Mbunge Sylvia Sigula: Serikali Imejipanga Vipi Kuzuia Maafa Katika Kipindi Hiki cha Mvua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Sylvia Sigula: Serikali Imejipanga Vipi Kuzuia Maafa Katika Kipindi Hiki cha Mvua

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga bungeni Dodoma, ambaye amewataka Wananchi kuepuka kuishi kwenye maeneo hatarishi kama vile mabondeni na maeneo yanayopitiwa na maporomoko ya udongo.

Naibu Waziri Nderiananga alikuwa akijibu swali la Mbunge Sylvia Sigula aliyetaka kufahamu Serikali imejipanga vipi kuzuia maafa katika kipindi hiki cha mvua.

Ametaja mikakati mingine ya Serikali katika kuwaepusha Wananchi na maafa kuwa ni kutekeleza mpango wa Taifa wa kukabiliana na madhara ya Elnino kwa kipindi cha Septemba 2023 hadi Juni 2024
 

Attachments

  • maxresdefaultqaswedc.jpg
    maxresdefaultqaswedc.jpg
    119.4 KB · Views: 1
  • 04952d74-b7b6-4308-9e42-a5fb25d9c05f-1024x847.jpg
    04952d74-b7b6-4308-9e42-a5fb25d9c05f-1024x847.jpg
    97.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom