Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
malando muongo kweli katuletea habari za mwaka arobaini na saba make kachukua taarifa ileile ya mwanahalisi ile ya uongo naye kaongeza uongo hapo wa kuchongea watu,tunajua malando hampendi zito but yai litawatobokea tu.
 
Sawa panaweza kuwepo maingiliano ya simu baina ya watu hao,lakini sote hatujui nini walizungumza na pengine ushaidi wa meseji (sms) ungekuwa ni mzuri zaidi.Anyway ni mawazo tu,kikubwa suala hili liko mahakamani na ni vema tukasubili uamuzi wake.
 
Mohamedi Mtoi, wa CDM naye anahusika na haya mambo ya utekaji nyara.

Mkuu.
Naamini umenifahamu kupitia hapa JF, basi usinichafue pia kupitia JF.

Naichukia CCM kama ninavyo mchukia shetani na mambo yake. Kwa matendo yao hawana tofauti na shetani anaye hitaji kukemewa.

Kwa taarifa yako, Kama kuna watu wameathiriwa na CCM mpaka kwenye mfumo wa ndani wa familia mimi ni mmoja wapo!

Ngoja niweke hakiba ya maneno.
 
nahofia future ya nchi, misingi ya ugawanyo na chuki ndo inajengwa sasa hivi huko mbele ni giza
 
Sijawahi kuona mfa maji akizama jumla tu bila kutapatapa

Umeonaa eeeeeh. Chadema ndo wanavyokufa. Tena wamejichanganya kwa kuweka namba ya mzee wa kigoma miongoni mwa namba zinazotakiwa kuchunguzwa, haponi mtu na hakitabaki kitu ndani ya chama hicho
 
Pasco nawe namba yako ni ipi? Kati ya alizotaja mabere? Maana inaonekana kuna jambo zito walijua ila hutaki kulisema kwa sasa. Wana JF jihadharini sana, maana inaonekana genge la magaidi lina mtandao mpana sana.
Kwamba Pasco ni gaidi? Sidhani...Pasco tutamchukia mamvi akipitishwa kugombea urais....short of that Pasco mwepesi kama toothpick
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi kuona mfa maji akizama jumla tu bila kutapatapa

We kilaza wa UK(erewe) hujui chochote kuhusu CDM na hujawahi hata kutia pua yako kwny inner circle ya CDM.

Endelea kungoja tenda, acha wanaume on ground wakuoneshe siasa ni zaidi ya kutumia M - Pesa na kusafirisha parcel!
 
wakihongwa basi huyo afisa wa voda aliyehongwa,aliyemhonga,namna alivyohongwa,tarehe,saa na details zote za tukio vitawekwa hadharani.hata wakifuta details na kubadilisha data kuwaokoa hawa mafisadi tukio hilo litatajwa hadi tarehe na data zilizobadilishwa,aliyebadilisha na alivyobadilisha na aliyemtuma,tangu anaamka asubuhi alikunywa chai na nini,chezea nguvu ya umma wewe?watu wameamua kutetea nchi yao hawana maskhara hata kidogo!
Unajua watu wengi sana wanajua wanaopinga dhurma inayofanywa nchini ni lazma uwe wanachama wa chadema uliye front line. Wanasahau kuwa wapo wanachama damu wa chadema ndani ya Ikulu, ndani ya ccm, ndani ya serikali na wizara zake na ndani ya vodacom, tigo etc ambao wala hawajitokezi wala kutambuliaka.

Watu wengi wanajua pia wenye uchungu na nchi hii wapo kwenye vyama vya siasa tu, wanasahau pia kuwa wapo wananchi wasiowanachama wa chama chochote na ambao ndugu zao wamekuwa wakiteswa na kudhurumiwa na serikali kila kona ya nchi hii.

Lakin la msing wanasahau kuwa siku zote watu wakishachoka na utawala dharimu, watashirikiana kwa kila njia kuutokomeza utawala huo. Katika hali hiyo, huwezi kushangaa kwann cdm inapata information toka kila kona ya nchi hii hata zile ambazo ni classified documents. Wananchi wamechoka, hawataki kukiona ccm kinaendelea kutuibia na kutudhalilisha na sera ya sisi masikini.

Aidha, ni iman yangu pia wakati wanachunguza hizo nani kumpigia/kamtumia nan sms, waliweza kupata pia ujumbe gani ulikuwa umebebwa katika hizo intensive communications. Sisi tupo pembeni tunasubiria kuona hii movie ya ukombozi.
 
Wadau, siamini kama tamko hili limetolewa na mwanasheria ambaye si tu amebobea katika fani yake bali pia ni mtu ambaye aliwahi kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa kutokana na ushahidi wa tamko lake hili. Cha kusikitisha zaidi, ameongea mambo ambayo anajua kuwa anayo fursa kupitia mahakama kueleza yote hayo ambako ninaamini ndiko kwenye msaada mkubwa kuliko kuongea na waandishi wa habari ambao wataishia kuandika tu. ninajua kwa sasa chadema wanatafuta huruma za wananchi kupitia matamko yao hayo kwa vile wamechungulia na kuona kuwa hawawezi kushinda kesi ya lwakatare.

Yale ya kisheria kama mazungumzo ya simu hajayaongea....hivyo alichofanya ni kutoa taarifa...
Kwa sababu hii kesi ni ya kisiasa na wanapambana ndani ya bunge,majukwaani na kwenye media...hivyo huwezi ukaacha kuwatoa uvulivuli wanachama na wapenzi pale inapohitajika...
Hajakosea na anajiamini kwa anachoongea...
 
Sijui kama kutakucha leo.....ushetani huu lazima mwisho wa Dunia ufike. It pains

uko sawa make watu wazima kama malando wanakaa na kutunga uongo mtu kama zito kapigania chadema maishayake yote halafu leo anaonekana msaliti kweli watu hawana shukuruni.
 
huu ni muendelezo wa komba huruma ya wananchi. Hayo mawasiliano hayana nguvu ya sheria labda makampuni ya simu yakubali kutoa hayo mawasiliani. Swali je watakubali? hapo ndio chadema inapoyumba.

Kesi imewabana poleni ndio ukubwa
 
Huyo mheshimiwa alikuwa anapiga mayowe hapa jamvini eti kwenye chama kuna kirusi kilichovujisha "barua yake" kwa Katibu Mkuu kumbe kirusi halisi ni yeye mwenyewe. Kweli duniani kuna wanafiki.

Nilishasema na nitaendelea kusema Zitto sio mtu wa kuaminika, ni kigeugeu na asiyekuwa na nidhamu! Hata mama yake alishasema 'Zitto ni mtoto mkorofi'.
 
Sasa ndugu zangu wa CDM, mmeshaanika mchele kwenye kuku wengi mnatarajia mkute hizo kumbukumbu za mawasiliano ya hao jamaa zikiwasubiri? Hamjui ya kwamba fedha ni mwanaharamu?

yaani hapo kinachotakiwani kupata ushahidi kwa mjibu wa mahakama lakini mpaka jamaa wakaibuke tayari wanaushahidi...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom