Tamko la serikali kuhusu ufafanuzi wa tozo kwenye miamala ya benki na simu, Septemba 1, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,977
Wizara ya Fedha imetoa ufafanuzi kuhusu tozo ya miamala ya simu na benki Septemba Mosi, 2022 ikiwa ni siku kadhaa tangu kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu gharama za huduma hizo za kifedha.



1b12004d-e186-40e0-a587-ffee1f90ccac.jpg

Waziri wa Fedha na Mipango - Mwigulu Nchemba
Chimbuko la tozo ilikuwa ni kwaajili ya kuunganisha nguvu kama watanzania ili tuweze kutekeleza baadhi ya mahitaji ya lazima kama madarasa, nyumba za walimu, ujenzi wa vituo vya afya, ununuzi wa vifaa tiba na ujenzi wa miundo mbinu ambayo yamekuwa yakekosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti.

Ufinyu wa bajeti umetokana na kuongezeka na majukumu ya msingi inayofanywa na serikari. Majukumu hayo ni kama miradi mikubwa kama bwawa la Mwalimu Nyerere, reli ya kisasa na maeneo mengine ni barabara, afya, elimu bure, mikopo elimu ya juu na umeme vijijini.

Kiwango cha tozo kilipunguzwa kutoka Tsh. 10,000/- mpaka Tsh. 7,000/- baada ya kupata maoni kutoka kwa watanzania kwamba tozo zimekubalika lakini zimeanzia kwa gharama ya juu sana. Lakini hii pia ikapunguzwa tena (na kwenye maeneo mengine) kutoka Tsh. 7,000/- mpaka Tsh, 4,000/- ili kuongeza wigo wa ushiriki ambapo ndiyo ilikuwa chimbuko la kwenda kwenye tozo za benki.

Nchi hii ni yetu na kila mtu yuko huru kutoa maoni akiona mambo hayaendi vizuri. Serikali imepokea maoni na itafanyia kazi swala la kutozwa mara mbili kwa fedha zinazo kuwa benki na swala la mpangaji kukusanya kodi ya jengo na kuipeleka kwenye mamlaka ya mapato badala ya mmiliki wa jengo.

Ni lazima mtu ambaye ana mapato alipe kodi iliyo sahihi aliye na kidogo alipe kidogo na aliye na kikubwa alipe kidogo, masikini kubeba mzigo mkubwa ni kutengeneza pengo kubwa kati ya waliyonacho na wasiyonacho.

Serikali inaendele kufanya uhakiki ili iweze kuongeza wigo wa tozo na kodi ambazo zitasaidia kupunguza mzigo kwa mtu mmoja mmoja.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Innocent Bashungwa
Tozo zimesaidia kuboresha sekta ya afya, elimu na barabara kwa kujenga vituo vya afya, madarasa na barabara vijijini na mijini, lakini pia kuongeza vifaa na watumishi.

Maswali na Majibu
Swali mwandishi DW
: Miaka ya nyuma watanzania waliaminishwa kuwa Tanzania ni tajiri na inaweza kujiendesha yeneywe bila kutegemea tozo kutoka kwa wananchi je, utajiri huu wa Tanzania uliofanya Tanzania kujiendesha yenyewe umepotelea wapi?

Jibu Mwigulu Nchemba: Utajiri wa rasilimali usipozivuna utaendelea kuwa masikini, unakuwa na utajiri ila wewe ni masikini. Bila kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji tutaendelea kuwa masikini.

Tozo kuongezeka ni sababu mambo yanabadilika na mahitaji yanaongezeka, ambapo na bajeti pia lazima iongekezeke. Tozo ni moja ya chanzo kinachofanikisha kufikiwa kwa mahitaji hayo ya kibajeti.

Swali mwandishi Azam Tv: Mpango wa serikali kubana matumizi umefikia wapi? Gharama za maisha kupanda licha ya serikali kutoa ruzuku kwa maadhi ya maeneo tatizo ni nini?

Jibu Mwigulu Nchemba: Jitihata zinafanyika hapa ndani kuhakikisha inapunguza ukali wa maisha lakini chanzo kama Uviko-19 na vita bado vipo hivyo gharama zitaendelea kupanda mbali na jitihada zinazofanyika.

Hatua mbalimbali za kubana matumizi zimechukuliwa na ufafanuzi utatolewa kadri nafasi itakavyopatikana.
 
Shida ya tozo sio ufafanuzi kwani hakuna asiyeelewa uwepo wake; tatizo ni maumivu yanayosababishwa na tozo, dawa yake zipunguzwe au kuondolewa kabisa, na kama zikipunguzwa, sharti tuambiwe mapato na matumizi yake ya kila mwezi.
 
Back
Top Bottom