Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
Mkuu, rekebisha bandiko lamp ..... leo ni sunday 14 April 2013

Sasa ndugu zangu wa CDM, mmeshaanika mchele kwenye kuku wengi mnatarajia mkute hizo kumbukumbu za mawasiliano ya hao jamaa zikiwasubiri? Hamjui ya kwamba fedha ni mwanaharamu?
 
aisee,watu wanadhuru watu,just kwa maslahi ya matumbo yao?pole kibanda
 
Ndoa maana ya hii tamko maana hayo yalijulikana! Kwa hiyo ni bora watu wajue!

Sasa ndugu zangu wa CDM, mmeshaanika mchele kwenye kuku wengi mnatarajia mkute hizo kumbukumbu za mawasiliano ya hao jamaa zikiwasubiri? Hamjui ya kwamba fedha ni mwanaharamu?
 
Mungu wangu liokoe taifa hili lililoachwa na wazee wetu nyerere, kawawa, karume, bibi titi, sokoine, na wengine wengi tu.
Hili genge la mafisadi na matapeli wa siasa na mali za umma wanataka kutuletea matatizo kwenye taifa lililojengwa kwa misingi ya uwelewano na mshikamano na leo wanataka kuliangamiza kwa sababu ya maslai yao ya kipuuzi....hakika chadema mtasimamiwa na maombi ya kila raia mpenda amani kwenye nchi hii mpaka ikulu mtaingia.
 
Hata kama watachomoka mwaka huu kwa kuwa wameshika dola lakini baada ya utawala wa dhaifu hili lisukule lake lazima tutakuja kusema nalo tu huko mbeleni. Haliwezi kutufanya kama sisi Watanzania wote ni wajinga kama anavyowafanya Yanga.
 
Wakuu mko makini sana, yaani hadi mnakera kwa kweli kwa umakini. Mungu azidi kuwafunulia hizi hila chafu hatimaye tuinuke kama taifa. ''HAKI HUINUA TAIFA''

KUDOS MAKAMANDA, Kila mpenda haki yuko nyuma yenu.

Daaah.. CHADEMA ni moto wa kuotea mbaya. These guyz are so smart indeed.
 
Ha ha ha! Hilo genge linaloshutumiwa ni kubwa mno hivyo tutege masikio hatukawii kusikia "HERI MIMI SIJASEMA" na ukweli utakuwa umejulikana. Hii kesi ni very interesting na itazua mambo mengi sana; ni milestone muhimu sana katika siasa za nchi hii. Wanafunzi wa sheria wa vizazi vingi vijavyo, I can guess, watafanya reference nyingi sana kwenye kesi hii. Asante Mola kwa kuwa upande wa waja wako kwani naona nguvu zako zikienda kudhihirika na kutenda kazi sasa. Kila mmoja na aseme Amina.
 
Huyo kigogo wa JF ni nani?

Ajitokeze mwenyewe!
 
Ndg wana JF sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha kiongoz mwandamizi wa CHADEMA akipanga mauaji ya mhariri wa gazeti. Mambo yako dhahiri kwani video inaonesha pale ni nyumbani kwake. Pili sikumtuma mtu akarekodi mkanda huo. Niliwahi kusema nina mkanda haina maana kuwa nilituma mtu.

Mikanda niliyokuwa nayo nilipewa na kiongozi wa CHADEMA anayechukizwa na vitendo hivyo vya kinyama. Ndugu zangu wa CHADEMA, najua nawakera na hampendi kusikia haya nawashauri msihangaikie habari ya Mwigulu ameshiriki bali hangaikieni kwanini kiongozi mwandamizi anafanya hayo pia kwanini anafanya kizembe mpaka mkanda unanaswa na tatu mjiulize. Kwangu mimi sioni kama kupata mkanda huo kwa kupewa au kwa hela ni dhambi kubwa kuliko ya kupanga mauaji.

Niwambie tu mkanda niliopewa sikuweka hata nukta na nilikabidhi vyombo vya usalama.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anda-wa-video-unaomwonesha-ndg-lwakatare.html
 
Sasa nimeielewa kauli ya 'the president elect 2015' kwamba, "CHADEMA ipo makini na imara kuliko serikali"
 
Mtu akikaribia kufa lazima arushe rushe miguu. Chadema inarusha rusha miguu
 
Ndio maana hiiissue anayeitamka upande wa ccm ni nchemba pekee, unajua nashangaa issue ya ugaidi itamkwe hata na Nape, ina maana nao wamemshitukia, wanacheza salakasi huku wamevaa mataulo
 
Magaidi wanajihami hapa. Hakuna kipya katika danadana za marando humu.
 
Jamani mbona ukisoma haya maelezo unaona kama hali ni mbaya!! Kama ni hivi basi nina wasiwasi na hali ya usalaama kwa watanzania. Hebu tujiulize, kweli thamani ya binadamu imekuwa kama takataka oza? Je kwa mtu yeyote awe raia au kiongozi yeyote ambaye anaifumbia macho hii hali basi aelewi kwa nini anaishi na hasa hajui nini maaana ya kuishi!
Jamani inawezakana haya mambo yakatokea hapa kwetu? Basi inabidi tukubali kuwa mzee wetu mwl Nyerere ALIONA MABALI!
 
Nimesoma mpaka mwili wangu umekufa ganzi. Nahisi hili litakuwa gumu sababu hakuna namna yakukataa kuwa mkuu wa kaya hajahusika hapa. Najiandaa kwa maandamano yasiyoisha mpaka haki itendeke
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom