Tahadhari: Kuanzia tarehe 1 November WhatsApp kuacha kutumika kwenye baadhi ya simu za iPhone na Android

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
They are doing it again!

WhatsApp moja ya mitandao maarufu duniani ya kijamii, kuanzia jumatatu ijayo ya tarehe 1 November itasitisha kutumika kwake kwenye baadhi ya simu za iPhone na zimu za Android.

Simu zote za Android zenye toleo la OS 4.0.4 hazitaweza kutumia WhatsApp ikiwa ni pamoja na simu za iPhone ambazo watumiaji itawabidi kufanya updates ili kupata toleo jipya la iOS 10.

Kuanzia tarehe 1 November WhatsApp haitaweza kufunguka na kutumika kwenye simu hizo tajwa na vifaa hivyo havitaweza kuisaidia App hiyo kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Simu zifuatazo za iPhone ambazo zitaathirika na zoezi hilo na ambazo haziwezi kupata toleo jipya la iOS 10 ni kama zifuatazo:
  • iPhone 4S
  • iPhone SE
  • iPhone 6S
Simu za Android ambazo zitaathirika na hatua hiyo ya WhatsApp na hazitaweza kupata toleo jipya la OS 4.04 ni kama zifuatazo:
  • Samsung Galaxy Trend Lite
  • Galaxy Trend II
  • Galaxy SII
  • Galaxy S3 Mini
  • Galaxy Xcover2
  • Galaxy Core
  • Galaxy Ace 2
  • Sony Xperia Miro
  • Sony Xperia Neo L
  • Xperia Arc 5
Kwa ufupi watumiaji wa simu hizi tajwa hapo juu wanahitaji simu mpya kabisa lakini wanakumbushwa kuhifadhi historia za sogoa zao (Chat) au mazungumzo.

Simu zinginewe ambazo zitaathirika na hatua hiyo ni pamoja na HTC, Huawei, LG, Alcatel, ZTE na Lenovo.

Simu hizi zitahitaji kusasisha ili kupata toleo jipya na kuweza kuendelea kutumia mtandao wa WhatsApp.

Hivyo wakuu wote wa JF nawatakia kila la kheri katika mchakato huu mgumu na kuwakumbusha kutosahau kusasisha zimu zenu kuanzia leo hii.

Kwa taarifa zaidi na maelezo kamili na kina waweza kuingia katika jamvi la masuali na majibu la WhatsApp kupitia kiunganishi hichi: WhatsApp Help Center
 
Back
Top Bottom