Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Mkuu Mzee Mwanakijiji

Itumike lugha rahisi tu, 1.5 zipo wapi au kwanini hesabu hazionekani kukokotolewa kwa usahihi. Hilo tu

Totallyl agree.. ndio lengo la hoja yangu vile vile... maana kama Zitto hakuelewa kilichoripotiwa tena kwa lugha ya Kiswahili sitoshangaa wanaosema "zimeliwa" kwani ni hitimisho rahisi kulifikia kuliko hitimisho la "haijaeleweka".
 
Mahaba ni hatari, ule uwezo na umakini was mwanakijiji sijui umeenda wapi!....kama vile anamatarajio Fulani Siku hizi!....time will tell..
Sina hakika kama anamatarajio yoyote zaidi yakuitukuza KANDA PANDWA
 
Tatizo siyo lugha nyepesi, wala si kuchelea kujibu. Tatizo ni kushikilia hoja kisiasa kwa manufaa ya kisiasa. Kujiondoa uelewa makusudi, ili unufaike kisiasa. Hilo ndiyo tatizo na lipo wazi.

Element ya siasa hapa haiwezi kuondolewa; na hatari yake ni kuwa wananchi wa kawaida wanaweza wasitofautishe siasa ndani ya hoja hii. Maana inaweza kuwa na lengo la kumfanya Magufuli kashindwa na hivyo hafai...
 
Haya sasa ndio naita magoli; hivi siku hizi zote hujasikia watu wanadai Magufuli kaiba, tena mwizi? Hujasoma watu wanaandika humu humu kuwa hizi trilioni 1.5 zimeliwa? Unafikiri kwanini Magu amemuliza CAG kwanini hakuripoti wizi wa trilioni 1.5? na mara moja CAG akasema "hakuna kitu kama hicho"? Kama fedha hazikuibwa ina maana hakuna uhalifu siyo; kuna hoja nyingine zinahitaji kujengwa kwa mfano 'hazikutolewa maelezo ya kutosha"..
Hata kama hazijaliwa ziko wapi?
 
Kuna hela zimepigwa, na inabidi zifuatiliwe. But not 1.5T hapo mnaleta siasa zilizodumaa.

Na hii ndio hoja halisi na hofu yangu ni kuwa tumeshindwa hata kujaribu kuzungumzia tulipolizwa kweli kweli..
 
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Proactive"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' inayosubiri kutenda baada ya tukio (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'pro active' (isiyosubiri) yaani inayowahi kutenda kabla ya tukio. Ukiona moshi una uamuzi wa kuwahi kuzima kabla miale haijaanza kuweka (proactive) au unaweeza kusubiri vianze kuungua uanze kujitahidi kuzima moto (reactive).

Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com

Nchi ya ajabu hii sijapata kuona. Central government imepata hati chafu (qualified opinion) mtuhumiwa namba moja ni PS wa Finance ambaye alipaswa kuwa amechukuliwa hatua ASAP kama wale wakurugenzi watatu lakini huyu anapigiwa simu tu eti anaulizwa kuna pesa yeyote imeibiwa anajibu hapana uncle hakuna kitu kama hicho halafu basi mambo yameisha- ARE WE REALLY SERIOUS? NI KWELI TUNAWAPENDA WATANZANIA KAMA VILE TUNAVYOHUBIRI MAJUKWAANI KWAMBA SERIKALI HII NI YA KIZAELNDO?
 
jamani mnapata tabu bure kudhani watanzania wa zama hizi ni mazwazwa,unadai eti naibu waziri wa fedha ametoa ufafanuzi ufafanuzi gani ule wa kindezi?Mwl Nyerere aliwahi kusema sikumbuki neno kwa neno,alisema"mtu ukiwa na akili timamu akatokea mtu akakushauri jambo la kijinga nawewe ukakubaliana na jambo hilo ATAKUDHARAU",sasa mimi nimekataa kumeza ufafanuzi unaoendelea kutolewa na serikali maana ilituaminisha hii ni serikali makini na inayopambana na ufisadi na moja ya njia za kupambana na ufisadi ni kufuata sheria na taratibu tulizojiwekea sasa ripoti inasema kuna wakandarasi wamelipwa pesa bila kuwa na mikataba linawezekanaje awamu hii kosa kama hilo?eti leo naibu waziri wa fedha anatoa ufafanuzi!Huo ufafanuzi walipaswa wampe CAG ili abadilishe ripoti yake aje na ripoti itakayo accomodate hizo takwimu za kupika ili kusiwe na sintofahamu ya ripoti hiyo.

kweli mnataka kutuaminisha serikali makini na inayopinga ufisadi CAG wake anaweza ku over look takwimu zilizotolewa na naibu waziri wa fedha?Vinginevyo CAG atoke aseme ripoti yake inamakosa aisahihishe na aingize hizo takwimu ambazo hakuziingiza kwenye ripoti,na akifanya hivyo tutamuomba ajiuzuru atakuwa hatufai.

mimi naamini 1.5T ni kweli ipo na haina maelezo ya jinsi ilivyotumika,kwamfano tuchukulie jambo la ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa CANADA hatukupewa taarifa mwanzo kama ilikamatwa na kwamba tulikuwa tunadaiwa,

Ndege imerudi hatujaambiwa taarifa yoyote kwamba tumeshinda kesi na hatujalipa hata senti tano maana mara ya mwisho nilimsikia RAIS akisema amemtuma mwanasheria mkuu wa serikali kwenda huko kupambana kisheria VIPI mbona matokeo ya huo mpambano hatuambiwi?

Na kama tumeshinda kesi hakuna kesi nyingine tuliyofungua kudai gharama za kesi na fidia kwa mdai kutucheleweshea ndege yetu kufanya biashara kitu ambacho kimetukosesha mapato?

Na kama tumeshindwa tumewalipa kiasi gani?
kumbuka kesi ilikuwa ni ya madai.serikali inasubiri mpaka lini ije kutuambia kwamba imemlipa mdai wetu aliyekuwa ameshikilia ndege yetu canada?na kama tumelipa tumetumia bajeti ipi na ilipitishwa lini na BUNGE?sasa kwa mambo kama haya utaacha kuamini kuna fedha za serikali zinatumika bila maelezo?
 
Mkuu mwanakijiji umejaribu kumtetea zitto na kuwalaumu wanaserikali lakini hutaki kutambua kuwa wapo wapinzani wa magufuli ambao kazi yao ni kumvuruga tu kwa maslahi yao binafsi....Serikali ikisema chochote lazima waspin ili wapate popularity na ujira wao.

Naona ungefanya vyema kwa kuwakumbusha wapinzani wa Magufuli kihoji matatizo ya kweli yanayofanywa na Serikali.

Leo hii wapinzani wakihoji kwa nguvu zote juu ya upungufu wa bajeti ya afya ...hilo litakuwa ni tatizo la kweli na lenye manufaa kwao na kwa jamii.
Hawatakiwi kuspin ukweli ili uonekana kama uongo...wanatakiwa wahoji kwa manufas ya wananchi na nchi.

Geremy Corbyn amemuhoji Theresa May kuhusu kuishambuli Syria kwa ustadi mkubwa sana wapinzani wajifunze kuhoji kwa style hii.
Msaidie Pole pole kujibu zilipo Bil 1,500
 
Ni hatari sana, mambo serious kama haya yanaletewa mchezo kiasi cha kuleta mkanganyiko.

Inawezekanaje ofisi nyeti kama ya CAG ikaleta taarifa Kwenye chombo kama Bunge halafu kukawa na mkanganyiko kwenye hesabu kiasi cha kuchanganya jamii na bado kirahisi rahisi tena majibu yanayoonyesha CAG kutokuwa makini au kutokujua masuala muhimu ambayo hata mwenezi wa chama anayajua yanatolewa na inaonekana ni sawa wakati kwenye ripoti husika hayo maelezo hayapo..

Kwa fikra zangu na kuelewa kwangu maelezo ya Naibu waziri na mwenezi wa chama fulani naona kabisa wanatuambia CAG hafai na kazi yake haifanyi sawasawa kiasi cha kushindwa kuelewa ABC ya hizo 1.5...
Kwa maelezo haya inaonyesha ni kweli mmekwiba hizi Hela!
 
ni rahisi sana kudai kuwa mtu ni mwizi; lakini ni vigumu sana kuonesha ushahidi wa madai hayo. Usitoe madai ili ujisikie vizuri.. aliyeiba ni nani na kaiba nini na wapi?
Ushahidi gani unataka wakati trillioni 1.5 zimeliwa?

Infact yeye mwenyewe huwaambia polisi wanachunguza kitu gani au mahakama zinatafuta ushahidi gani wakati wizi uko wazi!!! Sasa yanapomfika yeye mnataka ushahidi!
 
Ya kuchunguza nini sasa? hapa hakuna cha kuchunguza unless mnataka kuwatafutia watu upigaji wa ukweli sasa

Ina maana Mwanakijiji huoni logic ya uchunguzi kwenye hili? Hiyo 1.5 Trillion ni 6% ya pesa yote iliyokusanywa toka kwenye vyanzo vyote, hiki si kiasi kidogo cha pesa, kina material effect. CAG anasema pesa yote hiyo haijawa properly accounted for. Haionekani imetuma kwenye nini (kuna watu kwa makusudi au kwa kutokujua wanaichanganya hii na ile pesa iliyotumika bila kuwa na budget).

Kitaalaamu wale wanaosema IMELIWA na wanaosema HAIJALIWA (CAG ni mmojawapo-mwalimu wangu kaniangusha sana kwenye hili ikulu leo-hakupaswa kwenda ingebidi hata aumwe basi) wote wanakosea-kwa sasa hakuna uthibitisho kwenye either of the two. Kitaalamu kunapokuwa na hali kama hii kunafanywa INVESTIGATION au FORENSIC AUDIT (ambao ndio uchunguzi wenyewe huu) ili kuweza kutoa majibu halisi TUMEPIGWA AU VINGINEVYO maana hawa watu walipewa siku 21 kutoa majibu hii pesa imetumika kwenye nn hawakuweza kujibu so hatupaswi kuwapa muda zaidi. Sasa uchunguzi unapaswa kufanywa kufanywa na Bunge likishirikisha wataalamu husika. Hii ndio essence ya uchunguzi baba ni utaratibu wa kawaida kabisa. HATUPASWI ASILANI KUFUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE KWENYE HILI KWANI HII PESA NI NYINGI SANA.
 
Ninaona unajaribu kumtetea Magufuli kwa akili sana.


Kitendo tu cha kuitoa Tanzania kwenye mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi kinatakiwa kitoshe kukuonesha kuwa raisi aidha hana nia njema na nchi au anatuchukulia kama makondoo. Tujue, tusijue..hatuna shida.

La hasha, MM, Magufuli ameshindwa. Hata nikitaka kuanza na assumption kuwa ana nia njema...basi kwa maneno yake amekiri kuwa kuiongoza nchi ni zaidi ya alichotarajia. More than he bargained for.

Ila kwa sasa hata hiyo benefit simpi...Magufuli ana nia ovu tangu awali. Tukiendelea kusema tutaonekana wabaya tusioipenda nchi yetu..

Kwa hilo ninasema, only time will tell.
 
Ukweli ni kwamba serikali kila muda inasubiri yenyewe kuwekwa kwenye kona badala ya kufafanua vitu kwa mapana ambayo wananchi wataelewa. Ndio maana wengine wameamua kuhukumu tu kuwa zimeibiwa kinyume na hoja ya msingi ya Zitto na hata ripoti ya CAG.

Hili sakata linatoa taswira halisi ya siasa zetu lakini pia uzembe wa watendaji wa serikali kuhakikisha taarifa zao hazileti taharuki kwasababu ya ufafanuzi finyu kwenye swala zito.

Hata kama tunamchukia vipi JPM haiwezi kuingia akili kubeba Trilioni 1.5 kwa kipindi kifupi na mazingira haya ya uadui aliojijengea kwa wahujumu uchumi. Hoja ya Zitto ipo pale pale na sasa bunge lifanye kazi yake.
Unafikiri anaweza kushindwa kuchukua hizo pesa kwa sababu hiyo uliyoitoa? Kwani hizo anazozitumia nje ya bajeti anakuwa hajajijengea uadui na wahujumu uchumi?
 
Katika maisha yangu sijawahi kusikia ripoti ya ukaguzi ya mahesabu ikawa 100% sahihi na hii ni Dunia nzima, isitoshe huyu Mkaguzi yeye nani anamkagua? Kwa maana inavyoonekana kila mtu anaona mwingine ana makosa na huyu Mkaguzi yeye ni Malaika, siamini hilo kila kitu kuna margin of errors, hasa unadili na statistics, ...

Zito Kabwe hana usmart wowote sema tu nchi yetu wengi wetu ni less intelligent people ndo maana kitu ambacho kiko wazi kama hiki mtu anaonekana na genius, kumbe ni average tu!
Hata hakimu anapohukumu mtuumiwa usidhan katka kesi zote alizowahi kihukumu kuwa yeye hajawahi tenda kosa hilo, na hawez kupindisha sheria et kwa vile hakuna binadamu malaika.
 
Nasaha zinazotolewa na viongozi zinaakisi matarajio ya upande wa utendaji. Kutaka majaji washughulikie kesi haraka ni matarajio ya Watanzania wengi. Mzigo wa kesi ni mkubwa sana na mabadiliko mengi yanahitajika sasa kuna ubaya gani kwa Rais kusema matarajio yake?

Kuna tofauti ya matarajio na utashi wake. Labda kama hukuelewa nilichosema.
 
Usilazimishe mambo na pia acha kutumika kisiasa. Be free to think and search for information.
CAG huwa anatoa list ya votes ambazo inabidi zijieleze na sababu za ku-qualify for opinion. CAG hatoi qualification ya opinion Azam TV. He's a CPA and thats an insult to his profession and himself. Unajichora tu, ila CAG alisema wabunge waulize serikali chochote baada ya kuulizwa kuhusu 1.5T kwa sababu huwezi kumuuliza CAG fedha ambazo yeye hajauliza.
Alizouliza zipo kwenye kitabu and thats it.



Acha kutumia lugha ya kitapeli 2×3=6
3×2=6

Tubishane kwa hoja mambo ya kutumika hiyoo defence mechanism yakushindwa.

Tatizo lako nimeshalijua Mara ya kwanza ulivyoniquote nilijua tunaweza kulichambua hili swala lakini.

Nimegundua ugonjwa wa uchama unakusumbua.
 
Back
Top Bottom