Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Hapo ndio penye tatizo.. unaweza kufikiria uko moto lakini kumbe unajiunguza mwenyewe... jifunze kuangalia vitu with a balance.. siyo ili uonekane uko upande fulani uwaridhishe watu fulani.. usiogope kuwaudhi watu kwa msimamo wako.
Mwanakijiji. Kuangalia with a balance? Hakuna uandishi duniani ulio balanced. Labda uniambie ni balanced kwa kiwango gani. Period. Umendika, tumesoma lakini nayakumbuka sama maandishi yako toka zamani. Najua ulipokuwa unaegemea. Walao sasa mizani yako imefanyiwa matengenezo.
 
Hoja mezani imenikumbusha Mwalimu wangu wa hesabu nilipokuwa shule ya msingi, alikuwa hajui hesabu. Kujilinda, akawa mkali sana anapofundisha ili tusimwuulize maswali. Kwahiyo akija kwenye kipindi kila mwanafunzi alitamani muda uishe na mwalimu huyo aondoke.

Ilishasemwa huyu baba si mwanasiasa na uongozi hajui kabisa. Kwa agoli ya mkono wakamweka madarakani! Leo hii hata mafundi wa kuwaweka mambumbumbu madarakani kwa mkono nao wanajuta.

Natamani muda wake uishe aondoke. Hajui na hajui kama hajui, atakuaje Proactive? Hapo lazima awe Reactive. Kwasababu hiyo ndiyo kinga yake.

Nampa pole Lissu na kumpongeza kwa ujasiri wake na leo nampongeza zaidi Zitto ambaye amethubutu kusema wakati anajua kilichomtokea Lissu. Halafu ameenda mbali zaidi kwa kusema yuko tayari apigwe risasi zaidi ya 38 alizopigwa Lissu ili afe.

Lissu na Zitto wakifa, tutayaona machozi ya Tanzania lakini siyo Magufuli.
 
Kwanini kuwe na machafuko? wananchi nao ni lazima wawe na akili ya kutafakari vitu.. sasa mtu kasema Trilioni 1.5 haijulikani ilipo, watu wanaanza kusema imeibwa, imeliwa, amechukua kaweka Chato.. n.k sasa haya yote yanatoka wapi?
Usiposema zilipo si utakuwa umeacha room ya watu wa kusemee ziliopo?
 
Matumizi holela nje ya bajeti yanafanywa na yeye mwenyewe,
Tenda hazitangazwi anakwenda kununua vitu vya mabilion utadhani anakwenda kununua kitoweo?
Na akiambiwa anakuwa mkali na kujitapa eti sipangiwi, sasa hiyo bajeti inayopangwa bungeni ni ya kazi gani?
Bado tunataka kujua hiyo 1.5 t imetumikaje?
 
Mtoa mada na hoja dhàifu. 1.5 trilioni hazionekani mahesabu yake. Mambo ya Reactive na Proactive yapelekwe Lumumba fc. Kwani ni dhambi kuwa reactive kwa namna ya kujibu hoja kwa namna nzuri? Serikali inatakiwa iwe na hivyo vyote lakini kwa staha.
 
Hivi matuhuma yoote na tumbuatumbua hadi leo waliotumbuliwa hawawezi kuzipoteza hizi pesa?
 
Je,kuwa Rais una kibali cha kugawa hela mitaani kama njugu?
Wale ng'ombe aliowagawia maaskofu kule Arusha kawatoa kwenye zizi lake huko kwao?
Tujadili mambo mazito achana na huu utoto, hata dereva tu wa Rais anao uwezo wa kununuwa hao ng'ombe.

By the way labda nikutaarifu tu Rais ana fungu lake linaitwa consolidated fund na halihojiwi wala halina Auditing.

Tujikite kwenye report ya CAG ndipo tulipopigwa achana na maaskofu hao kwanza kina Pengo ni mawakala wa Kitengo na ccm.
 
Acha kutumia lugha ya kitapeli 2×3=6
3×2=6

Tubishane kwa hoja mambo ya kutumika hiyoo defence mechanism yakushindwa.

Tatizo lako nimeshalijua Mara ya kwanza ulivyoniquote nilijua tunaweza kulichambua hili swala lakini.

Nimegundua ugonjwa wa uchama unakusumbua.
Qualified opinions
 
Kwanini kuwe na machafuko? wananchi nao ni lazima wawe na akili ya kutafakari vitu.. sasa mtu kasema Trilioni 1.5 haijulikani ilipo, watu wanaanza kusema imeibwa, imeliwa, amechukua kaweka Chato.. n.k sasa haya yote yanatoka wapi?
Na siyo lazima yawe machafuko ya kutandikana "ngumi".Hata machafuko ya akili na nyoyo ni dhahma kubwa.
 
Nmesikia hao majaji wapya wameteuliwa kwa kazi maalum......kaz gani hiyo, au kushugulikia watu wenye kariba kama ya zito???
 
Acheni wapige pesa ndio muda wao huu wa kula
 
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Proactive"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' inayosubiri kutenda baada ya tukio (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'pro active' (isiyosubiri) yaani inayowahi kutenda kabla ya tukio. Ukiona moshi una uamuzi wa kuwahi kuzima kabla miale haijaanza kuweka (proactive) au unaweeza kusubiri vianze kuungua uanze kujitahidi kuzima moto (reactive).

Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com

Nakubaliana nawe 100%, pia nilikuwa nafikiri jinsi Zitto alivyosoma na kutafsiri taarifa ya CAG hata kupelekea haya kujulikana. Tunahitaji wabunge makini ili watusaidie katika kuhoji masuala yenye maslahi kwa Taifa.
 
Sasa hiyo hoja si wajibu..mbona kujibu hoja ya wakaguzi ni simple tuu ukiwa na nyaraka..kama hawana nyaraka basi wasitulaumu tukihoji, haiwezekani utumie 1.5T then hutuelezi umetumiaje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 23, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Butiama mkoani Mara Solomoni Ngiliule kuanzia leo kutokana na ubadhirifu wa fedha za Umma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza maamuzi hayo leo zikiwa zimepita siku tatu toka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Waziri Mkuu aliagiza kiongozi huyo kuchunguzwa kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo huku fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazikujulikani zimetumikaje.
 
Inawezekana kabisa anaamini anafanya kazi nzuri ya kuinyosha nchi; ripoti ya CAG inaonesha vinginevyo. Hata hivyo, kuna hesabu watu hawajazipiga vizuri... mnafikiria majaji walioteuliwa hivi juzi ni kwa bahati mbaya tu...
Sio kwa bahati mbaya. Ndio maana wengi wao ni makada.
 
Mkuu nje ya inchi???

CAG hakuwai kuuliza 1.5tril iko wapi?? Alivyo sema bunge lihoji ulipo na ilivyo tumika manaake ni nini?


PAC kama daraja kati ya serekali na CAG wamesubiri Maelezo lakini wapi.

IPSAS ni new to the government but not new to ACCOUNTING usifikiri Abas hajui alicho kiandika. IPSAS ni mlango wa kukimbia shutuma.

Wewe ndo hujaelewa achana na kukimbilia hatifungani. Pesa ilikuwepo na imetumika ila haikuingia kwenye vitabu vya mahesabu.
IPSAS hata mwaka jana wa pesa ilitumika kama sababu. Hii imeanza kutumika siku nyingi na wala haiwezi kuwa sababu. Nyuma ya pazia kuna sababu halisi ya 1.5 tr kutoonyeshwa kwa mkaguzi. CAG ana sababu ya kusema fedha hizo zimetumika sehemu ingine isiyoidhinishwa na Bunge
 
Ata endelea hivi mpka lini miaka 7 mbele kwa staili hii huoni anatumbukiza inchi kwenye machafuko?
Kweli nchi hii ina tatizo la uelewa hakuna mahali Zitto kasema zimeibiwa alichohiji ni "matumizi ya 1.5 hazijulikani matumizi yake ni yepi namkaguzi amesema wabunge wahoji wapewe mchangauo " mbona mnamtia zitto maneno mdomoni ?
 
Back
Top Bottom