Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Ukweli ni kwamba serikali kila muda inasubiri yenyewe kuwekwa kwenye kona badala ya kufafanua vitu kwa mapana ambayo wananchi wataelewa. Ndio maana wengine wameamua kuhukumu tu kuwa zimeibiwa kinyume na hoja ya msingi ya Zitto na hata ripoti ya CAG.

Hili sakata linatoa taswira halisi ya siasa zetu lakini pia uzembe wa watendaji wa serikali kuhakikisha taarifa zao hazileti taharuki kwasababu ya ufafanuzi finyu kwenye swala zito.

Hata kama tunamchukia vipi JPM haiwezi kuingia akili kubeba Trilioni 1.5 kwa kipindi kifupi na mazingira haya ya uadui aliojijengea kwa wahujumu uchumi. Hoja ya Zitto ipo pale pale na sasa bunge lifanye kazi yake.
 
Tanzania kila anachofanya mtu ni sahihi kulingana na upande alipo.

Kama yupo ccm au shabiki wa jiwe hata ukimwekea kisu shingoni atakwambia hela haijaliwa/ibiwa ....

Tabia hii ya kuacha kuambiana ukweli kutokana na ushabiki ITATUFANYA KUFA bila kuona Tanzania iliyoshamiri kiuchumi, elimu, kiafya ilihali tuna rasilimali almost zote

Mzee Mwanakijiji naheshimu sana mawazo yako na nilikuwa msomaji mzuri wa makala zako ila huu ni undezi wa kiwango cha juu.
 
Those are serious accusations; do you have any evidence to substantiate your claims? ni rahisi sana kudai kuwa mtu ni mwizi; lakini ni vigumu sana kuonesha ushahidi wa madai hayo. Usitoe madai ili ujisikie vizuri.. aliyeiba ni nani na kaiba nini na wapi?
Sasa Magufuli katoa ushahidi gani kwamba Pesa hiyo haijaibwa.

Unasema ushahidi wkt Rais mwenyewe hajathibitisha 1.5 zipo wapi..

Acheni kupotosha. Unataka tumwamini Rais Magufuli na wkt ripoti ya CAG ipo..
 
Kwangu mimi Magufuli si mtu sahihi..uongozi haumpendi ila yeye anaupenda uongozi.
Kama watanzania huwa wanasikia kuwa kuna maisha magumu mpaka mtu anakufa bila sababu basi ndo kipindi hiki..ni mwanzo tu
 
Hapo ndio penye tatizo.. unaweza kufikiria uko moto lakini kumbe unajiunguza mwenyewe... jifunze kuangalia vitu with a balance.. siyo ili uonekane uko upande fulani uwaridhishe watu fulani.. usiogope kuwaudhi watu kwa msimamo wako.
Ndio maana hawatokuja kukuelewa! Wamezoea wachambuzi wetu wanafiki ambao sometimes wanaisema serikali au wapinzani ili tu kuridhisha watu flani! Binafsi naheshimu mtu asiyeogopa kutoa maoni yake bila kujali nani atapenda au kuchukia!
 
Kwa hio umeridhika na maelezo ya Pole Pole kuhusiana na balance ya 1.5 Trillions?

And what make you think CAG is incompetent by adding the revenue ie Receivables and Zanzibar revenue unknowingly to the accounts?

Do you understand the methods and process of auditing?

Do you understand how the accounts are prepared? If CAG prepared the Accounts in cash basis, and Mr. Pole Pole addressing us it should have been in accrual, therefore you think CAG is incompetent, not understand the hell he is doing ?

And if that the case the whole report must be considered void and invalid, therefore going back to rectify substantial revenue and expenditure items that aren’t allotted in the first Audit?

Do you understand the implication on the audit report from what has been said by Pole Pole and Waziri regarding the issue of Accounts preparation?
 
Boss Mzee Mwanakijiji Umeandika vizuri bila kuegemea upande wowote. Mimi binafsi nilitegemea Rais au Wasaidizi wake, waelezee 1.5T zimetumikaje, Hata wangekuja na matumizi ya uongo au kweli, Mfano, wangesema Jomoni, 1.5T tumetumia kufufua ATC (Shirika la Ndege), au Jomoni 1.5T zimetumika kulipa deni letu la ndege iliyoshikiliwa Canada. WaTanzania tungeelewa. Hili la kulaumu Mitandao ni Hoja Mfu. Au Jomoni 1.5T tumetumia kununua Wapinzani (Jokes aka Natania).

Mimi nilishaishauri Jamhuri na Serikali na Chama, zikiibuliwa Hoja, Dawa yake ni kutoka haraka na kujibu Hoja, na wakijibu wajibu ki Hoja waache kutoa lawama au kuita watu wachochezi.

Siku zote Uongo unaaminika haraka, na ukweli unachelewa, ni muda tu. Uongo unapanda lift wakati ukweli unapanda ngazi.

Hivi kile kigugumizi cha Rais ni kuwa alikuwa na Hasira au Nafsi na Dhamira ilimsuta????

Hakuna mahala CAG alisema 1.5T zimeibiwa, alichosema ni 1.5T hazionyeshi matumizi yake, na akataka Bunge lihoji, 1.5T zipo wapi.

UOTE="Mzee Mwanakijiji, post: 26774324, member: 118"]
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Active"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'active' (isiyosubiri). Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com[/QUOTE]
 
Nafikiri Zito mwenyewe anajua hizo fedha zimetumika vipi, ila anataka kuijuza serikali kuwa haiwezi kujiamulia mambo bila taratibu...

Ndio maana anaibana kwenye kona, serikali badala ya kufafanua inazidi kujichanganya.

Tatizo ni kuwaona watanzania hawana uelewa, ama mtu mmoja kujiona mzalendo kuliko wote mil 55
 
Sasa Mzee Mwanakijiji unamtoaje Magufuli kwenye hii lawama kama yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kwenye kutekeleza questionable costly projects kama ule mradi wa Chato International Aiport. Pesa iliyojenga Chato International airport ilitoka kwenye bajeti gani. Na kama hii airport haina maslahi kwa umma, unawezaje kubisha kwamba huo siyo ufisadi. Ufisadi siyo tu kukwapua pesa kama kibaka mtaani. Willful misallocation of public resources ni ufisadi pia.
 
Waliotuhumiwa kuhonga madiwani wamechukuliwa hatua gani?

Waliotajwa kwenye ripoti za makinikia mpaka leo wamechukuliwa hatua gani?

Mleta mada acha kuwa vuguvugu wa kung'ata na kupuliza.

Kama vipi utaratibu wa kuandaa na kuwasilisha hizi ripoti za CAG utazamwe upya vinginevyo haya mambo hayataisha

Wananchi wanachanganywa tu.Kesho si ajabu baadhi ya magazet yakaandika "CAG amuumbua Zitto", mengine "CAG akana trilioni 1.5 kuibiwa", n.k lakini mtu ukijiuliza ni lini na wapi CAG aliwahi tamka kuwa hizo fedha zimeibiwa hupati jibu au ni lini Zitto alitamka kuwa hizo fedha zimeibiwa pia hutopata jibu.

Kwa kifupi, hata media zetu nazo ni tatizo na hata kumuhoji CAG pia kumeongeza tatizo.
Ushauri - Watumie TV STATIONS ZOTE KWA MASAAA YOTE YA WIKI NZIMA KUKANUSHA HILI , na wawatumie wanachama wao mahiri akiwemo huyu mleta mada , Bali wafahamu kwamba ripoti ya CAG Haiwezi kufutwa na bunduki ama watu wasiojulikana .
 
Hivi wakurugenzi waliofukuzwa kazi kwa kupewa hati chafu wamekutwa wamekula pesa? ..sawaa pesa hazijaibiwa na yeyote lakin kutumia fedha kinyume na financial bill ya mwaka husika ni kosa pia ni sawa na mkurugenz wa halmashauri upewe pesa ya kujenga zahanati yeye akajilipa perdiem ya safari zake, wanaishia kusema hazijaibiwa ila hawasemi wametumia kufanya nin na wanashindwa kutoka viambata vya matumizi
 
Nafikiri Zito mwenyewe anajua hizo fedha zimetumika vipi, ila anataka kuijuza serikali kuwa haiwezi kujiamulia mambo bila taratibu...

Ndio maana anaibana kwenye kona, serikali badala ya kufafanua inazidi kujichanganya.

Tatizo ni kuwaona watanzania hawana uelewa, ama mtu mmoja kujiona mzalendo kuliko wote mil 55
Very correct
 
Sasa hiyo hoja si wajibu..mbona kujibu hoja ya wakaguzi ni simple tuu ukiwa na nyaraka..kama hawana nyaraka basi wasitulaumu tukihoji, haiwezekani utumie 1.5T then hutuelezi umetumiaje
 
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Active"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'active' (isiyosubiri). Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com
Na kwa kuwa Magufuli ni MTU sahihi kwako hata hoja zako zimelenga kuonyesha kuwa ni MTU sahihi .
Uko biased sana
Kwa sasa kwako Kukosoa Rais hata angefanya uovu wa aina gani ni sawa na Kujikojolea ukweni hivyo umeamua vema kwamba hutajali nini utabaki na imani yako hata kama haina mashiko kuwa Magu ndiye MTU sahihi pasipo uwezo wowote kihoja wala kimantiki kuthibitisha ushihi wake kadri ya Muda na mambo na hata alipoliweka taifa letu,kisiasa, Kiuchumi na Kijamii
 
1.5 trillion imepigwa na huyu mliyekuwa mnamuita mzalendo na mpinga ufisadi.

Jiwe badala ya kutuma vyombo vichunguze pesa imeenda wapi yeye anachukia na kuwatisha wanaohoji wizi wa 1.5 trillion kwanini tusimuhisi kuwa ni yeye mwenyewe ameziiba???
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji labda kabla hatujaanza kumpenda,kumchukia,ama kumwogopa mheshimiwa rais hebu kwanza tujaribu kumweka kwenye mizani ili tumjue vyema! Inawezekana kuna mambo hayajui vyema ila hapendi/hataki kujidhihirisha kuwa hajui,na kuna wanaojua,na ambao wanajua kuwa Mheshimiwa hajui,na wanatumia kutokujua kwake "kumsokota"!! Na kwakuwa hapendi tujue kuwa amesokotwa kwa kuto kujua kwake basi anaamua ku grind the whole bump!! Na kusema hakukuwahi kuwa na tatizo!!lakini pia inawezekana kinachomsukuma kufanya chochote
anachofanya ni egoism! Labda ni partisanship! Lakini pia yawezekana ni nia yake njema ndiyo inayomsukuma kuwatisha wanaowatisha wananchi watiifu kwa kuwaeleza ukweli unaotisha!! Na. Labda kama atakuwa amebadilika siku hizi,maana angeweza tu kuwaambia wananchi wamdharau anayesema eti trilioni 1.5 hazionekani! Angewaambia tu waendelee "kuchapa kazi"kwani hizo story za matrilioni haiwezi kuwaletea ugali mezani!! Magu ana sura nyingi sana!! Tunashindwa kuelewa kama huyu wa leo ndiyo yule wa jana!! Tumjue kwanza!
 
Kwanini kuwe na machafuko? wananchi nao ni lazima wawe na akili ya kutafakari vitu.. sasa mtu kasema Trilioni 1.5 haijulikani ilipo, watu wanaanza kusema imeibwa, imeliwa, amechukua kaweka Chato.. n.k sasa haya yote yanatoka wapi?
Kuna wakati unaandika viroja hadi huruma
Kama haijaibiwa au kuliwa au kuwekwa kwenye akaunti ya siri ya kampeni 2020 Kwa nini Jedwali LA matumizi yake CAG alikose hadi atake bunge lihoji ?
 
Mbona maelezo yametolewa? tatizo ni kuwa wanaotoa maelezo hawatoi maelezo yakaeleweka au labda watu hawaelewi imeelezwaje. Angalia majibu ya Naibu Waziri leo..
Majibu ya Naibu Waziri yanaongeza utata kuliko kupunguza
Tuache kujitia upofu kwenye hili jambo
Ni rahisi sana kutumia hesabu za CAG za mwaka uliopita kugundua window dressing ya Naibu Waziri
 
Back
Top Bottom