Nipo Dar es Salaam ni wiki ya pili sasa toka nimetoka Dodoma kuja huku Dar es Salaam kushughulikia mambo yangu ya kikazi.
Nimefuatilia na kuchunguza kusema ukweli vijana wengi wanapoteza muda, vibarua wanavyofanya wanaishia kulipwa 4,500 mpaka 7,000 na hapo ale chakula avae apendeze na mengineyo
Jioni vijana wanataka wale starehe za Dar es Salaam, mwisho kijana anabaki hana kitu huku akijipa matumaini ya ipo siku kutoboa.
Umri wa miaka 35 mpaka 45 unaona ramani haisomi hama haraka hapo Dar es Salaam utakuja kudhalilika
Mkuu
Mwizukulu mgikuru natamani nisikubaliane na wewe ila sasa najikuta sina budi nikubaliane na wewe maana uhalisia unaongea kuliko longolongo.
Watakubishia wengi hapa jamvini na hawatakuelewa ila sasa naomba tu niwaulize wadau mafanikio ni nini ? Na ndoto ni nini ? Hasa za vijana .
Kibongo mafanikio ni pale kijana awe na nyumba , aoe ili jamii imuheshimu na pia aweze kutoa msaada mdogo mdogo katika jamii yake alikotoka ili jamii ione fahari kuwa na mtoto kama huyo .
Sasa kijana wa mkoa aliyemaliza chuo akasema wacha nitafute maisha mjini
Mfano yuko kiwanda cha Cello analipwa kwa wiki elfu (21000) baada ya makato au yupo viwanda vingine ila kaeni mkijua hakuna kiwanda utalipwa zaidi ya elfu saba hapo bado makato ya hapa na pale lakini pia usisahau yawezekana anatumia usafiri kufika sehemu takiwa .
Ndugu huyu kijana unahisi hata akifanya kazi miaka kumi anatengeneza nini ? Je atakuwa na mpango wa kuhama hapo kwa baba mwenye chumba ambaye kamstiri maana hata kusema ataishi kwenye chumba cha elfu hamsini ni uongo .
Ila ikiwa anatoka mikoa yenye kilimo mfano mbeya na wana vipindi vya mavuno na pia wanaingiza hela kiasi kizuri kila kipindi cha mavuno je ni sahihi kubaki mjini kupambania kula na kuvaa huku akiiishi nyumba asiyokuwa na matumaini yake mvua ikinyesha sana huko keko , Tandika na Mwananyamala?
Vijana mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa wasikudanganyeni hawa kaka zenu hapa jukwaani kwakuwa wao walitoboa wakiwa mjini miaka hiyo ila jueni zama zimebadirika siku hizi mjini kazi ni huko viwandani na kwingine kwenyewe makampuni ya usafi tu hivyo haiwezi kuwafanya kutobaoa .
Hao zamani walipiga dili feki wakapata hela , zamani ujanja wako ndiyo hela yako ila sio sasa mambo yamebadilika sana .
Ukiweza rudi kijijini kajipambanue vizuri kule kula uhakika maana vyakula mnalima wenyewe uzuri vijijini mnakotoka hakuna habari za kuwa na mtaji ndiyo ufanye biashara maana wazee wenu wangali na mashamba hivyo kilimo bado kina unafuu kwenu hivyo kalimeni .
Mimi nawakumbusha kuwa mjini bila hela ya uhakika au mzunguko mzuri ni kupoteza muda na kujizeesha kwa kazi za wahindi na mtazeeka mkiwa vibarua maana hata connections hamna hivyo nisiwadanganye mtapata ajira ni uongo nisiotaka kuwaaminisha .
Japo maamuzi ni yenu kuendelea kuvaa nguo nzuri huku una uhakika na future yako au kuwa na uhakika wa future yako ukiwa uko sawa kabisa.
Asanteni.