Singida Big Stars yatarajia kwenda Rwanda kucheza na Rayon Sports FC

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
893
1,936
Watu wa Soka,

Tunapenda kuwafahamisha wapenzi, wadau na mashabiki wa klabu ya Singida Big Stars kuwa tumepokea mwaliko kutoka kwa wenzetu Rayon Sports FC ya nchini Rwanda kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Timu yetu inatarajia kusafiri kuelekea Rwanda siku ya Ijumaa ya tarehe 02/09/2022 kwa ajili ya mechi hii ambayo inatarajiwa kuchezwa tarehe 04/09/2022 katika Uwanja wa Nyamirambo uliopo mjini Kigali.

Mwaliko huu umekuja wakati sahihi ambapo timu zote mbili zipo kwenye mapumziko mafupi ya Ligi, hivyo tutautumia mchezo huu kwa ajili ya kuendelea kujiandaa vyema na msimu mrefu wa Ligi Kuu 2022/2023.

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Klabu ya Singida Big Stars inaishukuru Rayon Sports FC kwa mwaliko. Pia kwa kugharamia safari nzima ya kikosi chetu pamoja na baadhi ya viongozi watakaoambatana na timu katika kipindi chote timu itakapokuwepo nchini Rwanda hadi kurejea nyumbani Singida, Tanzania.
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
6,265
4,570
Kila la kheri

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
7,140
7,451
Yanga yupo coco beach akijiandaa na mazoezi ya jinsi ya kumfunga simba taifa estadio de utopolo.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
17,070
46,618
Yanga yupo coco beach akijiandaa na mazoezi ya jinsi ya kumfunga simba taifa estadio de utopolo.
Hupendi kabisa kuona yimu yako inafungwa na Yanga! Kuwa mpole tu Mkurugenzi.
Msimu uliopita, timu zilizokoswa kufungwa na Yanga, basi ziliishia tu kupata sare. Kwa hiyo Yanga inampiga yeyote yule! Siyo simba pekee.

Na msimu huu Kimataifa tunaanza na ile timu ya Sudan Kusini! Na wenyewe tutawapiga kama ilivyo desturi yetu ya kutembeza kichapo kwa yeyote yule atakaye ingia kwenye 18 zetu.
 
goroko77

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
8,443
11,553
Inasemekana timu inaongozwa na tozo zetu je kunna ukweli wowote

Kwanin mlibadili jina la timu kutoka dimond. Bank nakuwa sbs.

Mwenye timu Ni Nani haswa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom