Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
msingeweka ushahidi mzito kama huu kwenye mtandao....nani ajuaye atakayehonga Vodacom wasitoe ushirikiano?

wakihongwa basi huyo afisa wa voda aliyehongwa,aliyemhonga,namna alivyohongwa,tarehe,saa na details zote za tukio vitawekwa hadharani.hata wakifuta details na kubadilisha data kuwaokoa hawa mafisadi tukio hilo litatajwa hadi tarehe na data zilizobadilishwa,aliyebadilisha na alivyobadilisha na aliyemtuma,tangu anaamka asubuhi alikunywa chai na nini,chezea nguvu ya umma wewe?watu wameamua kutetea nchi yao hawana maskhara hata kidogo!
 

Mohamedi Mtoi na Edwin Mtei hii namba mmeifanyia kazi?

Mkuu Mbara, kweli hii namba kwa M-pesa inatoa jina la Zitto Zuberi. Kama nimemwelewa vizuri Mabere Marando, Haya mambo yatafafanuliwa Mahakamani. Pengine ni vema mimi na wewe tukasubiri tu wenye hizi namba waitwe huko Mahakamani wakaeleze uhusiano wao umekaaje.
 
Mkuu Atongwele, mimi sinashaka kabisa kuhusu authenticity ya ile video, natatizwa na jambo moja tuu "The Motive Behind!" baasi!. Chadema badala ya kukanusha "the motive behind" hiyo video, wako bize na ukachero wa utengenezwaji na upatikanaji!, Ludo akikiri na kukubali ku confess, atageuzwa shahidi number moja wa Jamhuri na picha itageuka!, inaweza asiwe tena ni Rwaka peke yake!, mnaweza msiamini!, nawashauri subirieni!, tunazungumza hapa as if ni utani, kwa sasa kwa Chadema, the issue ni video tuu, na kwao, this is just the "going!" na kwa serikali, the issue ni ya Kibanda, na kwao its still "tough!". Subirieni picha na mchezo utakavyo geuka, "When the going gets tough, the tough gets going!" wapenzi, wanachama na washabiki wa Chadema, itakuja kunielewa nina maanisha nini with "the motive behind", kila nikiuliza hakuna anayejibu!.
Pasco.
 
Mbona sioni pahala ambapo zitto zuberi kabwe anatajwa? Au ni mtego utakaomnasa mbele ya safari automatically?
 
Mohamedi Mtoi, wa CDM naye anahusika na haya mambo ya utekaji nyara.

slaa amesema wanausalama wao hawa ndio wakutafutwa ndio wanajua kutoa kucha,meno na macho na wenzao ni kina rwakatale na ludo wakamatwe
 
Kwa ambao hamjui, huwezi kutumia information ambayo umeipata kwa kutumia njia zisizo halali mahakamani.

Hapa hata CHADEMA wawe na hizi taarifa kama hawajazipata kwa njia halali kwa kuomba kisheria toka mashirika ya simu, hizo information haziwezi kutumika mahakamani.

Kibaya zaidi wakijaribu kuzitoa na kuwataja waliowapatia TCRA itakuwa imepata sababu ya kuwachukulia hatua.

Hii habari nzima ni propaganda ya kisiasa na haina nguvu kabisa kisheria.
ndio hivyo mkuu, chadema wanazo details zote za mawasiliano, hapo wanachotaka ni ku cross check tu!
 
Nilikuwa mwanaCCM zamani ,kuanzia leo mimi ni CHADEMA .Tuangalie ukweli ndugu zangu.Hivi haya mambo ya kubambikiwa yalikuwepo na sasa ndio silaha ya mwisho ya CCM.Jamani CHADEMA NI MAKINI SANA.TUACHE USHABIKI.NAVAA GWANDA LEO HII

you will never walk alone!
 
Mbona sioni pahala ambapo zitto zuberi kabwe anatajwa? Au ni mtego utakaomnasa mbele ya safari automatically?

Huyo mheshimiwa alikuwa anapiga mayowe hapa jamvini eti kwenye chama kuna kirusi kilichovujisha "barua yake" kwa Katibu Mkuu kumbe kirusi halisi ni yeye mwenyewe. Kweli duniani kuna wanafiki.
 
Maneno ya Michuzi kwamba ni TISS imeibua hiyo video yanathibitisha ushiriki wa TISS kwenye mchezo huo mchafu, na kwamba Chadema kinajua kuwa Michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa taifa katika kazi hiyo chafu. Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka usalama na Ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na yule jamaa anayempelekea kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa JF.
Hapo kwenye RED sio Mchezo,jamaa wameshanunuliwa LONG TIME!NJAA MBAYA SANA,UKIZIENDEKEZA UTAUZA MPAKA MASABURI!
 
Pasco nawe namba yako ni ipi? Kati ya alizotaja mabere? Maana inaonekana kuna jambo zito walijua ila hutaki kulisema kwa sasa.
Wana JF jihadharini sana, maana inaonekana genge la magaidi lina mtandao mpana sana.

 

Mapovu yanakutoka ovyo hujielewi
 
Asante Mabere Marando

Taarifa ndio kama hivi, 'wanafiki' hawawezi kuipenda taarifa hii, watathubutu kuibetua ati imekiuka misingi ya uandishi na taratibu za kisheria. Lakini wale wanaopenda uwazi kama hivi wataipenda taarifa hii. Binafsi taarifa kama hii inanikumbusha toleo la mwisho la Mwanahalisi na Halali.

Mwigulu na mashabiki wake wajifunze kusoma alama za nyakati, salamu hizi ziwafikie huko walipo. Wakumbuke kuwa CHADEMA ni ISHARA tu ya ukombozi, na wala sio Dr Slaa, Mbowe ama yeyote awaye.

Tukutane mahakamani hiyo kesho
 
Upuuzi tu! CHADEMA acheni kuweweseka, ukweli wote utajulikana mahakamani.

Kama mna uhakika hamna hatia kwanini mnaweweseka hivyo? Tulieni.

Tumechoshwa na matamko yenu ya kipuuzi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

peleka manjanjaa yako huko kwa kina Riz
 
Hapa imesemwa hivi

"Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa taarifa zao simu
na meseji (sms) ni Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na. 255756xxxxx, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Lameck Nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 xxxxx, 0757 xxxxx, 0714 xxxxx na 0787 xxxxx na Ludovick Joseph Rwezahula, ambaye simu zake ni, 0715 xxxxx na 0753 xxxxx."

Kwenye namba inayotumiwa na Nzoka haijasemwa kuwa anamiliki, imesemwa anayetumia. Sasa kutumia na kumiliki ni vitu viwili tofauti.
 

Sidhani kama una akili na ujuvi wa sharia kushinda jopo zima la wanasheria waliokesha na kutafakari hadi kutoa taarifa hii kwa Umma.
 
9535 mwisho ni namba ya zitto anahusikaje hapa??
 
Pasco nawe namba yako ni ipi? Kati ya alizotaja mabere? Maana inaonekana kuna jambo zito walijua ila hutaki kulisema kwa sasa.
Wana JF jihadharini sana, maana inaonekana genge la magaidi lina mtandao mpana sana.
Mkuu Investa, zile number zote zilizotajwa ni za vijana tuu wa kazi, wao wakishamaliza ndio wanakuja kuripoti kwetu!, ofisi yangu iko pale nyuma ya St. Peter lile jengo jipya mithili ya meli, karibu unitembelee, pale ila usiniulizie kwa jina hili la jf, pale natumia jina la kazini, naitwa chifu!, ukifika tuu getini, ukisema wewe ni mgeni wa chifu, hutaulizwa chochote, utapitishwa ndani, ndipo nitaitwa na nitakutembeza tembeza sehemu mbalimbali!, hadi desk la jf, nitakuonyesha majina halisi ya vimbelembele wote hadi locations na ip address zao!. Karibu sana!.
Pasco.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…