Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
Unakwenda mahakama ipi wakati kila siku Chadema wanasema hawana imani na mahakama zetu.
 
Mwigulu amewashika vibaya hawa magaidi ndio mana wanaweweseka,mtulie dawa iingie vizuri
 
Jamani CDM kweli ni Mkombozi wa Watz na hakika CCM inatapatapa. Sijui dogo wa kule Mjengoni huwa anaambiwa mipango hii haramu na kutoa kibali, au hana habari KABISAA -- kama jinsi hana habari ni wizi na michoto kutoka fedha za umma na madudu mengine ya serikali yake.

Hata NCCR na CUF katika enzi zao walipokuwa juu kwenye 'dizzying heights' hawakuwa na watu makini kama hawa wa CDM na ndiyo maana vyama hivyo vilisambaratishwa bila resistance yoyote.

Kuhusu kupata nyaraka za simu, ninachokiona hapa ni kwamba mawakili wa serikali watajaribu kupinga kwa maelezo kwamba maafisa ni wa TISS kwa hiyo haiwezekani kutoa siri.

Lakini mahakama, kama inatka haki itendeke, inaweza kuagiza ushahidi utolewe in camera. Hii 'in camera' imefanyika katika kesi ile ya uhaini na hata ile ya Babu Seya.

Hongera sana MAKAMANDA -- sisi sote wanaopenda mabadiliko tuko very proud of you!
 
Mchawi aliyeuwa analia na kugaragara msibani hapa. Lets watch and see
 
Mkuu wa usalama hajaingilia mawasiliano kabisa,that mean usalama now wanachukua maelekezo toka kwa<moko wa miujiza> kuna jambo moja wasilolijua ccm,sie ndio wenye nchi na wao tumewakabidhi nchi hii,na wala hatujaikabidhi chadema,sasa ya nini wakae usiku na mchana wakiumiza vichwa jinsi ya kuuia cdm?

Mpaka hapa inaonyesha ni jinsi gani wameshindwa kuongoza nchi na sisi tuliowapata madaraka tupo hatarini,madawa fake tupewe sisi,condom fake sisi,cement fake sisi,magorofa yatuangukie sisi,barabara zao za miezi 4 kama dozi ya mgonjwa wa h.i.v,kutekwa tutekwe sisi,kusingiziwa kesi tusingiziwe sisi? kuna maana gani ya kuendelea kututawala?

Mungu sio Mr nice ipo siku na nyie mtakuwa kama sisi na misoto yote mtaipitia iwe hapa dunia ama chini ya futi 6.
 
Ninanusa halufu ya damu. katika hali hii sijui?? tuombe mungu atusaidie risasi zisiende angani. ulinzi na usalama ukitoweka sijui itakuwaje.
 
Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka usalama na Ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na yule jamaa anayempelekea kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa JF.

Naomba kamanda Maxence Melo na Invisible nipate muongozo juu la haya maneno kwenye hili tamko la chama changu....
 
Nitoeni haya mashaka niliyo nayo;

Je, mahakama haiwezi kukataa ombi la Chadema kutaka kutoa kibali cha makampuni ya simu kutoa taarifa za Namba hzo za simu?

Ikiwa mahakama itaridhia ombi la Chadema, je haya makampuni ya simu hayawezi kurubuniwa na kuchakachua hizo taarifa za namba za simu za hao wahusika 10?

Please naomba nijuzwe kuhusu hayo maswali yangu!

Mkuu hilo la mahakamani sina cha kusema maana sheria na taratibu za kimahakama sizijui vizuri ila hili hili la makampuni ya simu nahisi hawa jamaa tayari wameshajipanga na wana evidence. Na kwa kuweka angalizo kuhusu sheria inayoyaongoza haya makampuni ina maana wakijaribu kufanya uchuro yanaweza ingia matatani (sheria ipo). Lakini pia naamini mitambo ya simu ukitaka kucheza nayo mtu akitaka fuatilia kama kuna changes zimefanyika lazima itajulikana.
 
Mwigulu amewashika vibaya hawa magaidi ndio mana wanaweweseka,mtulie dawa iingie vizuri

C'MON CCM -- come to the point na ukiweza pangua hoja hizo hapo -- hata 30% tu. Hamuwezi chochote siku hizi zaidi kuwatia Watz umasikini, labda na uzinzi! SEMENI, KITU GANI MNAWEZA?
 
Naona leo una angaika sana! Umeelewa kilicho andikwa!

Yaani anajisikia raha mtu makini kama wewe ukimjibu upumbavu wake, nakushauri usiwe unamjibu hata moja ndo kwa anzisha lingine ajione mjinga
 
Akili ndogo Zinachezea akili kubwa.

ILA KUNAJAJI ALIYETAYARI KUNG'OLEWA KUCHA.

Je Chadema hamuwezi kuomba shitaka hili la Ugaidi dhidi yenu lisikilize na Mahakama za kimataifa kama the The Hegi?

Je makampuni ya CM YAKITISHWA NA KUTOA UTETEZI FEKI MTAGUNDUAJE.

Kwanini msitumie wahisani kama uwingeleza na Marekani watume wapelelezi wao kushiriki kun'gamua zuri na baya la sivyo wasitishiwe misaada na Wazuiliwe kuingia nchini Mwao kwa Kubinya democrasia.
 
Mkuu hilo la mahakamani sina cha kusema maana sheria na taratibu za kimahakama sizijui vizuri ila hili hili la makampuni ya simu nahisi hawa jamaa tayari wameshajipanga na wana evidence. Na kwa kuweka angalizo kuhusu sheria inayoyaongoza haya makampuni ina maana wakijaribu kufanya uchuro yanaweza ingia matatani (sheria ipo). Lakini pia naamini mitambo ya simu ukitaka kucheza nayo mtu akitaka fuatilia kama kuna changes zimefanyika lazima itajulikana.

na kuongezea -- na kwa taarifa kwa wengine ni kwamba bila shaka CDM wanazo taarifa kamili za mawasiliano yote hayo ya simu. Wanawatega tu CCM na Vodacom! Mark my words!

Yes -- CCM wameshikwa pabaya -- chezea CDM wewe!
 
Nimejikaza kiume nisitokwe na machozi.inauma sana ila we will never surrender mpaka mageuzi yafanyike tanzania
 
Mkuu ingekua vizuri ikaihurumia taifa lako Tz maana njama zote hizi za kuangamiza chadema zina lengo la kuendelea juihujumu taifa kupitia wizi wa rasimali za taifa na kuendelea kuwafanya watanzania maskini wa kutupwa huku watu wachache wakiendelea kutajirijika&#1548; jambo ambalo mwisho wake huenda ikazua vita kali kati ya walionacho na waliochoka na tukufika huko siyo chadema itakua imekufa bali taifa la Tanzania ndiyo itakua imeangamia.
watanzania tuhurumie taifa letu kwa kuikataa hiki chama kinachozidi kututia umaskini badala ya kuihurumia chadema, chadema na ccm kama vyama vinaweza kufa akini tz kama taifa is there to stay.
Well said mkuu. Ningekuwa kwenye PC ningekugongea like.
 
Kuna kitu tunaweza kujifunza hapa. Katika hivi vinchi vyetu vya kipuuzi ambavyo watawala wanahubiri hivi lakini wanatenda vile; wanahubiri demokrasia lakini wanatenda ufashisti; kuanzisha chama cha siasa unahitaji pia kuwekeza sana kwenye system bila hivyo sahau.

Nadhani kwa kipindi kirefu ambacho hawakujishughulisha sana "kukimbilia" Ikulu hawa Chadema waliamua kwanza kuwekeza kwenye system na ndiyo inayo payback hivi leo.

Siasa katika haya mataifa masikini inahitaji akili ya hali ya juu badala ya kutegemea hisani ya watawala unless mnataka kuwa wasindikizaji tu bila vision au mission yoyote. Sio utani Chadema wana vichwa! Duh!

Sasa nimeanza kuona mantiki ya maneno haya kutoka kwenye kinywa cha Dr. Slaa
"tuko makini kuliko wao, tuko makini kuliko CCM, tuko makini kuliko UWT, tuko makini kuliko hata serikali yao".
 
Nilikuwa mwanaCCM zamani ,kuanzia leo mimi ni CHADEMA .Tuangalie ukweli ndugu zangu.Hivi haya mambo ya kubambikiwa yalikuwepo na sasa ndio silaha ya mwisho ya CCM.Jamani CHADEMA NI MAKINI SANA.TUACHE USHABIKI.NAVAA GWANDA LEO HII
 
Mkuu hilo la mahakamani sina cha kusema maana sheria na taratibu za kimahakama sizijui vizuri ila hili hili la makampuni ya simu nahisi hawa jamaa tayari wameshajipanga na wana evidence. Na kwa kuweka angalizo kuhusu sheria inayoyaongoza haya makampuni ina maana wakijaribu kufanya uchuro yanaweza ingia matatani (sheria ipo). Lakini pia naamini mitambo ya simu ukitaka kucheza nayo mtu akitaka fuatilia kama kuna changes zimefanyika lazima itajulikana.

Nashukuru wa ufafanuzi, hata hivyo kuna post inasema kuwa hizo za mahakama ni taratibu tu ila washakamata hizo taarifa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom