Elfu 50 yako tu itakavyokuzawadia 'Eden' ya Serengeti - UVCCM Singida

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
104
477
ELFU 50 YAKO TU ITAKAVYOKUZAWADIA "EDEN" YA SERENGETI - UVCCM SINGIDA.

Nilipofaulu kidato cha nne Puma Sekondari Singida nikapangiwa kidato cha tano na sita Shule ya Sekondari Lufilyo, Mbeya mkabala na nyumbani kwake Prof Mark Mwandosya ambapo ndio ulikuwa mwanzo mwanzo wa kuanzishwa A level, hivyo kidato chetu chote tulikuwa HGL (History, Geography na Language) tukitoka mikoa takribani yote nchini.

Moja ya vitu ambavyo sitovisahau hapo shuleni ni kwamba nilipofika na kukutana na wanafunzi tu, majina yetu halisi tuliyaacha tukaitana majina ya mikoa tuliyotoka, mimi niliitwa "Singida" na hadi leo hii wananiita hivyo, na nami najivunia jina hilo, si kwa nia mbaya ya kustwawisha ukanda ila ni kama tu kuenzi utamaduni wa pahala tuliozaliwa.

Hakika tukiachana na binafsi kujivunia Tanzania yangu, sioni haya pia kutangaza "interest" kwamba najivunia Singida nilipozaliwa.

Singida kwetu ndipo ukija utakutana na makabila makuu-wenyeji Wanyaturu na wanyiramba yenye sifa kuu ya ukarimu, kujiamini na uchapa kazi, vyakula vya asili kama ugali wa uwele, mlenda na maziwa matamu ya mtindi ya ng'ombe. Hutakosa pia kuona pori la Itigi "Itigi thickets" lenye vichaka vya miti adimu visivyopatika popote duniani.

Ukitalii Mkoa wa Singida pia hutakosa kushangazwa na nyumba za asili za kujengwa kwa miti, fito na kuezekwa paa lake na udongo almaarufu kama "tembe" ambazo ni Imara mno kiasi cha kwamba hata mvua inyeshe vipi hazivuji.

Tukiachana na historia tamu za viongozi wa kale waliotawala ndani ya Mkoa wa Singida, waliopambana na Wakoloni kama Mama Litri aliyewashinda Wajerumani kwa nyuki; ukiwa Singida utaweza kukutana pia makabila ya Wahadzabe na Watindinga ambao hadi leo wanaishi msituni waki-enjoy dunia yao kwa kula wanyama pori, asali na matunda mwitu. Mambo hayo!!

Singida ndio Mkoa wa pekee nchini wenye kijana mdogo tu aitwaye "Kiemi" mwenye miaka takribani 35 aliyeanzisha mradi mkubwa wa ufugaji nyuki kibiashara ambao wenye viwanda vya kuzalisha mazao yote ya nyuki ikiwemo asali, Chavua ya nyuki (Vumbi la Singida), Nta, maziwa ya nyuki, supu ya nyuki na kadhalika ambao unaitwa Kijiji cha Nyuki Singida ambao kampuni yake ya Kijiji cha Nyuki ilialikwa Mkutano Mkuu wa wafugaji nyuki duniani utakaofanyika Istanbul Uturuki Agosti 24-28 mwaka huu. Sio kivutio hiki?

Kabla sijawaambia kuhusu timu bora kabisa ya mpira Tanzania na Afrika Mashariki ya SINGIDA BIG STARS, niseme tu hili la vivutio vya Mkoa wa Singida naomba nilitafutie muda mwingine nije niwaandikie, leo naomba niwakaribishe katika safari adhimu ya kwenda "kumwagilia akili, moyo na mwili" Katika Hifadhi namba mbili kwa ukubwa nchini ukiachana na ile ya Ruaha inayoshika namba moja; Hifadhi ya Serengeti. Safari iliyoandaliwa na vijana makini kabisa za Nchi yetu ya Tanzania, vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM Mkoa wa Singida, safari iyobatizwa jina la "UVCCM SINGIDA SERENGETI ROYAL TOUR"

Vijana hawa wakiwa na baraka tele za Chama kwa ngazi zote ikiwemo ngazi ya Mkoa hadi Taifa, wametuletea hili tukio la furaha likiwa na shabaha kuu ya kuunga mkono hatua ya kistoria na inayoendelea KUTUHESHIMISHA duniani, ya Rais Samia kurekodi filamu ya Royal Tour inayoendelea kutumwagia "mafuriko" ya Watalii kila pande ya dunia.

Yeyote yule awe wa Mkoa wa Singida au Mkoa mwingine nchini, awe Mwanachama wa CCM au Chama kingine, asiye na chama, Mzee au kijana, msomi ama hajaenda Shule ili ashiriki safari hii atatakiwa kulipa shilingi elfu 50 kwa namba 0656756372 au 0786355523.

Ambapo elfu 50 hiyo ni tiketi yako ya kwenda, kuingia na kutoka Serengeti, kulala ISIPOKUWA TU CHAKULA UTAJITEGEMEA. Safari itaanza Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Septemba 2 hadi 4 mwaka 2022 itapokoma huku ikikuacha umeshiba uzuri wa Urithi huu wa Dunia, Serengeti.

Ingawa kwa kukudokezea tu kampuni ya KIJIJI CHA NYUKI itakupatia Chai ya asali ya bure itokanayo na asali ya Singida "Ifoneo" wakati unaelekea Serengeti ambayo ni tiba ya magonjwa mbalimbali mwilini mwako. Kijiji cha Nyuki oyeee!!

Kwa wasiojua upekee wa Hifadhi ya Serengeti; kwa ufupi ni kwamba;

Hifadhi ya Serengeti iliyoanzishwa mwaka 1951 yenye ukubwa wa kilometa za mraba 14,763 ikiwa ni Hifadhi ya Taifa ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,226 ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.

Makala mbalimbali za utafiti zinasema neno Serengeti linatokana na neno la kimasai la "sirenget" lenye maana ya uwanda mpana wa nyasi fupi, malisho mengi na maji ya kutosha pengine ndiyo maana hifadhi hiyo inapewa majina mengi kama vile lulu, bustani ya Afrika na Edeni ya Afrika kutokana na utajiri wa maliasili uliopo ndani ya hifadhi hii ambayo kwa mara kadhaa imekuwa ikichukua tuzo ya kuwa Hifadhi bora mfululizo Afrika, na hata kuchaguliwa kuwa mshindi wa vivutio vya utalii duniani na kampuni ya Tripadvisor.

Umaarufu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti unatokana na kuwa na misururu mirefu ya nyumbu wanaohama kwa makundi na kuvuka hata mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara nchini Kenya ambapo takwimu za TANAPA zinaonyesha kuwa kila mwaka zaidi ya nyumbu milioni moja,pundamilia 200,000, swala tomi zaidi ya 300,000 na pofu 12,000 huunga misafara ya kutafuta malisho na maji.

Nani hapendi kuona maajabu haya dunia kwa elfu 50 tu ya kitanzania?

Sio hivyo tu, ni nani huyo asiyependa kukipa pepo ndogo kichwa chake kwa kupanda "balloon" na kuitazama kwa chini Hifadhi hii tambarare iliyosheheni wanyama wote wakubwa "BIG 5" na wanyama wengine ambao wengi wetu tumeishia kuwaona kwa televisheni ya "Tanzania Safari"?

Mwenzenu nayasema haya kwasababu nilishaenda Karibuni kupitia project ya Kimataifa ya Miss Jungle International kama mmoja ya waratibu wake, hakika jamani Serengeti patamu sana, na ndio maana nami sitokosa hii safari pia kwani kiu ya kuitakii Hifadhi hii pale iko pale pale.

Imagine nikiwa na Miss Jungle International tulifanikiwa kumwona Simba kadha wa kadha pembeni ya barabara wakiwanyemelea swali, akiacha na wewe utapoenda utapata kuona pia chui na wanyama wengine ambao wako hatarini kutoweka katika uso wa dunia kama faru na duma.

Hapa nimekumegea kidogo tu, usisahau pia utaenda kulala kwenye Tents, nyumba ambazo kimsingi ni "adventure" kwako, raha sana humo, unalala huku unawasikia simba, tembo, fisi na kadhalika wanalia mita moja nje ya tent lako.

KOSA, UPITWE!!
KAZI IENDELEE!!

Suphian Juma Nkuwi,
Mdau kindakindaki wa Utalii.
Singida, Tanzania.
Agosti 31, 2022.

IMG-20220830-WA0004.jpg
 

Kalpana

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
13,803
20,756
Huyo wa kijiji cha Nyuki ndo mwenye maduka ya kijiji cha nyuki hapa Ilazo Dodoma?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom