FT: Singida Big Stars 1-1 Simba SC | Ligi Kuu Bara | Uwanja wa Estadio de Liti 09/11/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kuvurumishwa leo November 9, 2022 kwenye Uwanja wa Estadio de Liti mkoani Singida ambapo Walima Alizeti Singida Big Stars ambao ni wenyeji, wanamkabili vikali Mnyama Mkali Mwituni Simba SC

Mechi inatarajiwa kuwa ni ngumu sana na ya kusisimua kwa muda wote wa mchezo kutokana na kila timu kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza walau kupata ushindi dhidi ya mpinzani wake.

Timu zote zina alama 17 kwenye msimano wa Ligi Kuu lakini wakiwa nafasi tofauti kutokana na mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo basi tutegemee kuona ushindani wa kweli na burudani ya aina yake ndani ya dakika 90 za jasho na damu.

Kumbuka mchezo kwa saa za Afrika Mashariki ni kuanzia saa 10:00 Alasiri.. Usikose Ukapata Simulizi Jikite Hapa Hapa JF

...Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana...

================

01' Kabumbu limeanza uwanja wa Liti, mkoani Singida

07' Phiri anafika lango la Singida, mpira unaenda pembeni ya lango. Goal kick.

09' Singida wanapata kona, inaingizwa kati bila kuzaa matunda

11' Goooooooooooooaaal Deus Kaseke anaiandikia Singida bao la kwanza, Singida 1-0 Simba

Simba SC wanapata Kona mbili mfululizo ambazo hazikuzaa bao.

Mpira ni mkali huku Singida wakitumia kupiga mipira mirefu kuelekea lango la Simba.

23' Haya Singida wanapiga mbele lakini golikipa Beno anatokea na kudaka, ilikuwa hatari sana

29' Mpira wanao Simba mbele kuleee lakini Sakho anaangushwa, lakini Refa Sasii anakataa.

Carno anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Kibu

Wameanza kulala kama Waarabu, Batambuzi yupo chini akigaagaa uwanjani.

40' Kapombe anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya, Pressure ni kubwa kwa pande zote mbili

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo Singida Big Stars wapo mbele kwa bao moja huku Simba wakifanya majaribio ya kusawazisha

Naaam mpira ni mapumziko

HT: Singida Big Stars 1-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi

46' Kibu anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Singida

Banda ameingia kuchukua nafasi ya Mkude Simba SC

Kona inapigwa kuelekea Singida Big Stars na Shomari Kapombe

50' Inapigwa Kibuuuuu anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango

Simba SC wanashambulia lango la Singida kutafuta nafasi ya kusawazisha bado, mpira hautoki kwao

54' Unarushwa mpira Lakini wanakaa vizuri kwakwe Hussein anamtafuta Phiri

Kapombe anapiga Krosii, lakini wanapoteza umakini Simba

59' Banda Goooooooooooooaaal gooal..Peter Banda anasawazisha Simba bao kwa Krosi na kwenda moja kwa moja | Singida Big Stars 1-1 Simba SC

61' Kibu anauruka mpira ambao ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga, namna gani Kibu

64' Kibu anakwenda kulee lakini shuti kali linadakwa na golikipa, ilikuwa nafasi kwa mara nyingine

Ndemla anapiga shutii lakini mpira unatoka sentimita chache ya lango la Simba

67' Bruno anacheza madhambi kwa Henock, ni Free Kick kuelekea Singida Big Stars

Peter Banda anamchekecha beki wa Singida, anapiga Krosi lakini Shuti la Phiri ninatoka nje.

74' Ametoka Kibu na ameingia Kyombo upande wa Simba SC.. Umiliki wa mpira Simba

Dario anapambana na Kapombe lakini mpira wanao Singida Big Stars

81' Hussein anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Singida Big Stars

84' Almanusura Singida Big wapate bao kwa mpira wa Kona ilikuwa hatari sana lango.

87' Kaseke anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumzuia Refa kufanya majukumu yake ni faulo kuelekea Singida.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

Mchezaji wa Singida Big Stars yupo chini anapoteza muda, Refa Sasii naangalia saa yake.

Naaam mpira umekwishaaaaaa

FT: Singida Big Stars 1-1 Simba SC
 
Kuelekea kwenye mchezo huu wa leo November 9, 2022

Simba SC inakosa huduma ya Kiungo Mshambuliaji hatari mwenye uwezo wa kukusanya Kijiji na kuwatupa kunako Lupango, Clatous Chama, kutokana kufungiwa michezo mitatu ya Ligi Kuu na Bodi ya Ligi.
 
Back
Top Bottom