Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

kwakweli bongo bado sana yaani 1.5T hazijulikani zilipo alafu wabunge wanapiga makofi na kushangilia ???.hasira kabisa
 
Hii Miafrika bana Majirani zetu nao ..... Mozambique government has not done enough to explain how $2 billion in loans was spent and roughly a quarter of the money remains unaccounted for, an independent audit of the debt showed on Saturday
 
Mimi nasubiri kuona watu wanahojiwa kuhusu upotevu wa takribani Sh Billion 40 kama kodi

Ripoti inaonesha mafuta yenye msamaha wa kodi wa takribani Sh. 12 Billion hayakutumika kwa wanufaika wa msamaha!

That said, kuna uwezekano mkubwa mafuta husika yameingizwa kwenye mzunguko pasipo kulipa kodi!!

Si hivyo tu, transit goods ambazo kodi yake ni takribani 27 Billion; hakuna ushahidi kwamba zilivuka border na kwa maana hiyo kuna uwezekano mkubwa bidhaa husika zimetumika Tanzania bila kulipa kodi!
Unaona sasa.. watu wanazungumzia trilioni 1.5... mimi nafikiri hii haikuja kwa bahati mbaya..
 
Kamati ya PAC na LAAC bado hazijaanza kujadili hoja au taarifa ya CAG, hivi Waziri/Serikali walikuwa wanamjibu nani?CAG,BUNGE au Wananchi ? na Walifanya hayo kwa mujibu wa sheria ya Ukaguzi au sheria ya kubalance habari mtaani?
Kuna maajabu lakini sio haya, ina maana Malaika Mkuu hajui kuwa kuna uchafu mwingi kwa serikali Kuu kuliko kwa Halmashauri zote Nchini?
Mafuta ya bilioni 12, manunuzi,kushindwa kukusanya kodi triliioni 4,
haya mbona hayajibiwi?

The road to hell is paved with good wishes
 
Hii ndio hoja muhimu sana. Nashangazwa na watu kukasirika kwamba wananchi wana hoji. Sasa wananchi wangefanyaje kama hakuna mtu anawapa taarifa kwa uhakika? Prof. Assad alitakiwa kusimama mara moja kabla ya kupigiwa simu na Rais kuulizwa... kwanini hakutoa maelezo kumsahihisha Zitto na badala yake kazi hiyo inafanya na Polepole? ambaye anawahi kutoa maelezo yanayofanana na yanayotolewa na Naibu Waziri leo?
Mbona yeye CAG mwenyewe hakupewa maelezo mkuu ina maana hili hakulihoji kabla ya ripoti kwenda hewani?
 
Hakuna haja ya kuwa na mitandao km inatumiwa kupotosha, kutukana na kudhalilisha watu..nchi haiwezi kuwa jalala na taifa la wahalifu, ufinyu wa akili wa watz wengi ndiyo tatizo kubwa elimu yetu haifuti ujinga tena..hata Phd holders ni wajinga, nchi hii ilikuwepo, ipo na itakuwepo kwa anayejua nadharia za maendeleo hafikirii kufa kwake ndiyo mwisho wa Tanzania, unapokuwa kiongozi una wajibu waa kulinda maslahi hata ya kizazi cha tano mbele! tunajenga taifa gani la kudhihakiana, wadogo kutukana wakubwa, lugha za matusi mitandaoni ndio ushujaa...ukiachia hali hiyo taifa halina future!! inashangaza wakati huu ambao serikali inadhibiti uhalifu na aina zote za uovu watu hawatambui, lakini hitilafu ndogo ya kitakwimu ndiyo imekuwa ajenda..siku za nyuma ambapo uovu ulitamalaki, mishahara hewa, safari hewa, Escrow..nk kelele hizi hazikusikika..nini maana yake, kelele nyingi mitandaoni ni za waathirika wa maamuzi na uendeshaji wa serikali awamu ya tano, wengi ni wahanga wa uhalifu uliozoeleka zama zilizopita ambao sasa umekomeshwa!
Yaani 1.5 trillion wewe unaona ni kijitakwimu kidogo? Kwa taarifa yako swala la mitandao halizuiliki siyo kwa miaka hii ya technolojia ya sasa! Hii siyo 70's huu ni mwaka 2018 the modern world. Serikali iwajibike kwa wananchi kujibu hoja na tuhuma siyo kuwafunga midomo. Hizi kukurukakara za kutumia vyombo vya dola na kuwakamata watu ovyo na kuwafungulia kesi zisizo na tija hazitowasaidia. Sana sana zinajenga chuki kwa wananchi tu.
 
Kwanini kuwe na machafuko? wananchi nao ni lazima wawe na akili ya kutafakari vitu.. sasa mtu kasema Trilioni 1.5 haijulikani ilipo, watu wanaanza kusema imeibwa, imeliwa, amechukua kaweka Chato.. n.k sasa haya yote yanatoka wapi?
ripoti ikishaandikwa serikali inapewa siku 21 kujibu mapungufu. mbona hawakujib, manake walishindwa. ww unatetea nn, kwnn watu wasiamini ziliibwa!
 
nimejifunza kitu kimoja.
katika zama hizi za mitandao au dunia kuwa familia taarifa zinasafiri haraka.
kujibu kwa wakati au kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo yanayoleta utata kutaleta tija ktika pande zote watawala na watawaliwa.
mitandao imewaweka wananchi karibu na taarifa leo kuliko miaka yote.
Wewe ndio unaona hilo na ndio ukweli kwa mwananchi wa kawaida unae enda na wakati .swali, je hawa viongozi wa serikali wanao ona Vinginevyo kabisa tuwaeleweje wa shamba au wako nyuma ya wakati !?
 
Wewe ndio unaona hilo na ndio ukweli kwa mwananchi wa kawaida unae enda na wakati .swali, je hawa viongozi wa serikali wanao ona Vinginevyo kabisa tuwaeleweje wa shamba au wako nyuma ya wakati !?
ukiwauliza wao watakupa jibu bora kabisaa kuliko mimi mkuu.
 
Ata endelea hivi mpka lini miaka 7 mbele kwa staili hii huoni anatumbukiza inchi kwenye machafuko?
Sio anatumbukiza. Tayari tumesha vurugwa mpaka hatuna hamu nae .yaani sasa hivi dua tumegeuzia siku ziende salama na haraka tushuke kwenye hili Lorry
 
Kwanza alianza Bwana Polepole na kejeli zake, akasema wachochezi, wakamatwe wahojiwe.....

Akaja yule aliyehamia juzi CCM, Bw. David Kafulila akaandaliwa kipindi maalumu ITV akasema hizo RECEIVABLE na PAYABLE tu.....

Funga kazi ikawa ni utetezi wa serikali yenyewe nje kabisa ya mfumo rasmi tena ktk matukio yaliyotokea kwa mfuatano moja likimuhusisha Rais Magufuli mwenyewe na jingine Bungeni....

Bungeni, NW wa Wizara ya Fedha, akatoa utetezi wa "wapi zilipo 1.5T" kwa kutoa Takwimu sawasawa na za Polepole kwamba RECEIVABLE na PAYABLE na zingine ni za Zanzibar hatujawapatia na blah blah zingine.

Mwisho kabisa, mama wa watu huyu NW, ktk kuhitimisha hoja yake kwa niaba ya Magufuli "anatema" nyongo ya mkwara mzito kwa, wanaohoji ilipo 1.5T kuwa ni wachochezi na wasiotakia nchi hii mema, "wanatumwa" hivyo wapuuzwe na wadharauliwe mbali kule....!!!

Kwa upande mwingine siku ileile NW akitoa maelezo ya serikali Bungeni, kule Rais John Pombe Magufuli akiongea na Majaji aliowateua, naye anatumia fursa hiyo purposely kutema nyongo na mkwara mzito juu ya hii ishu.....

Cha kusikitisha na katika hali isiyo kuwa ya kawaida kabisa na nadhani kwa makusudi maalumu, anawasimamisha CAG na PayMaster wa Hazina in public kuwauliza kama kuna 1.5T katika ripoti ya Controller Auditor General (CAG) imeibwa....

Nao maskini wa Mungu hawa wanajibu bila hiyana "Mheshimiwa Rais hakuna kitu kama hicho, hakuna wizi wowote...!! "

Sijui Bwana Magufuli alitegemea apate jibu gani tofauti na hili kwa wateule wake hawa katika mazingira yale dhariri..

Hata ungekuwa wewe MMM na kwa kutambua kuwa uongozi wa Rais Magufuli wa mkono wa chuma ungetoa jibu tofauti na alilolitarajia kulisikia???

Humwogopi Iddi Amin Dada mla nyama za watu wewe???

Au Je, ungekuwa jasiri kama Nabii Daniel mbele ya Mfalme Nebukadineza na kusema:

".......Hapana Mheshimiwa Rais, hatujathibitisha kama ni wizi kweli ama vinginevyo, isipokuwa tumeona kuwa pesa imekusanya, ikapokelewa na kuingizwa ktk vitabu vya mapato ya serikali lakini ktk ukaguzi wetu hatujaona imetumika kufanya nini kwa sbb hatujapata nyaraka za matumizi yake pamoja na kuwapa muda wa kutosha maafisa masuhuri wanaohusika kutuletea nyaraka za uthibitisho. Hivyo Mh. Rais hatukuwa na jinsi ikabidi tufunge ripoti yetu ya ukaguzi kwa kuandika tulichokiona na kukithibitisha........!! "

Aisee Mzee MwanaKijiji, leo hii usingekuwa unaonekana....ungepotezwa siku hiyo hiyo na pengine kuokotwa ktk viroba vya sandarusi kandokando ya ufukwe wa Bahari ya Hindi ama Mto Ruvu ukiwa tayari chakula cha Mamba...!!

Acha kabisa. We know what is going on. Tusidanganyane hapa ndugu yangu....
 
Kimsingi umeandika upuuzi, bado ni mtu sahihi pamoja na kuwa 1.5 haijulikani imeenda wapi?
 
Chanzo cha matumizi ya fedha za serikali yasiyo fuata bajeti ni viongozi wakuu wa serikali wenyewe. Hili suala la hoja za CAG zitaisha mpaka pale viongozi wetu watakapotambua kwamba maagizo yao yoyote wanayo yatoa yanakiasi fulani cha gharama zinazoingia ili yatekelezwe. Maagizo yanapotolewa nje ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge ndo mwanzo wa madudu anayoyaibua CAG kwenye taasisi za serikali.
 
Back
Top Bottom