Omari, hakuna perfect political party kama jinsi hakuna absolute freedom kwenye jambo lolote. Hivyo kila chama, kina madhaifu yake. Kwenye mada yangu humu jf ya 'CCM imechokwa Chadema Haijajipanga', niliorodhesha madhaifu ya CCM na ya Chadema. wapenzi wa CCM humu walijikalia kimya, wapenzi wa Chadema na viongozi wao humu wakanishukia kuwa nina chuki binafsi dhidi ya Chadema.
Wenzao CCM hawakujibu kitu lakini madhaifu yale wameanza kuyafanyia kazi kwa kusafisha nyumba yao, wao Chadema kila wakikosolewa, kamwe hawataki kukubali makosa, they play difensive huku manazi wao wakiporomosha kila aina ya matukano humu!.
Hakuna ubishi kuwa listi ya mafisadi na vita ya ufisadi, imewapa Chadema good political mileages, nawashauri wasikalie kushupalia vita ya ufisadi tuu kutwa kucha kwa maandamano na mikutano ya hadhara, its about time, wajenge chama, wajipange strategicaly over and above kubadili mind set ya Watanzania kuwa wao wanaweza, concetration iwe kusonga mbele.
Kwa vile vita ya ufisadi ndio mtaji pekee wa Chadema, sasa CCM inajipanga kuula mtaji huo, na believe me, CCM ikijipanga na kusafisha nyumba yake ikatakata dhidi ya tuhuma zote za ufisadi, 2015 ikasimamisha mgombea makini, Chadema itakosa pa kupumulia, tutarudi kule kule kwenye nchi ya chama kimoja, save CUF kwa Zanzibar!.
Mimi binafsi naikubali sana Chadema na naiwish all the best ili kufikisha idadi ya simple majority ndani ya bunge la 2015, ila kwa mwendo huu wa kuimba wimbo ule ule, wananitia mashaka!.
Heshima zikufikie mkuu Pasco,
Najua swala hili la CCM kumtoa Makamba na kumwingiza Makamba linaonekana kwa wana CCM na wapenzi kwamba ni jambo jema. Ila ukweli ni kwamba hakuna kitu kimetokea mpaka sasa zaidi ya kupwaya kimamlaka, dira, mfumo na mshiko wa kuwa na uthubutu wa kuwaletea wananchi maisha bora.
CDM imekuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi kuzitambua kerao zao, hasa maisha magumu, ukosefu wa elimu bora, ukosefu wa miundo mbinu thabiti na huduma zote muhimu za jamii. na imekuwa ikiwakumbusha wananchi matokeo ya umasikini huu ni kushindwa kwa uongozi wa CCM kwa miaka 50. Wapo wananchi wengi wanaoipenda CDM kwa sera za ukombozi.
Ili kuweza kuendesha nchi lazima ujue ni matatizo gani yaliyopo na jinsi ya kuyatatatua kwa resources zilizopo.
Hatuwezi kutumia rasilimali zetu wakati tukivuna baadhi wanakuala, ufisadi utaendelea kupigiwa kelele siku zote kwani huo upo sehemu nyingi na ndio bomba kubwa linalokula uchumi wa nchi.
CCM kubadili sura hukuwezi kurudisha mapenzi kwa Mtanzania ambaye hana ajira, anakosa dawa hospitali, hana maji wala barabara. Ananguzo ya umeme isiyotoa nishati. Akiingia mahakamni hana haki mpaka atoe kitu. Mtoto wake anakwenda shule yenye mwalimu mmoja.
Anachopata nia ahadi ndani ya VX kila baada ya miaka mitano na kunedelea kuisikia jina la Mwinyi, Mkapa, Makamba, Kikwete , karume. Malecela nk kila mwaka hadi mwaka kwani linabadilika la kwanza tu , na hakuna mtanzania mwenye nafasi ya sawa ya kufika huko walipo.
Pasco,
CDM imejipanga kisera na kimkamkati, kuwataja mafisadi ni sawa na kujiweka wazi kuwa mbadhirifu na mwizi hakubaliki kwenye nyumba hii, hata CDM ikiingia ikulu haitavumilia kiongozi wake mchafu.
CCM inatakiwa ibadilike kimfumo, itoa mzizi wa kulindana na kuacha kuwa tumbili kuficha kichwa na kuacha mwili mzima wazi. Kelele za jukwaani wanazopiga CCM wenye dola haziwezi kuwaletea mabadiliko.
Sidhani kama mwenye akili timamu atanunua kufanya suluhu ya kijuha na mafisadi bila kuwachukulia hatua, kama CCM wamekubali kuwa kweli wao ndio mafisadi, na wameona hawawezi kukaa na watu wenye tuhuma za kuibia taifa masikini, kwa nini wasimruhusu DPP awafungulie mashitaka ya makosa waliohusika nayo, wasiwatoa kwenye nyadhifa za serikali? wawaachia wapepelezi na CAG kufanya kazi yake na kila mtu kwa wajibika kisheria?
Ni wangapi wapo serikalini leo wanatuibia na kulitia taifa hasara? Je ni kweli ni lazima tuwe gizani kupoteza uzalishaji eti hatuna uwezo wa kuwa na nishati ya uhakika? Huu wote ni ufisadi.
Kamanda Ngoma ya Rushwa, ufisadi, madaraka mabovu na utawala wa urithi umewatoa viongozi na vyama vingi vikongwe madarakani kama Mexco, Misri, Tunisia, Kenya, Zambia, nk Si dhani kama Tanzania chini ya CCM itaweza kuendelea kuhadaa kizazi cha sasa chenye kiu ya kweli ya Maisha bora bila usawa wa mafanikio.
Leo Tanzania tunazaidi ya vyuo vikuu 25 amabavyo kila mwaka vinaongeza wahitimu mtaani bila mategemeo yeyote ya maisha bora. Graduates hawa ndio wamejaa vijiweni wakiona hali halisi ya maisha mabovu, na kila aliyedarasani sasa hivi hana uhakika wa nini kitatokea baada ya kumaliza. Sasa unasema kweli ngonjera za January na Nape zinawaletea ajira na maisha bora?
CCM wanatakiwa kujua wajibu wa chama tawala sio kujifanya na wao wanataka kuwa wakati ni watawala. Akili za yeyote mwenye kadi ya ccm huwa kama zinakutu, ya kufikiri, kuona, na kutenda.
Tanzania inahitaji watawala wanaojua shida zao na utatuzi, usanii wa CCM umefika kikomo na hawana jipya zaidi ya kuendekeza siasa za kiimla badala ya kuwajibika.