEJIFUNZA KITU., UBARIKIWE NA BWANA.
 
Samahani, sio kusudio.
 
Uongozi wa taneaco jengeni utamaduni wa kukagua mindombinu yenu kila wiki.
Pia chunguzeni ongezeko la watu na kisha muimarishe huduma zenu kma vile kuongeza transfoma nk.
Kuna baadhi ya maeneo yameeongezeka watumiaji wa umeme kama vile liluvya-hondogo, kwa komba nk hivyo kupelekea kuzidiwa kwa transfoma na hivyo umeme kukosa nguvu, hili sio jambo la kusubiria mwambiwe rekebisheni, ongezeni transfoma mawneo hayo niliyo yataja ali watu wandeshe shughuli zao bila kikwazo. Maeneo hayo umeme hauna nguvu na haujatulia labisaaaa
 
Nyumba yangu iko mbali na laini ya umeme, nimeambiwa panaitajika nguzo mbili(2).je? Zile nguzo lazima nilipie na nguzo moja bei gani?
Niambieni gharama zote sh,ngapi?
#NAITAJIUKWELINIJUE
 
UMEME UMEKATIKA MUDA MREFU ENEO LA ILALA AMANA NA BUNGONI. KUNA NINI TUELEZENI NA TAUREJESHA SAA NGAPI KWANI KAZI ZINALALA.
 
TANESCO nahitaj mita Namba ya jirani yangu ili nijaze kwenye fomu!

maswali-je ni lazima nichukue mita Namba ya nyumba iliyo chini ya nyumba yangu?au cha msingi ni mita Namba ya Jiran yoyote?

je nisipoipata hiyo meter Namba kwa huyo Jiran ndo basi sitaruhusiwa kufungiwa umeme?
 
Ukishafungiwa mita mpya inachukua muda gani mpaka kuingizwa kwenye ile tarrif D1 kama matumizi yako hayazidi unit 75 kwa mwezi??
Maana kuna wengine wamefungiwa tangu Septemba mpaka leo bado wapo tarrif 1 tu
 
Ukibadilishiwa mita na kupewa mpya huku kwenye mita ya zamani kuna Units unatakiwa kufanya nini ili Units kwenye mita ya zamani ziingizwe kwenye mita mpya?
 
Ukibadilishiwa mita na kupewa mpya huku kwenye mita ya zamani kuna Units unatakiwa kufanya nini ili Units kwenye mita ya zamani ziingizwe kwenye mita mpya?
Huwa wanazirudisha, mie waliniuliza nikambia zilizopo, baada ya muda nikatumiwa tokens kuangalia ni zile zile
 
Hii tabia ya kukata kila siku inakera sana mnakata halafu ukirudi hauna nguvu mnatwaribia vitu
 
Tanesco msaada tafadhali,naishi boko dsm,umeme umekuwa unakata mara kwa mara nyumbani kwangu ila nyumba nyingine unakuwa upo,nimeita fundi wangu akacheki akadai circuit breaker ndio ina shida,kabadilisha lakini tatizo bado liko,nimecheki kwenye mita ya luku ukikatika kuna maneno 'Loc out'....naomba pia namba ya emergency upande huu
 
Gharama kwa miradi ya REA ni 27000 tu mingine ni 177000 vijijini na 321000 mijini kwa walioko ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo ya TANESCO
Mhhh..juzi tu hapo nilimtembelea dada pale nziba alikuwa analalamika kaungiwa umeme Wa REA vijijini kwa laki sita, hii imekaaje hii!?
 
Kwanza napenda kuanza kwa kutoapongezi kwenu coz mmeboresha kwa asilimia kubwa Sana huduma zenu ktk jamii but na omba mchanganuo ktk 3% ya makato ya REA nikiasi gani kimekusanywa kwa Mwaka 2016/17 na matumizi yake kiujumla ahsante.
 
Mhhh..juzi tu hapo nilimtembelea dada pale nziba alikuwa analalamika kaungiwa umeme Wa REA vijijini kwa laki sita, hii imekaaje hii!?
umeme wa REA hakuna gharama ya Laki sita ndugu mteja,

je alivyotoa hio hela amepewa risiti yenye kiasi hicho?
 
Kwanza napenda kuanza kwa kutoapongezi kwenu coz mmeboresha kwa asilimia kubwa Sana huduma zenu ktk jamii but na omba mchanganuo ktk 3% ya makato ya REA nikiasi gani kimekusanywa kwa Mwaka 2016/17 na matumizi yake kiujumla ahsante.


asante sana kwa swali zuri sana, lakni tunapenda kukujulisha kuwa kiasi hicho hupelekwa moja kwa moja REA kwa ajili ya maendeleo umeme vijijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…