Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Tafadhali Magufuli: Matatizo Haya Mengine Mnajitakia Bure

Mahaba ni hatari, ule uwezo na umakini was mwanakijiji sijui umeenda wapi!....kama vile anamatarajio Fulani Siku hizi!....time will tell..
 
WALIPA KODI KODI KUHOJI KODI ZAO ZIMETUMIKA VIPI SIO KOSA.

KAMA ZIMETUMIKA KWA MAMBO MENGINE YASIYOPANGWA NA BUNGE WASEME TU,KULIKO KURUKARUKA NDIO KUNAZUA MASWALI!
 
Muhimu ni maelezo yatakayo tufanya tuone uhalali wa trilioni 1.5 zilikoenda hakuna haja ya kutisha watu kwa sheria ama mitandao kisa hawana udhibiti nayo.

Watoe maelezo hatutaki kutishana
 
CAG kabla ya kukamilisha ripoti Yake alitoa siku 21 kwa serekali itoe Maelezo/hesabu namna 1.5tril ilivyotumika wameshindwa.


Kwanini tusiseme ni wizi????

Kusema tu tumezitumia kwa hili na hili ni tatizo???


Mtu anaweza kukuita mwizi kwa matendo yako. Hii zungusha zungusha inatoa loop hole ya sisi kusema zimeibiwa.
CAG Hakuwahi kuuliza 1.5T. Hizo zimeibuliwa ukurasa wa 34 collection vs. expenditure.
Kwa mfumo wa IPSAS, collection huhesabiwa hata kama zipo kwenye form ya hatifungani ambazo hazijaiva.
Kuelewa kirahisi, jumlisha hela za kodi na zisizo za kodi na mikopo na misaada kutoka nje. Hizo ndiyo hela cash ambazo unaweza kuzitawanya chapchap utapozipata.
Hatifungani, pamoja na kuwa ni hela halali, liquidity yake siyo sawa na hela za kodi na misaada. Securities huwa zinawachanganya watu, na nyingi zao hutumika ku-rollover madeni ya ndani.
Hata wanasiasa wa CCM,CDM,CUF,ACT wote nimeshawasikia wakizielezea vibaya hela za hatifungani. Wengi wao, pamoja na kusoma kwao bado ni weupe sana kwenye haya mambo.
Wanasiasa wengi Tanzania, hawapo enlightened na hii itakuja kutugharimu mbele tusipochukua tahadhari.
 
CAG Hakuwahi kuuliza 1.5T. Hizo zimeibuliwa ukurasa wa 34 collection vs. expenditure.
Kwa mfumo wa IPSAS, collection huhesabiwa hata kama zipo kwenye form ya hatifungani ambazo hazijaiva.
Kuelewa kirahisi, jumlisha hela za kodi na zisizo za kodi na mikopo na misaada kutoka nje. Hizo ndiyo hela cash ambazo unaweza kuzitawanya chapchap utapozipata.
Hatifungani, pamoja na kuwa ni hela halali, liquidity yake siyo sawa na hela za kodi na misaada. Securities huwa zinawachanganya watu, na nyingi zao hutumika ku-rollover madeni ya ndani.
Hata wanasiasa wa CCM,CDM,CUF,ACT wote nimeshawasikia wakizielezea vibaya hela za hatifungani. Wengi wao, pamoja na kusoma kwao bado ni weupe sana kwenye haya mambo.
Wanasiasa wengi Tanzania, hawapo enlightened na hii itakuja kutugharimu mbele tusipochukua tahadhari.
what is your point?naona unazurura tu
unafikiri IPSAS imeanza kutumika kuanzia mwaka 2016?
hizi standard zimeanza kutumika tokea 2013,mbona hatukuwahi kusikia maelezo haya?kwa hiyo unataka kusema Assad ni mweupe kwenye accounting standards?
 
Ila hii pesa imetafunwa mazeee,wenye akili tunajua wanafanya danganya toto kujitetea. Pesa imefumuliwa.
 
Lumumba pekee mwenye uwezo wa kujenga hoja nzito humu JF.
Ana balance mambo na sio mnafiki.

Anyway nikirudi kwenye point nadhani kutumia pesa nje ya mipango ni utovu wa nidhamu na JPM ana kesi ya kujibu hapa,
Haitaji kua mkali.
 
Ninyi watu buaaaana
Sasa huyu mnayemtetea yupo vizuri hivi mmelogwa au
Okay hao aliowateua mpaka sasa wamefanya nini maana yeye ndiye kila kitu
Tupo pazuri wapi ununuzi wa ndege ndio tunaenda vizuri kujichotea pesa hazina na mpwa wake na bashite tunaenda vizuri bashite kufuja pesa za wavuja jasho tunaenda vizuri kwenda kutungiana mimba nje ya nchi tunaenda vizuri kuwabagua wabunge kwenye swala matibabu tunaenda vizuri kurusha vijembe kama mwana$&&e tunaenda vizuri kilimo hakina mwelekeo tunaenda vizuri vijana hawana kazi tunaenda vizuri bandari hakuna meli tunaenda vizuri hospitali hazina dawa tunaenda vizuri
Hivi vizuri ni vipi? Vizuri kwa wachache
Acheni kufanya WaTz wote wajinga ninyi ndio mna akili??
Hafai kuwa kiongozi period!
 
YAANI HII HABARI TA TRILION 1.5 INGEKUA UONGO KUNA WATU WANGESHALALA SELO,KUBALINI HUYO JIWE HASAFISHIKI!
 
Inawezekana kabisa anaamini anafanya kazi nzuri ya kuinyosha nchi; ripoti ya CAG inaonesha vinginevyo. Hata hivyo, kuna hesabu watu hawajazipiga vizuri... mnafikiria majaji walioteuliwa hivi juzi ni kwa bahati mbaya tu...

Kwa mtiririko wa maelezo yake, inaonekana hao majaji watakuja kutekeleza sheria kwa utashi wa mkulu. Jaribu kuangalia maelezo yake utajua ninachokuambia.
 
what is your point?naona unazurura tu
unafikiri IPSAS imeanza kutumika kuanzia mwaka 2016?
hizi standard zimeanza kutumika tokea 2013,mbona hatukuwahi kusikia maelezo haya?kwa hiyo unataka kusema Assad ni mweupe kwenye accounting standards?
Nani aliyekwambia zimeanza jana? We vipi?
Angalia cash budget za BoT. Kuna tofauti yeyote ya maana kwenye mapato na matumizi?
Mbona exchequer releases ni 20T? Hizo zingine zimeenda wapi?
13.16 recurrent na 6.9 development. Makusanyo, Grants na disbursed loans 3.1T na Revenue za ndani 16.34T.
Hiyo ni cash budget, easily explainable. Na BOT anakwambia (July, MER) cumulative domestic debt due ni 5.9T, waka-rollover 4.6T. Sasa explanations za leo zina tofauti gani na MER au BER? Au unaongea kishabiki tu?
Halafu nani kasema Assad ni mweupe? Are you serious?
Assad hakuuliza 1.5 hata sehemu moja. Kwenye appendix za Central Govt expenditure audits kuna hoja ya 325billions TRA ilizokusanya kwa ajili ya other agencies kuwa entered twice kwenye consolidated accounts[3.2: 4(m)].
List of qualified opinions zipo kuanzia ukurasa wa 307 mpaka 315. Hakuna 1.5T ilipotajwa, nada!
Usilazimishe mambo.
 
Anyway nikirudi kwenye point nadhani kutumia pesa nje ya mipango ni utovu wa nidhamu na JPM ana kesi ya kujibu hapa,
Haitaji kua mkali.

hii ni hoja na ushahidi uko wazi ndani ya ripoti ya CAG; ni tatizo la muda mrefu na bado halijapatiwa dawa..
 
1.png

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa Mara Nyingine

Kwa mara nyingine tena tunashuhudia Serikali inakimbia kujitetea (on the defensive). Zinatolewa tuhuma, tena nzito lakini kwa mambo ambayo yanajibika vizuri. Mtu mmoja aliwahi kuandika kitabu cha "Lies, Damn Lies and Statistics". Alitumia maneno ambayo yananukuliwa toka kwa mwandishi Mark Twain. Katika andiko hilo alielezea jinsi gani namba zinaweza kutumiwa kusema uongo, kuchanganya watu na hata kufanya watu waamini kitu kisichokuwepo. Takwimu zinaweza kutumika kuthibitisha lolote lile.

Kwa mara hii nyingine tunashuhudia serikali inaonekana kukerwa, kusikitishwa na kushangazwa na jinsi gani watu wanahoji takwimu mbalimbali. Serikali inasikitika kwa sababu kina Zitto na wengine wanasema "mbona hizi namba haziingii kichwani"? Majibu yanayotolewa yanatolewa kujaribu kuelezea kwanini hizi namba ziingie kichwani; hata kama hazitoshi!

Sasa mwisho wa siku Rais anakasirishwa kwa nini watu wanaandika kwenye mitandao na kuhoji kwenye forum mbalimbali kana kwamba tatizo ni mitandao! Lakini hili ni tatizo la kujitakia kwa kweli kabisa; ni tatizo ambalo linaweza kuepukika.

CAG Anajua Kulikoroga

Ripoti za CAG zimekuwa ni mojawapo ya nyaraka muhimu za kitaifa ambazo zinawafikia wananchi bila kuchujwa. Matokeo yake wananchi wanapozisoma wanaona vitu ambavyo "haviingii kichwani"; wanaamua kuhoji. Kwa mara nyingine ripoti ya CAG inazua mjadala mzito na kwa mara nyingine CAG anachelewa kuweka sawa na kuacha mjadala huu uwe kama unga uliokandwa ukisubiriwa uumuke.

Serikali Haiwezi Kuendesha Nchi kwa Usiri

Serikali inajikuta inaanza kujitetea. Inanikumbuka wakati wa hoja ya ndege yetu ya Bombardier kukamatwa Canada. Hatukujua kuwa imekamatwa, hakukuwa na kiongozi yeyote aliyesema (kabla ya Lissu) kuwa tunadaiwa na ndege yetu inaweza kuzuiwa. Wakuu wetu wakaamua kulimaliza kimya kimya hadi lilipoibuliwa, na kuumbuliwa na Tundu Lissu. Watu wakamkasirikia Lissu kwa kutuambia kile ambacho wao walipaswa kuliambia taifa! Walikasirishwa kwa sababu Watanzania (wenye hela zao) hawakutakiwa kujua. Lissu aoneshwa kama 'adui'!

Serikali inapojaribu kufanya vitu siri visivyopaswa kuwa siri itajikuta inaona imeumbuliwa wakati kama ingekuwa wazi mapema ingeonekana iko makini. Anayeficha maradhi wahenga walisema msiba ndio utamuumbua. Kama kuna tatizo ni bora zaidi kuliwahi na kuwaambia Watanzania mapema kuliko kuficha au kutokujali kuwaambia tukiamini kuwa hawatajua. Wakija kujua kwa njia nyingine tusiwakasirikie kwanini wameambiwa! Kama Mzazi hujakaa na watoto wako ukawaambia kuwa nyumba yenu imepigwa mnada usishangae watoto wakasikia mtaani na wakaja kukuhoji kwa ukali. Au tumesahau ya yule mtoto wa Bukoba hivi majuzi?

Hoja ya Trilioni 1.5

Kwa mara nyingine tena, wakuu wote wanajua kilichotokea kwenye Trilioni 1.5. Hazikuibwa, hazikuwekwa kwenye akaunti maalumu ya Magufuli, hazikuliwa. Ni hela ambazo ama zimetumiwa vibaya (kama anavyodai Zitto Kabwe) au hazijafafanuliwa vizuri katika ripoti ya CAG - kama Naibu Waziri wa Fedha, alivyodai katika taarifa yake leo. Hakuna njia ya katikati.

Kwa mara nyingine, tunataka kumfanya Zitto awe adui kwa kuhoji ambacho serikali na CAG haikukifafanua au kuyaweka wazi mapema. Hivi, walitarajia watu wafanye nini? Kwamba, watu waangalie namba tu wasijumlishe wenyewe na kuzikokotoa? Kwamba kwa vile CAG kaandika namba basi watu wazimeze tu bila kuhoji? Hivi Mungu alitupa ubongo wa nini? Wanaotawaliwa ni wananchi, na wanaotawala ni wananchi; watawala wana ubongo na watawaliwa wana ubongo; bongo zikigongana ndio tunapata mtazamo mpana zaidi wa mambo.

Binafsi naamini maelezo ya Serikali (ya leo) yanawezekana yanakaribiana na ukweli zaidi kuliko maelezo ya Zitto. Hata hivyo Zitto hajui fedha zimeenda wapi; hajadai zimeibiwa (madai haya ni ya wengine), hajadai Magufuli amezila au amegawa kwa washirika wake; hajadai zimeingizwa kwenye akaunti ya CCM au kwa ajili ya kampeni; anachouliza ni kuwa "hesabu haziingii kichwani". Jibu la serikali kwa mara nyingine limechelewa; linakuja likiandamana na mikwara na vitisho badala ya shukrani. Kama Zitto asingehoji kwa ukali hivi, nani angetoa maelezo? Kama Zitto asingehoji hivi kwa ukali Rais Magufuli angeamuaje kuwahoji kina Prof. Assad na Waziri wa Fedha leo hadharani? Angewapigia simu vipi kupata maelezo?

Zitto anatakiwa ashikwe mkono na kupewa shukrani. Inawezekana Zitto anahoji kwa ukali kwa sababu za kisiasa - ilianzia kwa halmashauri yake kuwa mionngoni mwa halmashauri zilizopata hati chafu, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo akaondolewa kazini. Inawezekana hilo lilimuua. Akaamua kutaka kuonesha kuwa "uchafu" huu hauko Kigoma tu; hauko Ujiji peke yake; ni uchafu ulioko kwenye mfumo mzima wa serikali zetu (kuu na za mitaa). Inawezekana ukali wake umetokana na haya. Na hata tukikubaliana kuwa hii ndio sababu, bado Zitto yuko sahihi kuhoji!

Serikali Iwe "Active"

Kwa mara nyingine, Serikali inapaswa kuacha kuwa 'reactive' (inayosubiri moto uwake ndio ikimbie na ndoo ya maji kuzima!); inapaswa kuwa 'active' (isiyosubiri). Ripoti ya CAG ilipotolewa na hoja ya Zitto ilipoibuliwa mara moja, Waziri na viongozi wa serikali walitakiwa kukaa chini na Mbunge huyu na kuhojiana na kupeana maelezo ya nini hasa kimetokea. Zitto kama mwakilishi wa wananchi ana haki ya kuhoji na wao Serikali iliyowekwa na wananchi wanapaswa kujibu! Si kwa vitisho bali hoja kwa hoja na siyo vihoja!

Kwa mara nyingine tena, Zitto anaibuka kama shujaa aliyejeruhiwa; shujaa ambaye ana chama kidogo zaidi na yawezekana kikiwa dhaifu lakini chenye kuthubutu. Udogo wa chama chake si udhaifu wa hoja zake. Ningekuwa naweza kupendekeza kumaliza hili ningewaita Zitto na Prof. Assad na Wizara wakae chini waje na maelezo ya kumridhisha Zitto na kwa niaba yake kuwaridhisha wale waliodandia treni la "IKO WAPI TRILIONI 1.5". Inawezekana kabisa treni hilo lilikuwa haliendi popote lakini mlio wake unashtua!

Magufuli Bado ni Mtu Sahihi

Ukiniuliza mimi hata hivyo bado imani yangu haijapotea. Sidhani kama kuna Rais yeyote au mtu mwingine yeyote anayeweza kufuatilia haya kwa ukali unaostahili kama Magufuli. Wale ambao wanataka Magufuli ashughulikie wasome alama za nyakati. Watu wasije anza kulia tena "dikteta kacharuka" Rais Magufuli atakapoanza kuwatia ndani na kuwatimua watu kazi sababu ya ripoti ya CAG. Hili lipo, linakuja, na litawashtua wengine. Sisi wengine hatutashtuka kwa sababu tunajua kama kuna mtu anaweza kuthubutu kumvika paka kengele mtu ni Magufuli.

Ni kwa sababu hiyo bado tunamuunga mkono. Ashughulikie na wafujaji na wanaotumia madaraka vibaya, ashughulike na vibaka wa urithi wetu na utajiri wetu. Ashughulike kwa ukali na wanaochezea fedha za umma kama wana akili mbovu. Hawa wanaohoji, hawa wanauliza wala wasimsumbue kwani wanamsaidia hata kama wanafanya hivyo kwa sababu nyingine. Lakini kusaidia wanasaidia.

Tukimalizana na Hili

Tukimalizana na hili; kwa mara nyingine tujadili sasa ripoti ya CAG na yale makubwa yaliyoibuliwa ndani yake, yale ya ufujaji wa fedha za umma, yale ya kutozingatia sheria za manunuzi, yale ya matumizi mabaya ya madaraka, yale ya vitabu vya ukaguzi vyenye kucheza tiari bado, yale ya akaunti zenye miiba na yale yote ambayo yanatuonesha na kututhibitishia kuwa tatizo letu la matumizi ya fedha za umma bado lipo.

Kwamba, bado pamoja na jihada kubwa za kuisafisha nchi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavvyo na kuwa za moto hadi ziwatokee watu "puani" kama alivyodai Magufuli, bado Rais Magufuli anakabiliwa na tatizo kubwa sana la kusimamia fedha za umma. Siyo yeye kama yeye tu bali watu wa safu za chini bado hawaogopi fedha za umma. Na kama hawaziogopi ripoti ijayo ya CAG itakuja na mengine na mwaka mwingine tutarudi tena hapa hapa mwakani mwezi Aprili.

Tumegoma kujifunza, hatutaki kujifunza, ni wagumu kujifunza.

Au ni wepesi kusahau.

itaendelea: mwanakijiji@jamiiforums.com


Katika maisha yangu sijawahi kusikia ripoti ya ukaguzi ya mahesabu ikawa 100% sahihi na hii ni Dunia nzima, isitoshe huyu Mkaguzi yeye nani anamkagua? Kwa maana inavyoonekana kila mtu anaona mwingine ana makosa na huyu Mkaguzi yeye ni Malaika, siamini hilo kila kitu kuna margin of errors, hasa unadili na statistics, ...

Zito Kabwe hana usmart wowote sema tu nchi yetu wengi wetu ni less intelligent people ndo maana kitu ambacho kiko wazi kama hiki mtu anaonekana na genius, kumbe ni average tu!
 
Wananchi wanachanganywa tu.Kesho si ajabu baadhi ya magazet yakaandika "CAG amuumbua Zitto", mengine "CAG akana trilioni 1.5 kuibiwa", n.k lakini mtu ukijiuliza ni lini na wapi CAG aliwahi tamka kuwa hizo fedha zimeibiwa hupati jibu au ni lini Zitto alitamka kuwa hizo fedha zimeibiwa pia hutopata jibu.!

Haya sasa ndio naita magoli; hivi siku hizi zote hujasikia watu wanadai Magufuli kaiba, tena mwizi? Hujasoma watu wanaandika humu humu kuwa hizi trilioni 1.5 zimeliwa? Unafikiri kwanini Magu amemuliza CAG kwanini hakuripoti wizi wa trilioni 1.5? na mara moja CAG akasema "hakuna kitu kama hicho"? Kama fedha hazikuibwa ina maana hakuna uhalifu siyo; kuna hoja nyingine zinahitaji kujengwa kwa mfano 'hazikutolewa maelezo ya kutosha"..
 
Back
Top Bottom