TAHADHARI: Vijana wengi wanapoteza muda Dar es Salaam

TAHADHARI: Vijana wengi wanapoteza muda Dar es Salaam

umenishema mimi nafanya kazi sokota kwenye kiwanda cha nondo kutwa sh 8000 kazi ngumu moto mkali sana

nauli kwenda na kuludi sh 1200
chai 1000
mchana 1500
maji 1000

salio 3700

bado familia inataka kula kodi ya nyumba kutibiwa kuvaa

nauli ya juludi kijiini kwetu sina umri wenyewe umesha nipa kwaheli miaka 40 sasa hehe hatari
Kwanini usibebe maji na msos toka nyumbani kupunguza gharama?
 
Sometimes hua inatokea Unarudi home kusalimia from daslam umeshine na kasmartphone kakuzugia unakuta Kuna baadhi madogo uliowaacha kitaa wamejenga na wana familia maisha yanaenda. Mbaya zaidi ukijitafakari life lako uko dar unajihurumia mwenyew ila ni siri yako tu, nimeshuhudia sana lifestyle ya vijana wa namna hii na mm mwenyew nilikua mmoja wao kabla ya kuamua kurudi home kufanya kilimo na kazi nyinginezo

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kwa mtoa mada anaombwaje atoe ushauri humu JF? Unajuaje je, kuna watu walimuomba awashauri huko mtaani?

Nia yake ni njema, kutokana na kushuhudia na kuumia ameamua kutoa ushauri, kama mtu anajijua mhusika anaweza kuuchukua au kuuacha. Ni mawazo huru na si lazima.

Mtoa mada ni moja ya aina ya vijana tunaowataka kama Taifa kwa sababu ni wasema kweli. Kaongea ukweli tupu.
Hajasema nani kamuomba ushauri.

As for "Nia yake ni njema..."

Waingereza wana msemo, "The road to hell is paved with good intentions".
 
Ni kama wewe Kiranga ndiyo hujaelewa mada na umekurupuka. Umeandika above kuwa Wabongo ni mabingwa kushauri pale wasipoombwa KWA VITU WASIVYOVIJUA. Sasa kakujibu kuwa hivyo vitu anavyoshauri anavijua na ndiyo maana kashauri.

Mzee una kichwa kigumu mno
Nakwambia hivi, unaweza kusema hivyo vitu anavijua kwa sababu wabongo mna tabia ya kujimwambafy kwamba mnajua mambo msiyoyajua, na wengi wenu mnafikiri sawa kama watoto wavivu wa kufikiri nyumba moja.

Haya mambo watu wanayasomea na kuyachunguza kwa kina mpaka level ya Ph.D, halafu wanasema "uchunguzi zaidi unahitajika".

Ila hapa JF anakuja ngumbaru mmoja kapita mjini kaona watu kwa mbali hata hajakaa nao kuwahoji maisha yao yakoje, kwa nini wako hapo walipo, kwa nini hawaendi kulima vijijini, tofauti ya mjini na vijijini/mikoani ni nini, mtu anahukumu kirahisi tu.

Halafu anakuja JF na uzi.

Ndiyo maana nakwambia Watanzania wengi, si wote, wengi, ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kuhusu mambo wasiyofahamu, kwa watu wasiowajua.
 
Hajasema nani kamuomba ushauri.

As for "Nia yake ni njema..."

Waingereza wana msemo, "The road to hell is paved with good intentions".
"The road to hell is paved with good intentions"

[emoji115]
Hiyo ni assumption tu ambayo inaweza kuakisi uhalisia wa kilicholetwa na mtoa mada, au isiakisi.

Point is, mtoa mada katoa ushauri kwa vijana wanaojijua wanaishi Dar maisha ya kubangaiza na hawaoni dalili za mafanikio kesho yao kuwa wakajaribu mikoani.
 
Back
Top Bottom