Hizi ndio simu 49 zitakazozuiwa kutumia WhatsApp kuanzia 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Kila mwaka WhatsApp inajifuta simu za zamani ambazo haziwezi kuwa na uwezo wa kufanya kazi na kupata app ya WhatsApp. Hii ni kwa sababu kila muda WhatsApp inaweka mabadiliko mapya na baadhi ya mabadiliko yanahitaji simu yenye nguvu ili kuwa na uwezo wa kufanya kazi bila kusumbua na kupata features mpya.

Zaidi ya simu 49 hazitakuwa na uwezo wa kupata app ya WhatsApp kwa mwaka 2023 na mwisho wake wa kufanya kazi ni December 31.

Kwa watumiaji wa iPhone wanatakiwa kuwa na iOS 12 na kuendelea; ambapo mwakani ni mwisho kwa iPhone SE ya kwanza na iPhone 6 kupata updates. Kwa watumiaji wa Android ni kuanzia Android 4.1 na kuendelea.

Swipe kuona kuona simu ambazo zitaanza kukosa uwezo wa kuwa na app ya WhatsApp mwaka 2023.

iPhone 5, iPhone 5c

Huawei Ascend D, D1, D2, G740, Ascend Mate, Ascend P1

Samsung Galaxy Ace 2, Galaxy Core, Galaxy S2, Galaxy S3 min, Galaxy Trend II, Galaxy Trend Lite, Galaxy Xcover 2

Sony Xperia Arc S, Xperia miro, Xperia Neo L

LG Optimus L7, L7 II, L7 Dual, Nitro HD, LG Enact, Lucid 2, Optimus 4X HD, Optimus F3, Optimus F3Q, Optimus F5, F6, F7, Optimus L2 II, L3 II, L3 II Dual, L4 II, L4 II Dual, L5, L5 Dual, L5 II

Quad XL, Lenovo A820, Archos 53 Platinum, Grand S Flex ZTE, Grand X Qaud V987 ZTEM HTC Desire 500, Memo ZTE V956, Wiko Cink Five, Wiko Darknight ZT

SwahiliTek
 
Hatimaye sisi wenye tecno na infinix tunatembea kifua mbele.

Mbona takno na itel zijaziona au zenyewe zinafaa
Logic kwenye uzi ni simu ambazo zina android 4.1 kushuka,

So Zile Tecno za zamani kama P3, N3 etc zenye Android 2.3 hazitaweza ingia whatsapp.

Kifupi kuna simu zaidi ya 10,000 zina Android za zamani, haziwezi kutajwa zote, zinatajwa tu maarufu.
 
Back
Top Bottom