Ushauri: TANESCO itumie kipindi hiki cha mgao kufanya ukarabati wa miundombinu yake

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,730
2,082
Salamu na poleni ya wote.

Hali ni tete na ngumu lakini ndio ivo hakuna namna.Kama mkubwa kakaa chini we mdogo utafanya nn.

Pamoja na mgawo tatizo kubwa jingine kwa umeme wetu kukatika katika ni kuwa na miundo mbinu uliyokaa muda mrefu bila kufanyiwa ukaguzi au service. Yaani kutofanya gwaride la ukaguzi wa miundo mbinu ya umeme ili kujua wapi pamekaa ndivyo sivyo ili kupashughulikia mapema kabla hapajaleta shida au tatizo.Tunasubiri tatizo ndio tutoke tukatengeneze.🙁

Na hi ni kwa miundo mbinu yote ya umeme iliyopo mjini wilayani manispaa na huko maporini.

Kuna sehemu ukiangalia juu kwenye nguzo za umeme unawaza mpaka unaogopa kwa jinsi nyaya za umeme zilivyotawanyika kwenye nguzo na jinsi nguzo yenyewe ilivyosimama.

Mimi sijawahi kuona gwaride la tanesco la kupitia miundo mbinu yake labda wana utaratibu wao.

Kipindi jpm akiwa rais kuna daraja pale dumila njia ya kuelekea dodoma kutoka morogoro lilikatika likakata mawasiliano ya mikoani na dar kwa njia hiyo nakumbuka jpm alitaka kuondoka na vichwa vya watu.Lawama nyingi hapo zilienda kwenye wakaguzi.Walilala kidogo.

Mwaka huu watabiri wa hali ya hewa wamesema kutakuwa na mvua kubwa.Sasa ninavyoijua miundo mbinu yetu ya umeme nahisi tutakuwa na mabalaa mawili ya mgao wa umeme na uvurugikaji wa miundo mbinu ya umeme utakaotokana na upepo mkali na mvua kubwa ya radi na mawe.

Sasa kwa hali hi kama hakuna ukaguzi wa mapema basi tutakuwa katika hali mbaya mara mbili ya sasa. ,Kuna hatari baadhi ya maeneo kipindi hicho yakakosa nishati hata kwa siku mbili mfululizo yaani Giza siku mbili.

Sasa ndo nasema kipindi hiki cha mgao je kuna gwaride la kukagua hiyo miundo mbinu au tuna uhakika iko vizuri?

Kukagua kipindi hiki itaepusha hapo baadae kukata tena umeme kwa ajili ya matengenezo.

Miezi sita sio leo kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom