Nipo daressalam ni wiki ya pili sasa toka nimetoka dodoma kuja huku daressalam kushughulikia mambo yangu ya kikazi, nimefuatilia na kuchunguza kusema ukweli vijana wengi wanapoteza muda, vibarua wanavyofanya wanaishia kulipwa 4500 mpaka 7000 na hapo ale chakula avae apendeze na mengineyo jioni vijana wanataka wale starehe za Daressalam, mwisho kijana anabaki hana kitu huku akijipa matumaini ya ipo siku kutoboa. Umri wa miaka 35 mpaka 45 unaona ramani haisomi hama haraka hapo Daressalam utakuja kudhalilika