TAKUKURU chunguzeni utajiri wa timu ya SINGIDA BIG STARS.

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,673
22,264
Ni wazi SINGIDA BIG STARS ilianza kuonesha ukwasi baada msingida mshika kibubu chetu kuteuliwa, huyu mheshimiwa alianza na matengenezo ya viwanja vyetu vya mpira vilivyoporwa na CCM kukarabitiwa kwa kutumia pesa za serikali! Leo nimesikia klabu hiyo imemlipa mchezaji shs 100,000,000/=! Ili aendelee kuichezea klabu, pia klabu inawachezaji wa kutoka kwa wenye mpira wao! Hawa wote naamini malipo yao pia yamenona.
TAKUKURU ni vizuri wananchi tujue isije ikawa kibubu chetu kinakaushwa kwani hivi sasa ukaushaji ndio umeshamiri kila kona.
 
Unaiomba Takukuru hii hii ambayo uwezo wake wa kuchunguza kesi za rushwa ni ule wa kiasi cha elfu 50 tu za wale mahakimu wetu wenye njaa!!

Siku ya kumiliki vyombo huru vya uchunguzi, hakuna atakaye iibia nchi mchana kweupe. Ila kwa sasa, jitahidi tu kusahau.
 
Hakuna haja ya takukuru kuingilia hapo.

Solution ni vilabu vya mpira kushurutishwa kujiondesha katika structure kampuni. Na hiyo itakuwa rahisi kuweza ku monitor sources zote za mapato na matumizi, na hata kwenye masuala mazima ya kulipa kodi.

Hiyo inatakuwa ku apply kwa vilabu vyote vya mpira Tanzania.

Sema mamlaka zimelala sana hata wanasiasa wanashindwa kuona hizi house keeping rules zinakuwepo kila mahali.

Huwezi kutegemea Takukuru wafanya kila kitu, hiyo ni ngumu
 
Ni wazi SINGIDA BIG STARS ilianza kuonesha ukwasi baada msingida mshika kibubu chetu kuteuliwa, huyu mheshimiwa alianza na matengenezo ya viwanja vyetu vya mpira vilivyoporwa na CCM kukarabitiwa kwa kutumia pesa za serikali! Leo nimesikia klabu hiyo imemlipa mchezaji shs 100,000,000/=! Ili aendelee kuichezea klabu, pia klabu inawachezaji wa kutoka kwa wenye mpira wao! Hawa wote naamini malipo yao pia yamenona.
TAKUKURU ni vizuri wananchi tujue isije ikawa kibubu chetu kinakaushwa kwani hivi sasa ukaushaji ndio umeshamiri kila kona.
Labda waje TAKUKURU ya Ukrane
 
Huyu mpishi wa nyama ukifuatilia kwa karibu bakuli lake limejaa minofu ila anatuambia sufuria la nyama liko salama, na unaweza kukuta lile neno stupid halimhusu yeye na huenda linawahusu watu hewa, maana bongo hewa zimejaa kila mahala kuanzia kwa watumishi hewa nk.​
 
Kichekesho! Timu changa kama hiyo lini imekuwa tajiri ndio kwanza iko ligi msimu wa kwanza? Huo utajiri uko wapi mbona haunekani, au ni hao wafadhili wake wengi makampuni makubwa maarufu? Hebu tulieni kwanza timu ikomae ndio muanze kuchunguza utajiri wake
 
Back
Top Bottom