Rais Samia, ichunguze Benki Kuu(BoT) kama kweli wako serious katika kusimamia Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha kwa wanaokepesha bila leseni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,016
144,373
Hii taasisi kila wakati inatoa taarifa kwa umma kupitia tovuti yao ya www.bot.go.tz kuonya watu waache kufanya biashara ya kukopesha bila leseni yaani kinyume na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake.

Kinachinishangaza ni kuona matamko mengi ya kuonya watu wanaojihusisha na hii biashara kinyume na sheria lakini sijaona ni wapi BOT wametoa orodha ya watu binafsi au taasisi zinazoshitakiwa kwa kuvunja hii sheria mpaka sasa.

Mitaani uvunjifu wa hii sheria ni mkubwa ikiwemo watu kufanya hii biashara pasipokuwa na leseni huku baadhi ya taasisi zilizosajiliwa zikifanya hii biashara kwa kuvunja sheria kama vile kukaa na ATM kadi za watu, kutotoa mikataba kwa wakopaji, n.k.

Hivyo, namshauri Mhe. Raisi achunguze hii taasisi kama kweli wako serious katika kusimami sheria husika na si kutoa tu presss release kila baada ya muda halafu hakuna kinachofanyika.

Pia, inanishangaza kuona Bunge kama taasis,i na wabunge waliopitisha hii sheria, nao hawako seriuos kabisa huku baadhi ya wananchi wao hasa kina Mama, wakidhalilika mitaani.Ni majuzi tu ushuhuda umetolewa mbele ya Katibu Mwenezi wa CCM, Paul Makonda katika ziara yake mikuona huku Waziri husika akitia majibu mepesi kwa maswali magumu mbele ya wananchi na Mwenezi wa chama chake kuhusu wakopeshaji wasiofuata taratibu.

Leo kupitia website yao, nimeona tangazalo la kufuta leseni ya kampuni moja na kama kawaida pia nimeona taarifa kwa umma ya 03/01/2024 juu ya kuonya wale wanaofanya hii biashara bila leseni.

Tangazo husika utaliosoma kupitia hii link:


Ifike hatua BOT waanze kuchukua hatua serious kwa hawa watu kwani licha ya kuvunja sheria, baadhi yao bado wanajiona wana haki hata ya kupeleka watu Polisi huku wao wenyewe wakiwa ni wavunja sheria.

Press release za mara kwa mara bila vitendo ni kazi bure na ni dalili ya usanii.
 
Kila sekta watu wanaishi kama kiurefu wa kamba,yaani ni tafrani.
Najiuliza hivi kweli BOT kwa kushirikiana na vyombo vya dola wameshindwa kufanya hata msako wa kushitukiza kwenye hizi microfinance kubaini kasoro mbalimbali kama vile kukaa na kadi za benki za wateja wao?

Nahisi huenda baadhi ya haya makampuni ni ya wakubwa huko serikalini na ndio maana wanaishia tu kutoa Press release waonekane wanafanya kazi.
 
Najiuliza hivi kweli BOT kwa kushirikiana na vyombo vya dola wameshindwa kufanya msako wa kushitukiza kwenye hizi microfinance kubaini kasoro mbalimbali kama kukaa na kadi za benki za wateja wao?

Huenda baadhi ya haya makampuni ni ya wakubwa huko serikali ndio maana wanaishia tu kutoa press release waonekane wanafanya kazi.
Hawajaamua tu,siku wakitapeliwa watoto wa vigogo mbona hao wakopeshaji waovu ni siku Moja tu hutawaona tena.
 
Back
Top Bottom