TAHADHARI: Tukateni miti iliyokaribu na nyumba au umeme kuepusha maafa kipindi hiki cha mvua iliyoambatana na upepo

Zogolo1550

Member
Dec 2, 2018
32
15
Nawasihi sana kukata miti iliyo karibu na nyumba au umeme/ nguzo kwa kipindi hiki cha mvua iliyoambata na upepo.

Leo maeneo mbalimbali Dar es Salaam miti imeleta maafa makubwa kwa mfano nyumba mbili zimeangukiwa na miti maeneo ya Mbezi Makabe na maeneo ya Sinza mti umeangukia gari iliyokuwa imeegeshwa.

Miti hatari zaidi ni aina ya galveria kwani ni rahisi kun'goka inapopigwa upepo.

Nimejua hayo kwasababu Mimi ni mtaalamu wa kukata miti kwa kutumia machine (chainsaw) kwahiyo unajua jinsi niliyohangaika leo kuokoa maisha ya watu!
 
Inaitwa Gravelia bwana

Halafu hata kwetu muembe umedondoka ukakata waya wa tanesco
 
Nawasihi sana kukata miti iliyo karibu na nyumba au umeme/ nguzo kwa kipindi hiki cha mvua iliyoambata na upepo...
Wewe mjanja sana naona unatafuta tenda ya kukata miti ili upate mbao, sababu uliyotoa haina mvuto kwani miti huanguka na kama unaona inao basi bora tuondoe waya zote za umeme kwani nazo hukatika wakati wa mvua na kuleta hatari kuliko miti.
 
Shida yangu sio mbao wala kujitangaza kupata tenda kwa sababu nilichokisema ni kweli kimetokea sehemu mbalimbali kwahiyo kupata tenda si lengo kuu.
 
Asanteh kwa kunirekebisha Mimi si mtaalamu sana wa botanical science especially taxonomy of higher plants!! Bila shaka kwa wale ambao wanaona najitangaza watapata ushahidi wa kutosha!
Inaitwa Gravelia bwana

Halafu hata kwetu muembe umedondoka ukakata waya wa tanesco
 
Shida yangu sio mbao wala kujitangaza kupata tenda kwa sababu nilichokisema ni kweli kimetokea sehemu mbalimbali kwahiyo kupata tenda si lengo kuu.
Hayo matukio mawili hayana mvuto kwani zipo nyumba na magari vilivyowahi kuangukiwa huku kukiwa hakuna mvua. Miti yote mijini ipo karibu na nyumba na kando ya barabara hivyo tukiikata hatutukuwa na miti mijini, pia watu wenye chainsaw huwa ndio wanaoongoza kwa uharibifu na kupelekea serikali kuzifuatilia sana.
 
Unajitahidi kuficha ukweli lakini hujui nini unaongea, tafuta majibu ya haya maswali .je ni kweli serikali hairuhusu hairuhusu matumizi ya chainsaw?, je nini kilitokea baada ya hizo nyumba,umeme na gar kuangukiwa na miti?
 
Mimi ni mpandaji mkubwa wa miti na laiti ningejua uko wapi ningekuchukua uone jinsi nilivyopanda miti mingi na maua nyumbani pangu wakati wewe haujawahi kupanda hata mti mmoja, ukisema niweke picha naweza kuweka japo inaweza kuwa si ya nyumbani pangu, pia ujue ukiukata mti mmoja eti kwa sababu ya upepo na mvua hautaurejesha kwa zaidi ya miaka minne, pia miti huzuia upepo kuidhuru nyumba yako.

Kwa tamaa yako ya kukata mbao uliamua kununua huo msumeno na nyie ndio mmekata miembe asilia na miarobaini kwa ajili ya mbao za kutengeneza vitanda pia mmewashawishi wasiojua manufaa ya miti wawauzie miti iliyopo kwenye maeneo yao.

PANDA MTI KATA MTI.
 
nimezungumza kuhusu miti iliyokaribu na nyumba na umeme,sijui kwanini unazunguka kukwepa uhalisia, haihitaji shahada ya uhandisi kujua madhara ya mti kuangukia nyumba au umeme, pia nimetoa mfano wa miti ambayo IPO katika hatari zaidi aina ya gravelia, sijasema kuhusu mbao sasa sijui umeyatoa wapi hayo!
 
nimezungumza kuhusu miti iliyokaribu na nyumba na umeme,sijui kwanini unazunguka kukwepa uhalisia, haihitaji shahada ya uhandisi kujua madhara ya mti kuangukia nyumba au umeme.pia nimetoa mfano wa miti ambayo IPO katika hatari zaidi aina ya gravelia,sijasema kuhusu mbao sasa sijui umeyatoa wapi hayo!
Tatizo umelianzisha mwenyewe kwa kujipa sifa ya ujuvi wa kukata miti kawa kutumia chainsaw, mimi ninahasira na wenye chainsaw kwani wamekata miembe asilia na miarobaini iliyokuwa karibu na nyumba kwa kuwadanganya kwa sababu kama zako.
 
Katika hoja yangu ya mwanzo umeona kipengele cha kuchana mbao za miembe au miarobaini? Je kila mwenye chainsaw anaitumia hivyo? Unataka kuendelea kupoteza muda na nguvu nyingi kutumia shoka na mapanga? Huu ni ulimwengu wa sayansi ya teknolojia huwezi kukwepa matumizi ya mashine!!
 
Katika hoja yangu ya mwanzo umeona kipengele cha kuchana mbao za miembe au miarobaini?, Je kila mwenye chainsaw anaitumia hivyo?, unataka kuendelea kupoteza muda na nguvu nyingi kutumia shoka na mapanga?,huu ni ulimwengu wa sayansi ya teknolojia huwezi kukwepa matumizi ya mashine!!
Hauwezi kununua chainsaw kama si mkataji miti kwa wanaochana mbao, hauwezi kunidanganya na hauwezi kununua jeki kama hauna gari au si fundi gereji.
 
Back
Top Bottom