Serikali ipunguze usumbufu kwa wafanyabiashara wanapoenda kukata leseni za biashara

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
386
765
Mwaka huu wa Fedha kumekuwa na usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara wanapoenda kukata leseni za biashara. Mfanyabiashara anapofika kwa Afisa Biashara anaelekezwa kufanya taratibu zote akitakiwa kwenda kwenye Internet cafe ili kukamilisha taratibu zote za kupata leseni.

Aidha wanaombwa na Maafisa Biashara kuwalipa ili wawakamilishie taratibu zote ili apate leseni. Kwenye Internet cafe mfanyabiashara analipa mpaka 20,000 kupata leseni moja na kwa Maafisa biashara analipa mpaka 30,000 ili kupata control number na kupata leseni. Kuna changamoto nyingi zinajitokeza kwa mfano mtu ametoka kijijini kuja kukata leseni na kwa siku hiyo taratibu zote hazikukamilika hivyo itabidi aingie gharama ya kulala akisubiri control number ya kulipia leseni.

Ushauri:-

(1) Waziri wa Viwanda na Biashara kwanza wewe ni msomi wa ngazi ya PhD tunakuomba upunguze mlolongo huu na mfanyabiashara anapoenda kukata leseni yake asikae zaidi ya masaa matatu akisubiri leseni yake.

(2) Malipo yanayoambatana na leseni kama Zima Moto, Afya, Osha zijumuishwe kwa pamoja na mfanyabiashara alipe kuliko kufuatwa fuatwa na hao wahusika.

(3) Leseni za biashara zihamishwe kutoka Halmashauri ambapo kuna usumbufu mkubwa na milolongo mingi mpaka kuja kupata leseni. Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom