Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Kinachonifurahisha ni kwamba watanzania huwa tunatazama picha upande mmoja kama watu wa kale!

Hakuna fisadi mwema, wala fisadi mwenye heri,
hakuna fisadi mwenye umalaika, wala ufisadi haubagui...
Fisadi ni fisadi awe mtawala ama mtawaliwa...
Cha ajabu ni kwamba wapo mafisadi hawatajwi na wamo katika upinzani na wengine wapo uraiani...
Kuna siri gani katika kubagua mafisadi??? Je kuna fisadi rafiki na fisadi adui???
 
Njia za kupata 8 zipo nyingi, mfano:
  • 2^3 =8
  • 4x2 =8
  • 6+2 =8
  • 10-2 =8
  • ...
Swali, je ni njia ipi iliyo bora zaidi?
 
Yeyote aliye msafi ndani ya ccm bara asimame na ajieleze mbele ya umma wa watz !!!!
 
Hivi Huyu January Makamba ana usafi kiasi gani ina maana kesi yake ya kuiba mitihani iliishia wapi? CCM ina maana watakatifu wake ndo hao hapo kwenye kamati kuu na Secreterieti yake. Hakika kama hawa ndo gamba jipya basi kumbe CCm ime tuthibitishia haina watu. Nawashauri wasitumie nguvu sana jamani kwani KILA CHENYE UHAI IKIWEPO CCM SHARTI KIONJE MAUTI, hAPA ccm INATAKA KUPINGANA NA NATURE TU WAKATI UKWELI NI KWAMBA tayari imezeeka na mauti yanakaribia . Wanapambana na kurudisha umri nyuma ili wasife . Wafanye wafanyalo hawana uwezo wa kujisafisha wakae tu ICU wasubiri Israel mtoa roho
Kama January ana issue ya mitihani, basi hiyo ni issue ndogo sana, issue haswa iko mji kasoro, wakati huo baba mjeshi. All and all, haijalishi ulifanya nini zamani, mambo mengine ni utoto. Kwa sasa he is a smart guy!. Yeye na Nape, ni vichwa vinavyokubalika, tatizo ni hili li dudu-CCM!.
 
Kama January ana issue ya mitihani, basi hiyo ni issue ndogo sana, issue haswa iko mji kasoro, wakati huo baba mjeshi. All and all, haijalishi ulifanya nini zamani, mambo mengine ni utoto. Kwa sasa he is a smart guy!. Yeye na Nape, ni vichwa vinavyokubalika, tatizo ni hili li dudu-CCM!.

Mkuu Pasco;

I quote you "Tatizo ni hili Dudu-CCM" and ask you two questions:

1. Ungekuwa ni wewe Kiongozi Mkuu wa CCM ungefanya nini?

2. Ungekuwa wewe ni Kiongozi Mkuu wa Chama kikuu cha Upinzani ungefanya nini?

Tunazungumzia katika kuleta maendeleo ya kweli ya Nchi.

Respect.
 
Hapo umenikumbusha story ya jamaa yangu Mkongo hapa zamani tulipokuwa tunafanya PhD alikuwa yuko bussy na biashara na alikuwa hakai sana Europe ili biashara zake zisi kuse connections; sasa nika muuliza wewe uko kwenye academia na unahangaika na biashara badala ya kukazana na publications ili upande haraka baadaye kuwa professor. Akaniambia inaelekea wewe ni mwafrika mwenye mawazo ya kizungu. Mimi ni mwafrika ninaye ishi kwa mbinu za vita maana Afrika bado tuko vitani na hii PhD ni Scud yangu pale silaha ndogo ndogo za kivita zikishindwa kumwondoa adui umaskini. Maana nipo hapa kutengeneza maisha si maisha kunitengeneza. So PhD hainiletei ugali kwenye sahani na bia kwenye glass kwa urahisi na kwa uhakika ila hizi biashara zangu. Ila ikitokea Africa ikawa kama Europe watu wakawa kwenye order basi ndo na mimi naingia kwenye silaha hii ambayo nai hifadhi kwa sasa yaani kuishi kwa ubongo uliokuwa formated ambayo kwa Africa kwa hali ilivyo shagalabagala utaishia kuning'iniza vyeti sebuleni na watoto hawana viatu mguuni. So I guess CHADEMA wanaielewa hasa siasa ya Tanzania na wanatumia silaha ndogo ndogo kwanza ku confuse the camp!

PhD ya kugema ulanzi au?
 
Pasco said:
Kama January ana issue ya mitihani, basi hiyo ni issue ndogo sana, issue haswa iko mji kasoro, wakati huo baba mjeshi. All and all, haijalishi ulifanya nini zamani, mambo mengine ni utoto. Kwa sasa he is a smart guy!. Yeye na Nape, ni vichwa vinavyokubalika, tatizo ni hili li dudu-CCM!.

Pasco,

..hata uwe kichwa namna gani, ukiingia kwenye hii CCM ya sasa hivi shurti uuvae ukilaza.

..nenda ukasome walichoongea Nape na Januari ktk mikutano yao ya Dsm na Zanzibar halafu uniambie kama kuna tofauti yoyote ile na matamshi aliyokuwa akitoa Tambwe Hiza.

..tatizo ni kwamba CCM ya sasa hivi iko so much out of touch na wananchi wa Tanzania. vilevile mkakati wa CCM kuwalaghai wananchi kwamba ufisadi unahusisha watu watatu tu ndani ya CCM nao ume-backfire.

..vijana hao walipaswa kusoma alama za nyakati na kujiunga na vyama vingine tofauti na CCM. nina hakika nje ya CCM vijana hawa wangeweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa hili.

NB:

..HUU MPOROMOKO WA CCM WA SASA HIVI UNAANZIA MWAKA 1995 BAADA YA LOWASSA NA JK KUWA NA MKAKATI WA PAMOJA WA KUTAFUTA URAISI WA NCHI HII.
 
Yeyote aliye msafi ndani ya ccm bara asimame na ajieleze mbele ya umma wa watz !!!!

Kwa nini ulihisi Magufuli ni Msafi wakati unajua kuwa yeye ni wa chama kile kile, tena ni muumini wa dini ile ile, na anatokea upande uleule wa wezi waliyoifikisha nchi hii pahala pabaya saaaaaaana.
 
Jamani hakika nimeshindwa hata kuamini!!.. post ya mwana jf inayo eleza yaliyo jiri tabora inaonyesha John malecela ni miungoni mwa mafisadi wa EPA na John magufuli ni FISADI wa nyumba za serekali sasa kama hawa naliokuwa wanaheshimiwa na jamii nao ni MAFISADI nani aliebaki ndani ya ccm alie msafi?

Kwa nini ulihisi Magufuli ni Msafi wakati unajua kuwa yeye ni wa chama kile kile, tena ni muumini wa dini ile ile, na anatokea upande uleule wa wezi waliyoifikisha nchi hii pahala pabaya saaaaaaana
 
William, Katiba ya Tanzania na sheria ya uchaguzi haitoi sehemu yoyote ya kushitaki kwa wizi wa kura za urais kama tume ikishamtangaza mgombea mmoja kuwa mshindi. That is end of it. Na ndiyo maana Watanzania tunataka Katiba mpya.
Lakini kumbuka kuwa wa kwanza kumwambia Malecela ni fisadi ni Sophia Simba wakati huo akiwa waziri. Hapo hujasema chochote, kama ufisadi wa Mzee Malecela ulionekana mpaka na walio ndani ya CCM na wakathubut kusema, basi nadhani kwetu sisi wananchi wa kawaida, tunadhani kuna makubwa zaidi na mengi kwa Mzee Malecele. Kama watu wana data zaidi za ufisadi wa huyu Mzee Malecele watujuze labda ni zaidi tu ya kusema ni fisadi.
Pia kumbuka kuwa kama mtu ameshiriki katika maamuzi ambayo yamepelekea fedha za nchi kutumika isivyo kwa manufaa ya kikundi fulani haijalishi kama yeye kama mtu amechukua kiasi gani au hajachukua lakini ni fisadi. Ukiangalia Mangula na Deep Green,Kagoda, nk. nadhani anafahamu zaidi kwani alikuwa katibu mkuu wa CCM wakati huo na kama alibariki zitokee maana yake yeye ni part of it, hawezi kukwepa lawama!!!

- Mkuu unasema kwamba tuna sheria iliyomruhusu Mtikila kwenda mahakamani na kuishinda Serikali? Hivi ni lini umewahi kumsikia Slaa akisema alishinda Urais? niwekee nukuu moja tu kutoka mdomoni mwa Slaa akidai alishinda Urais? Anyways ninakushukuru sana kwa usahidi wako mzito sana unao onyesha Malecela na Mangula kuhusika na wizi wa EPA!

William @ NYC, USA.
 
- Well, I guess huu wako ni ushahidi mzito sana kwamba Malecela anahusika na EPA, sawa sawa mkuu kwa kweli una ushahidi mzito sana!

William @ NYC, USA.

Mbona unajiuma na maneno? Malecela si bado ana influence ndani ya serikali - inner circle, let the democratic process takes its course then we will find out who store our money - EPA, Dowans, Richmond, Radar, Madini na shade deals zenu na familia za mafisadi. Achane wananchi na viongozi wa Chadema wapate kuona docs, mbona kama mmesoma Univ. nje ya nchi si mdajua umuhimu wa credibility na transparency katika society? au mlikuwa mnasoma jinsi ya kuwaibia wananchi na kujiweka madarakani miaka 50 kama kwamba wananchi milioni 43 Tanzania they are not smart or intelligent like you guys. You guys screw this country na mnataka kutuambia mnajua really democracy sio.
 
Heshima mbele waheshimiwa wote,
Kazi yetu kubwa sisi CDM ni kuwaeleza umma tatizo la umasikini wao liko wapi.
Na ili kuhakikisha umma unaelewa vizuri tatizo na jinsi ya kutoka kwenye tope lazima wajue wanaowaingiza kwenye matope ya umasikini.
Mafisadi wanatajwa na chama chetu ni njia moja ya kuwaelimisha wananchi wajue maana ya uwazi, usafi na nia thabiti ya kupambana na uhalifu bila kumung'unya maneno.

Orodha ya kwanza CCM wakiongozwa na familia zao walibisha walikataa, walisema maneno yote mabovu, walimtukana Dr. wa ukweli ila CDM walibaki firm kwani hawajakurupuka. Siku zinavyokwenda watakubali tu kwamba Malecela ni fisadi. najua sasa ni shock hawaamini. Kama hawa sio mafisadi waseme wakane wanayotuhumiwa nasi tutathibitisha, ila uthibitisho mkubwa ni maisha magumu ya watanzania chini ya viongozi wa CCM.

Ufisadi upo kwenye maeneo mengi,wizi wa moja kwa moja wa fedha za umma, matumumizi au maamuzi mabovu yamadaraka, usimamizi na kufumbia macho uozo, ushawishi ili kunufaisha kikundi au mtu kwa kutumia rasilimali za taifa huu wote ni ufisadi. CCM wanatakiwa kujua mafisadi wapo wengi sana humo ndani ila sisi tutawatangaza kwa awamu kwani hatutaki kukurupuka au kumwonea mtu. Wote waliotajwa ni mijizi mifisadi na watu hatari sana kwenye uchumi wa taifa letu masikini.
 
- Brother, Mzee siku zote anasema hivi ni haki ya wananchi kumtukana kwa sababu ni politician na huwa anatuasa sana kutokujibu, lakini binafsi sina wasi wasi naye hata chembe moja kwamba sio fisadi, ndio maana na mimi kama wewe ninaamini sana in the Truth hata kama kuna costs lakini unakuwa free, katika mijadala kama hii unachoweza kufanya ni kweka the doubt tu lakini huwezi kuwa-convince wananchi wote hasa wa hili taifa ambao tumezoea siasa za mabomu, zilizomfikisha Mrema alipo sasa!

- With all due respect ninasema hivi Dr. Slaa, afike mahali aambiwe na Chadema, kwamba enough na hizi siasa za kulipua mabomu na kuwepo kwenye media kila siku na ishus ambazo ni hadithi za mitaani zaidi kuliko faida yoyote kwa taifa, Mangula unawezaje kusema ni fisadi? I mean it does not make any sense, anachotaka Slaa ni kuendelea kusikika kwenye media na kujibizana na wasiomuelewa vizuri, huwezi kukisaidia chama chako cha siasa na habari ambazo huwezi kuthibitisha kisheria, ndio maana Marehemu Kambona aliishia kuanguka vibaya sana kisiasa aliposema Mwalimu na Kawawa ni mafisadi, yes it made a big headlines kwenye media, ila in the end ikammaliza kabisaa Kambona kisiasa.

- Otherwise, muda wangu siku hizi ni mdogo sana na JF imepanika sana sasa sio kama zamani sio rahisi ku-catchup na ishus zote hapa, ndio maana huwa tunachangua chagua, heshima yako sana ndugu yangu kwa debate ya kistaarabu na kufikia kwenye conclusion bila matusi na kejeli zisizo na tija wka taifa, UBARIKIWE SANA NITAKAPO KUJA TENA BONGO TUONANE MKUU, NILIKUWA HAPO BUNGENI LAST JUNE KWENYE BAJETI, NITAKUJA TENA SOON MAANA NINATAKA KUTAFUTA JIMBO YOU KNOW!

William @ NYC, USA.

Nimecheka sana! badala ya kulia; hivi unaweza vipi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Chama Cha Mafisadi, wewe ndio katibu Mkuu tena Makini alafu husiwe fisadi! Sijui kama inawezekana. hakuna mtu amefanya kazi baada ya Nyerere aliyeitendea haki Tanzania, nasikia ni Mramba Pekee na ndio maana Mkapa aliongea na Kikwete amkomeshe; taarifa sahihi ni kuwa aliye mwambia Kikwete amkomeshe Mramba ni Mkapa! Kama ambavyo Mkapa alivyoambiwa Mkomeshe Nalaila.

Kama ambavyo huwezi kumtenganisha Mwinyi, Malecela, na Marehemu Gama, ndivyo ambavyo huwezi kumtengenasha Mkapa, Sumaye na Mangula, hawana tofauti kama Kikwete, Lowasa na Makamba hiyo ndio CCM baada ya Mwalimu.

Mkama anazunguka kunadi CCM mpya sijui imesajiliwa lini? Tusibiri hiyo mpya labda Kikwete, Pinda na Mkama itakuwa kama Mwinyi, Msuya na Kolimba!
 
Sikuwahi kudhani kama politics ni mchezo mgumu hivi kwa baadhi ya watu! Wanaopinga hatua ya CDM kutaja mafisadi wapya, kwa kweli hawajui kabisa mchezo wa siasa.

Baada ya muda mrefu wa CCM kudhibitiwa na kuwa hawana ujanja, wamejitutumua na kuja na kauli (sio matendo), ya kujivua gamba. Kwa taarifa yenu hili lilikuwa shuti zuri sana la kuwarudisha CCM kwenye chati. So, CDM kukaa kimya ikiangalia, ingekuwa na grave mistake, kwani CCM wangekuwa wameenda mbali sana. Kwa hiyo CDM wameamua wadeflect move ya CCM.
Effect zake tayari mnaziona. Akina Nape hawana tena focused direction, anapambana na mambo mawili kwa wakati mmoja. Anapambana na mafisadi na anapambana na CDM. Anaenda mikoani sasa hivi, hajui lipi alipe uzito. Anapinga hoja ya mafisadi wapya lakini hana ubavu wa kuwataja kwa majina wale wa zamani. Anapotamka sentensi kuwa 'mafisadi' wajitoe kwenye nafasi zao, lazima ajitahidi kufafanua kuwa mafisadi anamaanisha kuwa wale waliotajwa mwanzoni, sio hawa wa sasa. Kimantiki hii inapunguza uzito wa kauli yake ya kwanza.
Akina nape hawana ushahidi wa ufisadi wa wale wa Mwanzo, lakini Slaa anao. Hii ina maana kuwa Nape hawezi tena kumshupalia Lowassa aondoke NEC kwa sababu ametajwa kwenye ufisadi, na hapo hapo anamwacha malecela, mabye naye ametajwa.

Uwepo wa EL, RA, AC, na wengine ndani ya CCM, ni mtaji mzuri kwa CDM. Kwa hiyo wanachofanya CDM ni kuwapa kazi ngumu CCM kuwaondoa hawa ili CDM wawe na attacking point bana...
Tuko

Kuna watu hawajajua timing ya Chadema kwanini wataje leo na si kabla ya CCM kutangaza kujivua gamba kwani hii list mpya Chadema hawakuwa nayo. Kama unavyosema Chadema wangekaa kimya lingekuwa kosa la mwaka, mara baada tu ya kikao cha NEC Dodoma tulianza kuwasikia wakisema Chadema hawana hoja kwa vile tumewatimua EL na RA ambao ndio ulikuwa mtaji wa Chadema, kwa hiyo timing ya Chadema imeifanya hoja hiyo kufa kwa vile kina Nnuye wanatakiwa waanze tena kuwatetea waliotajwa.

Kwa Chadema kutaja list of shame no.2 imewachanganya kabisa CCM hawajui watetee ipi, leo hawana tena guts kama zamani za kusema CCM haina mafisadi kwa vile wameshakiri kwa ile no 1, na hii list no. 2 itakuwa vigumu sana kwao kuipinga wakaeleweka kwa wananchi. Kama ulivyosema Nape sasa ana wakati mgumu anapambana na maadui watatu wa ndani list no. 1 waliopewa siku 90 hawatakubali kwa vile kuna wengine kwenye list no. 2 at the same time anatakiwa ajibu hoja za Chadema wakati huo huo akijenge chama kwa ku prove kweli wamejivua gamba.

Kuna mzungumzaji amesema CCM wana alternatives tatu na zote ni mitaji kwa Chadema
1. Waamuae kuziba masikio wajifanye kuwasamehe (mtaji tosha kwa wapinzani)
2. Wawafukuze kina EL na wenzake (moto ndani kwa ndani) vipi watauliza list no. 2?
3. Wabadili slogan yao ya kujivua gamba (hawataeleweka).

Kwa hiyo unaweza kuona kabisa ulikuwa ni mpango mahususi wa Chadema kutaja leo ni kama walijua CCM watatoka na singo fulani kwa hiyo kuifunika ni kutoa vol. 2.
 
- Well, I totally disagree na Dr. Slaa na infact hii inaweza kumshushia hadhi yake na chama chake pia, kwanza slaa ni lazima awe mkweli kwamba EPA ni idea ambayo imekuwepo toka hata yeye akiwa CCM, tatizo halikuwa kuchukua hela za EPA kwa sababu katika kuzichukua zimekua zikichukuliwa kama mkopo na baadaye kurudishwa na wahusika, yaani toka enzi za TANU na baadaye CCM.

- Katika uchaguzi wa Rais 2005, kama kawaida CCM alikopa hela hizo, lakini tatizo ni kwamba kuna wasiohusika walioshirki katika zoezi hilo la kukopa hizo hela na hela hizo zilitumiwa na kundi la Mtandao kwa ruhusa ya Rais wa wakati huo, badala ya CCM kama chama, sasa DPP ana haki kikatiba yetu kuamua the final decision kesi gani iende kwenye sheria na ipi isiende in EPA's case, aliamua waliokopa wote wazilipe zile hela back walipozikopa, now it is debatable legally na politically I mean the integrity ya uamuzi.

- Now nimeshitushwa na Dr. Slaa kumuhusisha Dr. Malecela na EPA, huku inafahamika na kila mwananchi taifa hili kwamba hela za EPA zilitumika kwenye kampeni za Urais, against the very Malecela sasa alihusikaje na hizo hela hapo ninaomba msaada wa yoyote anayelewa FACTS kuliko ninazijua on this ishu!

William @ NYC, USA.

Ok Mheshimiwa William Malecela najua hii taarifa yako umeipata jikoni. Kwamba CCM ni kweli walichukua fedha za EPA kupitia kagoda chini ya uchukuzi wa Rostam na usimamizi wa John malecela.

EPA haukuwa mfuko wa kukopesha, zilikuwa fedha kwa ajili ya kulipa madeni, sasa ni lini EPA walianza kukopesha? Kwa hiyo kama uyasemayo ni kweli kwanini kina malecela wasiseme kwamba hatukuiba tulijikopesha? Mbona tuliunda tume na haikusema zile fedha kuna watu walikuwa wamekopeshwa.

Marehemu Wakili maarufu Moses maira akiwa anamsimamia Jeetu patel kwenye wizi wa EPA akiwa alitumika kununulia magari ya CCM, Jeetu alishtakiwa kwa kosa la wizi, na ujanja waliofunya walimwambia alipe ila alikuwa hana fedha za kulipa kwani fungu kubwa alilipeka CCM Sasa kama ni mkopo mbona mlitumia wajanja na akaunti mnazikana?

Nikimnukuu Katibu wenu mkuu mliemtuliza alisema EPA wezi wote ni watu waliojitfanyia wenyewe chama hakihusiki, kama kweli ni mkopo mbona chama kinawakana wote na leo kina waita mafisadi ndani ya chama?

Nakushukuru kwani umekubali Mzee ameshiriki tena unasema waliaanza kutuibia tangaia Tanu. Mwaka huu mtamu.
 
Nadhani mojawapo ya maazimio ya vikao vikuu vya CCM vilivyomalizika siku za karibuni lilikuwa ni kutuma watu JF waje waitete hapa. Ndio maana unaona mara baada ya kikao wako watu wanaushabiki wa CCM usio na mbele wala nyuma hapa. Na walianza kwa Msekwa kulalamika rasmi kwamba JF inawaumiza.

CCM na mtangulizi wake TANU wametutawala kwa mika 50 mfululizo bila kuweza kuleta maendeleo. Sasa wanataka miaka mingine zaidi ili wafanye nini?

Ni kazi ya CDM kuikosoa CCM kwa kuwataja mafisadi inaowaatamia. Hongera Kamanda wetu Dr. Slaa kwa kujitoa mhanga kupigania Watanzania. Endelea kuwataja. Mwizi akiitwa mwizi hukasirika sana, na wale anaokula nao pia wanakasirika. Ndio maana unaowaona wakipiga kelele za uongo hapa. Wanadai eti unatumiwa na mafisadi. Hatudanganyiki.
 
Kama January ana issue ya mitihani, basi hiyo ni issue ndogo sana, issue haswa iko mji kasoro, wakati huo baba mjeshi. All and all, haijalishi ulifanya nini zamani, mambo mengine ni utoto. Kwa sasa he is a smart guy!. Yeye na Nape, ni vichwa vinavyokubalika, tatizo ni hili li dudu-CCM!.
Pasco pole kweli upenzi huwa unapofusha unasema January na Nape ni smart guys tatizo CCM what do you mean, hujui kuwa hawa ni baadhi ya viongozi wa kitaifa wa CCM, huwa unaonekana unataka sana kusifia lakini tatizo huwa unakosa cha kusifia ndani ya CCM matokeo yake unalazimisha.
 
- Slaa hajaenda mahakamani kuhusu kuibiwa kura za urais alioushinda, Chadema haijaenda mahakamani kuhusu kupokea hela za nje kuleta vurugu, mkuu wewe na Slaa ndio waamuzi wa mwisho kuhusu public opinion soma vizuri mawazo ya watu hapa utaona kwamba kwenye haya majina mapya Slaa ameharibu so is Chadema, ndio maana kuna siku nilisema hivi kuna wananchi wengi Tanzania hawajui kwamba Slaa ni kiongozi wa Chadema, kwa sababu it is always about him na kuwepo kwenye media kila siku, ameibiwa kura za uchaguzi hajaenda mahakamani mpaka leo, Mtikila kesi ya mgombea binafsi ameenda kwenye sheria na kuishinda serikali, now you wonder nani mwenye nafuu!

- Mangula na Malecela hawawezi kuwa mafisadi for that Slaa ametuhadaa na binafsi nimekosa heshima tena na huyu kiongozi wenu mlipua mabomu, niliongea na mtu mmoja aliyewahi kugombea ubunge na Slaa, akaniambia ni tabia yake kukuzushia maneno mengi sana ya uongo, anasema hata yeye mpaka leo hana hamu naye, Slaa arudi chini kukijenga chama badala ya kulilia media headlines kila siku hazikijengi chama huko vijijini ambako kuna majimbo Chadema haikuweka wagombea kabisa kwa kutokuwa na presence, ni ushauri wa bure tu!

William @ NYC, USA.

Umeamua kuweka busara zako pembeni.Hivi na usomi wako hujui kwanini Dkt Slaa hakwenda mahakamani?Rejea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za Uchaguzi kuhusu matokeo ya urais.

Umeng'ang'ania kwanini Chadema hawajaenda mahakamani kuhusu tuhuma kuwa wanapewa fedha kutoka nje.Usijaribu kusaka utetezi kwenye hoja hii kwa vile Chadema WALITANGAZA NIA YA KWENDA MAHAKAMANI.Sasa kama wameshaenda au wataenda mwakani,la muhimu ni kuwa WALITANGAZA HADHARANI.What about Mzee Malecela?Anaona aibu hata kujibu maswali ya waandishi wa habari.Je Chadema nao waliona aibu kujibu maswali ya waandishi wa habari walipotuhumiwa kupewa fedha kutoka nje ya nchi?

Eti maoni ya watu hapa yanaonyesha kuwa Slaa ameharibu?Kaharibu kwa vile kamtaja baba yako?Well,anaweza kuwa ameharibu hadhi ya familia yenu lakini kwa sie wenye nchi,tuliochoka kuibiwa huku wezi wakipeleka watoto wao ng'ambo,na kuwarithisha madaraka serikalini wakijifanya watetezi wa mfumo huo wa kisultani.

Katika kuropoka kwako unaweza kutuonyesha udhaifu wako.Mtikila hakwenda mahakamni kupinga matokeo ya urais.Ungekuwa na uelewa mdogo tu ungetambua kuwa matokeo ya urais yakishatangazwa hayawezi kutenguliwa na mahakama.Na kama baba yako alipoenguliwa mara kadhaa katika jitihada zake za kuutaka urais wa Tanzania kwa tiketI ya CCM hakwenda kulalamika japo kamati ya malalamiko ndani ya chama hicho,how come umtolee mimacho Dkt Slaa?

Na je baba yako aliposhindwa kwenye kura za maoni huko Mtera alikwenda mahakamani?Slaa hakWenda mahakamani kwa vile anafahamu kanuni na sheria zinasemaje.Badala yake amehamasisha mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya free and fair elections huko mbeleni.What about Mzee Malecela?

Malecela hawezi kuwa fisadi kwa vile ni mwadilifu sana au kwa vile ni baba yako?Angekuwa mwadilifu angekubali "kuwa JUMANNE" kwa ajili tu ya tamaa za urais?Angekuwa mwadilifu angewatukana Watanzania kwa kuwaambia they could go to hell?Huyu mzee amejiumbua mwenyewe hata kabla ya kutajwa kwenye list ya ufisadi.Miaka nenda miaka rudi ameng'ang'ania madaraka mpaka wapiga kura walipompa za uso....wakamgaragaza,kisa tamaa ya madaraka.Halafu unasema "Malecela hawezi kuwa fisadi".Labda hawezi kuwa fisadi kwenye familia yenu lakini sio kwa taifa letu.

Na utasema kila baya kuhusu Dkt Slaa au Chadema lakini ukweli ndio ushawekwa hadharani kuwa JOHN (a.k.a JUMANNE) CIGWIYEMISI MALECELA NI MIONGONI MWA MAFISADI,period!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom