Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Inawezekana kabisa anaamini anafanya kazi nzuri ya kuinyosha nchi; ripoti ya CAG inaonesha vinginevyo. Hata hivyo, kuna hesabu watu hawajazipiga vizuri... mnafikiria majaji walioteuliwa hivi juzi ni kwa bahati mbaya tu...
Mwanakijiji usilewe u ccm hapa tunazungumzia pesa ambayo haijulikana imetumikaje

Yaani imeingia kwenye account haijulikani imetolewa na Nani na kufanyia nini hakuna mtu kasema imeibiwa lakini kwanini haijulikani imefanyia nini..??

By the way hakuna mtu anae kukataza kuwa na Imani na magufuli
Sisi tunauliza pesa imeenda wap basi
 
Humu JF alishajibiwa, Polepole alishamjibu jibu ambalo linafanana na jibu hilohilo alilolitoa Naibu FM leo bungeni.
Kwanini jibu litolewe wakati ukaguzi unafanyika? Kwani Prof. Assad aliuliza hilo mpaka ajibiwe? Hilo ni swali alilokuja nalo Zitto.
Pof. Assad hakuuliza swali kama hilo.
Hivi polepole ndo alipaswa kutoa jibu? Kwani yeye au ccm ndo auditee? cag alihojiwa na azam tv akasema kuna pesa zimetumika na anaamini zimetumika kwenye eti kwenye matumizimengine ya serikali ambayo hayakuwa yameidhinishwa na bunge na akataka bunge lihoji zimekwenda wapi! Je cag hapa alikuwa mjinga kutoa kauli hii? Hivi matumizi ya pesa za serikali yanakosaje supporting documents? zama hizi za dunia ya sasa? Na hata serikali ilipopewa muda bado wakashindwa kuleta uthibitisho wa matumizi!! Huoni kuwa hili ni doa kubwa? The fact tu kwamba kuna pesa imetumika nje ya iliyoidhinishwa na bunge na haina supporting ni hoja kubwa au we kwako hii ipo sawa kabsaaaa?
 
Inawezekana kabisa anaamini anafanya kazi nzuri ya kuinyosha nchi; ripoti ya CAG inaonesha vinginevyo. Hata hivyo, kuna hesabu watu hawajazipiga vizuri... mnafikiria majaji walioteuliwa hivi juzi ni kwa bahati mbaya tu...

1. sio kunyoosha nchi tuseme kuna visasi vibaendelea mbona ndani ya chama tu kashindwa.

2. majaji hakuna jipya uzuri wa sheria haina tofauti sana na hesabu. hao wasukuma ni junior judges wakienda kutoa hukumu za kijinga na kikabila senoirs mahaka za rufaa watasahihisha na itabaki aibu yenu wasukuma.
 
Those are serious accusations; do you have any evidence to substantiate your claims? ni rahisi sana kudai kuwa mtu ni mwizi; lakini ni vigumu sana kuonesha ushahidi wa madai hayo. Usitoe madai ili ujisikie vizuri.. aliyeiba ni nani na kaiba nini na wapi?
Ndiyo maana kuna haja ya kuwa na tume huru kuchunguza hili.
 
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Active"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'active' (isiyosubiri). Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com
Ndugu mfuasi wa uncle
Una ufahamu wowote jinsi mchakato wa ukaguzi unavyofanyika? Naona umekurupuka tu na maelezo ya kisiasa; na kumpigia debe yule jamaa wa chattle.
 
Zito Kabwe ametoa hoja sita na zote ni za nguvu, mbona hizo zingine hazijibiwi isipokuwa ya tr 1.5? CAG alipohojiwa na Azam tv alisema bunge lihoji wapi hizo trilion zilipo. Halafu mbele ya Rais anasema hamna kitu kama hicho, hiyo ni double standard ya kiwango cha lami. Ninavyojua ni kuwa serikali imefanya mbinu za kujiondoa kwenye lawama. Angalia hiyo timing. Asubuhi naibu waziri anatoa ufafanuzi na kisha baadaye CAG anakula matapishi yake mwenyewe. CAG amepewa kibano ili kuinusuru serikali. Bado nina imani hiyo pesa imepotelea hewani. TUSIDANGANYANE.
 
Mbona maelezo yametolewa? tatizo ni kuwa wanaotoa maelezo hawatoi maelezo yakaeleweka au labda watu hawaelewi imeelezwaje. Angalia majibu ya Naibu Waziri leo..

Figure za pesa zilizokwenda Zanzibar, zilizotolewa kama majibu hazijawa audited na CAG, zitaaminika vipi Kuwa ni authentic?
 
Mbona maelezo yametolewa? tatizo ni kuwa wanaotoa maelezo hawatoi maelezo yakaeleweka au labda watu hawaelewi imeelezwaje. Angalia majibu ya Naibu Waziri leo..
Mwananchi wa kawaida hawezi.kuelewa yale maelezo ya naibu waziri. Labda pale mwisho aliposema, " hii yote ni kwa sababu ya watu wasioitakia mema nchi yetu".
Sasa hapo mwananchi wa kawaida anaweza akajiuliza, hivi kweli mtu asiyetakia mema nchi yake anaweza kuhoji pesa za nchi hiyo hiyo kutokuwa na maelezo ya jinsi zilivyotumika?! Mawaziri wanahitaji semina elekezi....
 
Waliotuhumiwa kuhonga madiwani wamechukuliwa hatua gani?

Waliotajwa kwenye ripoti za makinikia mpaka leo wamechukuliwa hatua gani?

Mleta mada acha kuwa vuguvugu wa kung'ata na kupuliza.

Kama vipi utaratibu wa kuandaa na kuwasilisha hizi ripoti za CAG utazamwe upya vinginevyo haya mambo hayataisha

Wananchi wanachanganywa tu.Kesho si ajabu baadhi ya magazet yakaandika "CAG amuumbua Zitto", mengine "CAG akana trilioni 1.5 kuibiwa", n.k lakini mtu ukijiuliza ni lini na wapi CAG aliwahi tamka kuwa hizo fedha zimeibiwa hupati jibu au ni lini Zitto alitamka kuwa hizo fedha zimeibiwa pia hutopata jibu.

Kwa kifupi, hata media zetu nazo ni tatizo na hata kumuhoji CAG pia kunaweza kuongeza tatizo badala ya kulipunguza..

We are creating problems that we are not ready to face or even hearing about them!!
.....
....Salute
 
kwani hapa unashindwa kujiongeza kwenye kujumlisha na kutoa!!!

Kati ya
Shilingi
bilioni 25,307.48 zilizokusanywa,
Shilingi
bilioni
23,792.30 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi,
matumizi mengine, matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya
kulipa madeni yatokanayo na amana za Serikali pamoja na riba
Kwa hiyo unaishia hapo na kusema 1.5T haijulikani ilipo.
Sasa mimi naenda kwa kutumia cash, ambayo itakuwa rahisi kwetu sote kueleza.
Nikitumia accrual utaona naleta longolongo kwa sababu jibu litakuwa kama la Polepole na PS wa Treasury kwamba hatfungani za 0.7T ziliiva baada ya ukaguzi, 0.7T tax receivables (expected, not collected yet) na 0.2T transfer to Zanzibar. Jumla 1.6T roughly ni hela ambazo umehesabu kama collected ila siyo collected as such at that time. Hapo utatoa overdraft kupata 1.51T balance mnayolilia.
Sasa twende kwa kutumia cash, ambayo ni rahisi mno kuelewa natamani wangetumia explanation hii.
upload_2018-4-20_15-15-26.png

On cash basis, can you explain what this money means? Huku siyo kutumia hela kabla ya kuzipata? Si lazima uzilipe hizi?
Na hapo chini ni balance sheet ya BoT na inaonyesha overdraft hiyo na jinsi ilivyolipwa mwezi uliofuata. Hiyo overdraft ilikuwa 0.17T mwezi March na ikapanda mpaka hapo mwezi June. Cant you tell that money was borrowed and paid in a couple of months based on anticipated funds(accrual)?
upload_2018-4-20_15-35-15.png

Kuna hela zimepigwa, na inabidi zifuatiliwe. But not 1.5T hapo mnaleta siasa zilizodumaa.
 
Mkuu nje ya inchi???

CAG hakuwai kuuliza 1.5tril iko wapi?? Alivyo sema bunge lihoji ulipo na ilivyo tumika manaake ni nini?

PAC kama daraja kati ya serekali na CAG wamesubiri Maelezo lakini wapi.

IPSAS ni new to the government but not new to ACCOUNTING usifikiri Abas hajui alicho kiandika. IPSAS ni mlango wa kukimbia shutuma.

Wewe ndo hujaelewa achana na kukimbilia hatifungani. Pesa ilikuwepo na imetumika ila haikuingia kwenye vitabu vya mahesabu.
Usilazimishe mambo na pia acha kutumika kisiasa. Be free to think and search for information.
CAG huwa anatoa list ya votes ambazo inabidi zijieleze na sababu za ku-qualify for opinion. CAG hatoi qualification ya opinion Azam TV. He's a CPA and thats an insult to his profession and himself. Unajichora tu, ila CAG alisema wabunge waulize serikali chochote baada ya kuulizwa kuhusu 1.5T kwa sababu huwezi kumuuliza CAG fedha ambazo yeye hajauliza.
Alizouliza zipo kwenye kitabu and thats it.
 
Kwa hiyo unaishia hapo na kusema 1.5T haijulikani ilipo.
Sasa mimi naenda kwa kutumia cash, ambayo itakuwa rahisi kwetu sote kueleza.
Nikitumia accrual utaona naleta longolongo kwa sababu jibu litakuwa kama la Polepole na PS wa Treasury kwamba hatfungani za 0.7T ziliiva baada ya ukaguzi, 0.7T tax receivables (expected, not collected yet) na 0.2T transfer to Zanzibar. Jumla 1.6T roughly ni hela ambazo umehesabu kama collected ila siyo collected as such at that time. Hapo utatoa overdraft kupata 1.51T balance mnayolilia.
Sasa twende kwa kutumia cash, ambayo ni rahisi mno kuelewa natamani wangetumia explanation hii.
View attachment 751462
On cash basis, can you explain what this money means? Huku siyo kutumia hela kabla ya kuzipata? Si lazima uzilipe hizi?
Na hapo chini ni balance sheet ya BoT na inaonyesha overdraft hiyo na jinsi ilivyolipwa mwezi uliofuata. Hiyo overdraft ilikuwa 0.17T mwezi March na ikapanda mpaka hapo mwezi June. Cant you tell that money was borrowed and paid in a couple of months based on anticipated funds(accrual)?
View attachment 751492
Kuna hela zimepigwa, na inabidi zifuatiliwe. But not 1.5T hapo mnaleta siasa.
majibu ya serikali bungeni umeyaona?naona unazunguka sana
1.hela kwa niaba ya zanzibar
2.hati fungani
3.receivables
jikite hapa
 
Unampongeza wakati taratibu za matumizi ya fedha ya umma hayazingatiwi? Ni ugonjwa ule ule wa kujipendekeza.
 
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Active"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'active' (isiyosubiri). Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com
Umeharibu hapo unapoamini kwamba atafunga watu ikiwa Serikali KUU imepata HATI CHAFU Mlipaji Mkuu kamwambia mambo ni Salama na Mkuu kamuelewa!
hii kusema nivile unafeel Vibaya kusema mmetuletea Janga lkn ukweli NCHI hii mmeiletea matatizo Makubwa!
 
Ukweli ni kwamba serikali kila muda inasubiri yenyewe kuwekwa kwenye kona badala ya kufafanua vitu kwa mapana ambayo wananchi wataelewa. Ndio maana wengine wameamua kuhukumu tu kuwa zimeibiwa kinyume na hoja ya msingi ya Zitto na hata ripoti ya CAG.

Hili sakata linatoa taswira halisi ya siasa zetu lakini pia uzembe wa watendaji wa serikali kuhakikisha taarifa zao hazileti taharuki kwasababu ya ufafanuzi finyu kwenye swala zito.

Hata kama tunamchukia vipi JPM haiwezi kuingia akili kubeba Trilioni 1.5 kwa kipindi kifupi na mazingira haya ya uadui aliojijengea kwa wahujumu uchumi. Hoja ya Zitto ipo pale pale na sasa bunge lifanye kazi yake.
Acheni povu onyesheni zilipo BL 1,500
 
Kwa mtiririko wa maelezo yake, inaonekana hao majaji watakuja kutekeleza sheria kwa utashi wa mkulu. Jaribu kuangalia maelezo yake utajua ninachokuambia.

Nasaha zinazotolewa na viongozi zinaakisi matarajio ya upande wa utendaji. Kutaka majaji washughulikie kesi haraka ni matarajio ya Watanzania wengi. Mzigo wa kesi ni mkubwa sana na mabadiliko mengi yanahitajika sasa kuna ubaya gani kwa Rais kusema matarajio yake?
 
Nafikiri Zito mwenyewe anajua hizo fedha zimetumika vipi, ila anataka kuijuza serikali kuwa haiwezi kujiamulia mambo bila taratibu...

Ndio maana anaibana kwenye kona, serikali badala ya kufafanua inazidi kujichanganya.

Tatizo ni kuwaona watanzania hawana uelewa, ama mtu mmoja kujiona mzalendo kuliko wote mil 55
Kama CAG hajui ZITTO atajuaje au unahakika anafanyakazi kama Afisa wa Serikali?
 
Mkuu mwanakijiji umejaribu kumtetea zitto na kuwalaumu wanaserikali lakini hutaki kutambua kuwa wapo wapinzani wa magufuli ambao kazi yao ni kumvuruga tu kwa maslahi yao binafsi....Serikali ikisema chochote lazima waspin ili wapate popularity na ujira wao.

Of course Zitto ana lengo lake na labda si kuhoji tu; hii ni mara ya pili wakati wa ripoti ya CAG anakuja na hoja kali za kusumbua. Siwezi kumlaumu na hata akihoji kwa ukali ni haki yake. Tatizo ni kwa nini anapata nafasi hiyo? Na wapinzani kuspin ndio siasa yenyewe, hili binafsi halinisumbui. Ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa haitoi nafasi kwa wapinzani kuspin. Hili la trilioni 1.5 ni mfano halisi wa jinsi gani serikali haipaswi kushughulikia tetesi na hoja zisizo hoja..
 
Back
Top Bottom