TAHADHARI: Vijana wengi wanapoteza muda Dar es Salaam

Nakwambia hivi, unaweza kusema hivyo vitu anavijua kwa sababu wabongo mna tabia ya kujimwambafy kwamba mnajua mambo msiyoyajua, na wengi wenu mnafikiri sawa kama watoto wavivu wa kufikiri nyumba moja.

Haya mambo watu wanayasomea na kuyachunguza kwa kina mpaka level ya Ph.D, halafu wanasema "uchunguzi zaidi unahitajika".

Ila hapa JF anakuja ngumbaru mmoja kapita mjini kaona watu kwa mbali hata hajakaa nao kuwahoji maisha yao yakoje, kwa nini wako hapo walipo, kwa nini hawaendi kulima vijijini, tofauti ya mjini na vijijini/mikoani ni nini, mtu anahukumu kirahisi tu.

Halafu anakuja JF na uzi.

Ndiyo maana nakwambia Watanzania wengi, si wote, wengi, ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kuhusu mambo wasiyofahamu, kwa watu wasiowajua.
"Ila hapa JF anakuja ngumbaru mmoja kapita mjini kaona watu kwa mbali hata hajakaa nao kuwahoji maisha yao yakoje, kwa nini wako hapo walipo, kwa nini hawaendi kulima vijijini, tofauti ya mjini na vijijini/mikoani ni nini, mtu anahukumu kirahisi tu."
[emoji115]

Kimsingi alitakiwa awahoji, kama ni mistake kaifanya hapa. Upo sahihi.
Ila bado nia yake ni njema hata kama kuna baadhi ya changamoto kwenye uwasilishwaji. Binafsi nimebahatika kujionea kwa macho maisha ya wengi kwenye jamii nyingi hapa DSM. Hayaridhishi.! Maono yangu hayatofautiani sana na ya mtoa mada.
 
"The road to hell is paved with good intentions"

[emoji115]
Hiyo ni assumption tu ambayo inaweza kuakisi uhalisia wa kilicholetwa na mtoa mada, au isiakisi.

Point is, mtoa mada katoa ushauri kwa vijana wanaojijua wanaishi Dar maisha ya kubangaiza na hawaoni dalili za mafanikio kesho yao kuwa wakajaribu mikoani.

Shida yako we hujitambui

Hapo juu umesema una connection kubwa hapa mjini mbona ndugu zako huko kwenu wanaangaika kutafuta kazi why usiwalete dar ninyi ni aina ya watu mnaotaka kuonekana mko perfect wakat hamna uperfect wowote
 
"The road to hell is paved with good intentions"

[emoji115]
Hiyo ni assumption tu ambayo inaweza kuakisi uhalisia wa kilicholetwa na mtoa mada, au isiakisi.

Point is, mtoa mada katoa ushauri kwa vijana wanaojijua wanaishi Dar maisha ya kubangaiza na hawaoni dalili za mafanikio kesho yao kuwa wakajaribu mikoani.
Mafanikio ni nini?
 
"Ila hapa JF anakuja ngumbaru mmoja kapita mjini kaona watu kwa mbali hata hajakaa nao kuwahoji maisha yao yakoje, kwa nini wako hapo walipo, kwa nini hawaendi kulima vijijini, tofauti ya mjini na vijijini/mikoani ni nini, mtu anahukumu kirahisi tu."
[emoji115]

Kimsingi alitakiwa awahoji, kama ni mistake kaifanya hapa. Upo sahihi.
Ila bado nia yake ni njema hata kama kuna baadhi ya changamoto kwenye uwasilishwaji. Binafsi nimebahatika kujionea kwa macho maisha ya wengi kwenye jamii nyingi hapa DSM. Hayaridhishi.! Maono yangu hayatofautiani sana na ya mtoa mada.
Hata yule kijana aliyejirusha kutoka ghorofani pale Morogoro Road akaangukia kwenye Simtank na kufa, akiamini kwamba yale maji ya kwenye Simtank yangemuokoa asife, alikuwa na nia njema ya kutuonesha umahiri wake katika mchezo mpya wa kuruka kutoka ghorofani.

Nia njema inaweza kukuua, tuongelee usahihi na tija ya mantiki katika hoja, sio nia.

Na kwenye usahihi na tija ya mantiki kwenye hoja, ushakubali kwamba mtoa mada kakurupuka kuwahukumu watu kabla hata ya kuwahoji awaelewe.

Kwa mtaji huu, unaweza kumlaumu victim wakati anayestahili lawama umemuacha.
 
Kukaa jijini dar na kukaa mkoani ni magereza ila utofauti wa mikoani na dar ni rahisi kutoboa ukiwa dar kuliko mikoani kutokana na mzunguko mkubwa wa hela uliopo dar.
mikoani wilaya unamznguko mkubwa wa pesa tatizo akili yako aina mzunguko
 
Ila angekaa kijijini angechakaa zaidi hata hiyo 5000 hangeipata. Mjini ukiwa na nidhamu ya pesa na usichague kazi unatoboa kuliko kijijini.
nani kakudanganya tumeshi dar tunapajua pia kijijini tunapa jua dar kama ujawekeza utabaki kuangaikia pesa ya nauli na kodi ya chumba na kutu
 
IMG_4369.jpg

Haya tunakuja mkoani
 
Kiuchumi mzunguko wa pesa mjini ni mkubwa kuliko kijijini. Mf. Fungua duka Manzeze na mwingine afungue kijijini, atakaeuza kwa wingi ni nani? Mjini omba tu usiugue kwani hakuna cha Bure ila ukichakarika sio sawa na kijijini. Hata kama huna duka, basi beba mizigo ya dukani ulipwe. Kuna jamaa anatembeza mikate kwa baiskeli juzi kanunua kiwanja. Kijijini utamtembezea nani mikate?
 
Nakwambia hivi, unaweza kusema hivyo vitu anavijua kwa sababu wabongo mna tabia ya kujimwambafy kwamba mnajua mambo msiyoyajua, na wengi wenu mnafikiri sawa kama watoto wavivu wa kufikiri nyumba moja.

Haya mambo watu wanayasomea na kuyachunguza kwa kina mpaka level ya Ph.D, halafu wanasema "uchunguzi zaidi unahitajika".

Ila hapa JF anakuja ngumbaru mmoja kapita mjini kaona watu kwa mbali hata hajakaa nao kuwahoji maisha yao yakoje, kwa nini wako hapo walipo, kwa nini hawaendi kulima vijijini, tofauti ya mjini na vijijini/mikoani ni nini, mtu anahukumu kirahisi tu.

Halafu anakuja JF na uzi.

Ndiyo maana nakwambia Watanzania wengi, si wote, wengi, ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kuhusu mambo wasiyofahamu, kwa watu wasiowajua.
mkuu niombe msamaha mimi sio ngumbaru...nina diploma ya ustawi wa jamii, diploma ya uuguzi na ukunga na shahada ya miradi (project planning)
 
Back
Top Bottom