Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,838
Je,kuwa Rais una kibali cha kugawa hela mitaani kama njugu?
Wale ng'ombe aliowagawia maaskofu kule Arusha kawatoa kwenye zizi lake huko kwao?
Hela yote ya JMTZ ni Mali ya Raisi wa JMTZ!
Je,kuwa Rais una kibali cha kugawa hela mitaani kama njugu?
Wale ng'ombe aliowagawia maaskofu kule Arusha kawatoa kwenye zizi lake huko kwao?
Kabisa hata mimi nafikiri hivyo hili ni wazo zuri. Wangekutana CAG, Mh. Zitto, Katibu wizara ya fedha wasome taarifa hizo na kutoa tamko la pamoja kabla ya PAC. Ili kuondoa mzizi wa fitina - Inasikitisha kuona Rais anakerwa sana na watu kuhoji au kutuhumu serikali kwa mambo tofauti. Sasa huwa nashindwa kuelewa kiapo gani yeye alichokiapa kulinda na kufata katiba ya nchi? Yeye siku zote anasema kwamba aliapa kulinda katiba kwamba hakuna mtu ataleta vurugu. Anafikiri kulinda katiba ni kutumia vyombo vya dola tu kwa kukamata watu na kuwatisha! Hajui kwamba katiba hiyo hiyo inawapa raia na wanasiasa haki sawa ya kuhoji na kutuhumu. Yeye tafsiri ya uzalendo ni mwanachi kutokuhoji chochote! Yaani mtu akihoji tu ni kosa anataka kila kitu serikali inachofanya au inachotenda kisiulizwe ila watu waseme 'ndiyo mzee' kwa lolote. Anadiriki mpaka kufikiria kudhibiti mitandao ndiyo inaweza kuwa suluhisho. Badala ya serikali kuwa 'Proactive' na kujibu hoja kwa wakati na pia kuondoa usiri. Watanzania wote wana haki na wanapaswa kujua kila senti ya serikali inavyotumika sababu ni hela zao!Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!
Naona wanataka kuiga China lkn kule hela za wachina hazichezewi hovyo hata ukiwa raisi unanyongwa tu,Facebook na Wasap hakuna lkn wanayo mitandao yao mfano we chat nk,si kila nchi ina mitandao sawa nchi zingine wanayo ya aina yao,Hakuna mchina anaekufa kwa kukosa Dawa hospital au kashindwa kusoma sababu ya ada,miundombinu ya China hadi vijijini iko vizuri, China hawafikirii basic needs walishatoka huko.Umasikini wetu ccm ndo chanzo na heri ya hata wakoloni japo walitunyima Uhuru lkn walituletea maendeleo, kuliko ccm inatunyima vyote.Kabisa hata mimi nafikiri hivyo hili ni wazo zuri. Wangekutana CAG, Mh. Zitto, Katibu wizara ya fedha wasome taarifa hizo na kutoa tamko la pamoja kabla ya PAC. Ili kuondoa mzizi wa fitina - Inasikitisha kuona Rais anakerwa sana na watu kuhoji au kutuhumu serikali kwa mambo tofauti. Sasa huwa nashindwa kuelewa kiapo gani yeye alichokiapa kulinda na kufata katiba ya nchi? Yeye siku zote anasema kwamba aliapa kulinda katiba kwamba hakuna mtu ataleta vurugu. Anafikiri kulinda katiba ni kutumia vyombo vya dola tu kwa kukamata watu na kuwatisha! Hajui kwamba katiba hiyo hiyo inawapa raia na wanasiasa haki sawa ya kuhoji na kutuhumu. Yeye tafsiri ya uzalendo ni mwanachi kutokuhoji chochote! Yaani mtu akihoji tu ni kosa anataka kila kitu serikali inachofanya au inachotenda kisiulizwe ila watu waseme 'ndiyo mzee' kwa lolote. Anadiriki mpaka kufikiria kudhibiti mitandao ndiyo inaweza kuwa suluhisho. Badala ya serikali kuwa 'Proactive' na kujibu hoja kwa wakati na pia kuondoa usiri. Watanzania wote wana haki na wanapaswa kujua kila senti ya serikali inavyotumika sababu ni hela zao!
Hii ndio hoja muhimu sana. Nashangazwa na watu kukasirika kwamba wananchi wana hoji. Sasa wananchi wangefanyaje kama hakuna mtu anawapa taarifa kwa uhakika? Prof. Assad alitakiwa kusimama mara moja kabla ya kupigiwa simu na Rais kuulizwa... kwanini hakutoa maelezo kumsahihisha Zitto na badala yake kazi hiyo inafanya na Polepole? ambaye anawahi kutoa maelezo yanayofanana na yanayotolewa na Naibu Waziri leo?
Hakuna haja ya kuwa na mitandao km inatumiwa kupotosha, kutukana na kudhalilisha watu..nchi haiwezi kuwa jalala na taifa la wahalifu, ufinyu wa akili wa watz wengi ndiyo tatizo kubwa elimu yetu haifuti ujinga tena..hata Phd holders ni wajinga, nchi hii ilikuwepo, ipo na itakuwepo kwa anayejua nadharia za maendeleo hafikirii kufa kwake ndiyo mwisho wa Tanzania, unapokuwa kiongozi una wajibu waa kulinda maslahi hata ya kizazi cha tano mbele! tunajenga taifa gani la kudhihakiana, wadogo kutukana wakubwa, lugha za matusi mitandaoni ndio ushujaa...ukiachia hali hiyo taifa halina future!! inashangaza wakati huu ambao serikali inadhibiti uhalifu na aina zote za uovu watu hawatambui, lakini hitilafu ndogo ya kitakwimu ndiyo imekuwa ajenda..siku za nyuma ambapo uovu ulitamalaki, mishahara hewa, safari hewa, Escrow..nk kelele hizi hazikusikika..nini maana yake, kelele nyingi mitandaoni ni za waathirika wa maamuzi na uendeshaji wa serikali awamu ya tano, wengi ni wahanga wa uhalifu uliozoeleka zama zilizopita ambao sasa umekomeshwa!Kabisa hata mimi nafikiri hivyo hili ni wazo zuri. Wangekutana CAG, Mh. Zitto, Katibu wizara ya fedha wasome taarifa hizo na kutoa tamko la pamoja kabla ya PAC. Ili kuondoa mzizi wa fitina - Inasikitisha kuona Rais anakerwa sana na watu kuhoji au kutuhumu serikali kwa mambo tofauti. Sasa huwa nashindwa kuelewa kiapo gani yeye alichokiapa kulinda na kufata katiba ya nchi? Yeye siku zote anasema kwamba aliapa kulinda katiba kwamba hakuna mtu ataleta vurugu. Anafikiri kulinda katiba ni kutumia vyombo vya dola tu kwa kukamata watu na kuwatisha! Hajui kwamba katiba hiyo hiyo inawapa raia na wanasiasa haki sawa ya kuhoji na kutuhumu. Yeye tafsiri ya uzalendo ni mwanachi kutokuhoji chochote! Yaani mtu akihoji tu ni kosa anataka kila kitu serikali inachofanya au inachotenda kisiulizwe ila watu waseme 'ndiyo mzee' kwa lolote. Anadiriki mpaka kufikiria kudhibiti mitandao ndiyo inaweza kuwa suluhisho. Badala ya serikali kuwa 'Proactive' na kujibu hoja kwa wakati na pia kuondoa usiri. Watanzania wote wana haki na wanapaswa kujua kila senti ya serikali inavyotumika sababu ni hela zao!
Kuchunguza kile CAG alichokiripoti juu ya kutoonekana kwa zile pesa. Naamini ulimsikia CAG akiliasa Bunge liihoji serikali juu ya hizo pesa. Sitaki kuamini kwamba umeridhika na 'utetezi' wa serikali, wakati walipewa nafasi ya 'kujitetea' kabla ya ripoti kupelekwa Bungeni.Ya kuchunguza nini sasa? hapa hakuna cha kuchunguza unless mnataka kuwatafutia watu upigaji wa ukweli sasa
Hakika chiefhii ni hoja na ushahidi uko wazi ndani ya ripoti ya CAG; ni tatizo la muda mrefu na bado halijapatiwa dawa..
A BIT CLUELESS BRUH, LETS END IT UP HERE.Qualified comment
![]()
Na. M. M. Mwanakijiji
Kwa Mara Nyingine
Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.
Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!
Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.
CAG Anajua Kulikoroga
Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.
Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri
Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!
Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?
Hoja ya Trilioni 1.5
Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.
Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.
Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?
Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!
Serikali Iwe "Proactive"
Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' inayosubiri kutenda baada ya tukio (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'pro active' (isiyosubiri) yaani inayowahi kutenda kabla ya tukio. Ukiona moshi una uamuzi wa kuwahi kuzima kabla miale haijaanza kuweka (proactive) au unaweeza kusubiri vianze kuungua uanze kujitahidi kuzima moto (reactive).
Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!
Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!
Magufuli Bado ni Mtu Sahihi
Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.
Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.
Tukimalizana na Hili
Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.
Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.
Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.
Au ni wepesi kusahau.
itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com
MM watu wapo sahihi kiasi fulani; ikitokea sitofahamu katika jamii ambayo kuna kikundi kinafanya kazi kwa usiri mkubwa ni lazima watu waanze kuspeculate differently. Chanzo cha speculation ni kutafuta majibu ambayo wanajua hawatapata kutoka kwenye kundi amabalo halitaki mambo yao yajulikane na yahojiwe.Kwanini kuwe na machafuko? wananchi nao ni lazima wawe na akili ya kutafakari vitu.. sasa mtu kasema Trilioni 1.5 haijulikani ilipo, watu wanaanza kusema imeibwa, imeliwa, amechukua kaweka Chato.. n.k sasa haya yote yanatoka wapi?
Mkuu riwaya yetu bado haijaingia mtaani?
Mwana Kijiji bandiko lako limetiririka vizuri lakini likamaliza vibaya. Usahihi wa JPM na hali tuliyo nayo kama nchi unatoka wapi? Mtu anayelaani tarishi (mitandao) badala ya "yaliyomo"? Una lako jambo na usitulazimishe tuanze kubuni ni lipi?
Kaiba nini na wapi?We Mwanakijiji unatetea Mwizi
1.5 T haijulikani ilipo mkuuKaiba nini na wapi?