Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Si Magufuli aliyezua uuzwaji wa nyumba za Mawaziri kipindi cha Mkapa? Nyumba zinazouzwa ni miradi ya shirika la nyumba. Kujenga na kuuza. Slaa kwishnei. Subiri Magufuli amjibu.
 
Mkuu Dr. Slaa

Hapa inatakiwa Chadema kucheza Chess na sio Checkers. EL, RA & Chenge ni watu ambao ni Mafisadi Papa, pesa walizonazo ni nyingi na EL ni kama amepagawa yeye anataka urais 2015 utadhani ameambiwa atafariki bila kukamilisha hilo. Chadema wasubiri damage na mpasuko mkubwa unaokuja utakaosababishwa na hii move. Unaposema Mangula, Malecela, Magufuli ni mafisadi unaongeza nguvu kwa kina EL na kuwafanya wananchi ambao wanampenda Magufuli kuanza kuquestion Chadema Motives.

All in all, dhamira ya kutaka hawa watu waondolewe ubunge nk ni nzuri, lakini subirini kwanza mpaka JULY, CCM ikiwatema tu, then Chadema waanze kudai lazima wapelekwe mahakamani na ubunge watoswe. Hapo kutakuwa na hoja ya msingi.

After JULY, then unaweza kuja na hii hoja kuwa CCM wafisadi wako wengi nk, lakini muda huo Chadema itakuwa kwenye wakati mzuri sababu kina EL nao watakuwa wanaiattack CCM direct kwa kutumia watu wao serikali, vyombo vya habari, CCM nk. Kuna siri nyingi sana tutajuwa wakishatoswa.

Chadema itapata hasara sana kama CCM watashindwa kuwatosa hawa watu watatu.
Moelex23, asante sana kwa hili, Chadema ina udhaifu mkubwa wa kukosa long time strategiest hivyo kukalia kushindana kulipua mabomu.
Mimi ni miongoni mwa wapenzi wachache wa Chadema (sio mwanachama) ambao sikubaliani na baadhi ya moves za viongozi wa juu wa chama hiki.

Baada ya uchaguzi mkuu, nilisema it was wrong move kwa Dr. Slaa kususia kutangazwa kwa matokeo, nikasisitiza siku ya kutangazwa matokea was the best opportunity ya kueleza kutoridhishwa kwake na kutoyatambua matokeo.

Baada ya kutoyatambua matokeo yale, nilitegemea by now, Chadema wangekuja na altenative matokeo yao kujusfy kile wanachopinga, mpaka leo hakuna.

Sipendi Chadema ibaki kuwa ni chama cha kulalamika na kuendesha maandamano, natamani Chadema wewe chama chenye vision ya kuona political opportunity and seize such opportunities for their advantage.

CCM kujivua gamba is an opportunity huku ni kuvuja kwa pakacha (CCM), ambayo inatakiwa kuwa nafuu kwa mchukuzi (Chadema), badala ya mchukuzi kujituliza na kujiachia tuu mpaka pakacha libaki tupu, yeye ndio wa kwanza kumweleza mwenye pakacha, kuwa pakacha linavuja!, hivyo kumpa nafasi kuziba matundu yote hata yale ambayo yangempa unafuu mchukuzi!.

Kwenye hoja ya ufisadi, tayari CCM wanashikana mashati kutafutana uchawi, Chadema ilitakiwa ikae kimya iangalie tuu hii sinema. Kitendo cha Chadema kupiga kelele mpya, na kuwataja vipenzi vya watu kama kina Magufuli, kutaifanya CCM kuwasamehe hata mafisadi wake kama kina RA, EL na Mzee wa Vijisenti!.

Kwa mfano mtu kama Magufuli, hata ukiutangaza ufisadi wake kwa mabango, vipeperushi na maandamano nchi nzima, halafu uchaguzi ukaitishwa kesho, John Pombe Magufuli akasimama na Dr. Slaa, John Pombe, atamtupa kwa mbali Dr, kwa sababu moja tuu, watu watachagua mtu na sio chama. Pombe ana good track record ya kudeliver, Dr. yeye ndio kwanza anaitafuta hiyo opportunity ya kuwathibitishia Watanzania kuwa ata deliver.

Ndani ya Chadema, nadhani kitu vitu vikipangwa, hakuna wa kushauri otherwise, and this is not good kwa chama makini.

Pasco.
 
Mkuu Dr. Slaa

Unaposema Mangula, Malecela, Magufuli ni mafisadi unaongeza nguvu kwa kina EL na kuwafanya wananchi ambao wanampenda Magufuli kuanza kuquestion Chadema Motives.
.
Hapa tatizo ni kutajwa Magufuli?????????
Nyumba za serikali ziliuzwa chini yake kwa hiyo anapaswa kubeba hiyo dhambi.
Ni kweli Magufuli anakubalika sana, personally namkubali lakini hii si sababu yakutufanya tusahau uuzwajwi wa nyumba zile.
 
Kwa mfano mtu kama Magufuli, hata ukiutangaza ufisadi wake kwa mabango, vipeperushi na maandamano nchi nzima, halafu uchaguzi ukaitishwa kesho, John Pombe Magufuli akasimama na Dr. Slaa, John Pombe, atamtupa kwa mbali Dr, kwa sababu moja tuu, watu watachagua mtu na sio chama. Pombe ana good track record ya kudeliver, Dr. yeye ndio kwanza anaitafuta hiyo opportunity ya kuwathibitishia Watanzania kuwa ata deliver.
Pasco.
Binafsi ningempigia Magufuli. (lengo ni Dr Slaa abaki watchdog wa serikali ya Magufuli as he is best at this)
Magufuli kutajwa kwenye list ni jambo lisiloepukika.
Ushindi wa Magufulu kwa Dr Slaa halialalishi ubora wake hasa tukizingatia mfumo wetu TZ (CCM hata Rostam akigombea atatangazwa mshindi)
 
Moelex23, asante sana kwa hili, Chadema ina udhaifu mkubwa wa kukosa long time strategiest hivyo kukalia kushindana kulipua mabomu.

Sipendi Chadema ibaki kuwa ni chama cha kulalamika na kuendesha maandamano, natamani Chadema wewe chama chenye vision ya kuona political opportunity and seize such opportunities for their advantage.

Kwenye hoja ya ufisadi, tayari CCM wanashikana mashati kutafutana uchawi, Chadema ilitakiwa ikae kimya iangalie tuu hii sinema. Kitendo cha Chadema kupiga kelele mpya, na kuwataja vipenzi vya watu kama kina Magufuli, kutaifanya CCM kuwasamehe hata mafisadi wake kama kina RA, EL na Mzee wa Vijisenti!.

Kwa mfano mtu kama Magufuli, hata ukiutangaza ufisadi wake kwa mabango, vipeperushi na maandamano nchi nzima, halafu uchaguzi ukaitishwa kesho, John Pombe Magufuli akasimama na Dr. Slaa, John Pombe, atamtupa kwa mbali Dr, kwa sababu moja tuu, watu watachagua mtu na sio chama. Pombe ana good track record ya kudeliver, Dr. yeye ndio kwanza anaitafuta hiyo opportunity ya kuwathibitishia Watanzania kuwa ata deliver.

Ndani ya Chadema, nadhani kitu vitu vikipangwa, hakuna wa kushauri otherwise, and this is not good kwa chama makini.

Pasco.

Great thinking bro!!

Nina hofu sana na hatima ya kisiasa ya Dr.Slaa kwa mwendo huu anaoelekea nao sasa!!
 
My god,ufisadi ni tatizo la binadamu.ufisadi means personal interest.poleni sana msiojua.nampenda silaa lakini ni binadamu ana personal interest.unamjua obama watu walipiga debe.kumbe kbaraka wa GEORGE SORO. nenda Abovetopsecret.com.utashangaa.USITUMIE EWE MBONGO.elungata need you to accept him as your prez.usijali sana u will know me soon
 
Kumbe tunaongea na watu wko neywork.umefikaje huko wily mmefisdi mali yetu wabongo.vijana WAKEUP MSIKUBALI.Ewe mbongo wa kawaida hata nauli ya kutoka mkoa kwenda mkoa shida leo hii mtu yuko newyork anajifanya ana machungu.WEWE TUSIKUBALI
 
Kwenye hoja ya ufisadi, tayari CCM wanashikana mashati kutafutana uchawi, Chadema ilitakiwa ikae kimya iangalie tuu hii sinema. Kitendo cha Chadema kupiga kelele mpya, na kuwataja vipenzi vya watu kama kina Magufuli, kutaifanya CCM kuwasamehe hata mafisadi wake kama kina RA, EL na Mzee wa Vijisenti!.

Pasco.

Mkuu Pasco;

Hivyo ni vile ambavyo wewe unaona. Ni chaguo lako kuona ni upande upi wa shillingi unataka kuuona.

Najiuliza maswali mengi una maana gani unaposema "na kuwataja vipenzi vya watu kama kina Magufuli, kutaifanya CCM kuwasamehe hata mafisadi wake kama kina RA, EL na Mzee wa Vijisenti!". Elewa kuwa wakati mbaya wa CCM kuwatosa makada hawa ilikuwa ni kabla ya uchaguzi. Hawakufanya hivyo kwa kuwa chama kingesambaratika. Hawakuweza kufanya hivyo kimikakati na ndiyo maana JK aliwakumbatia na kuwasafisha kipindi hicho. Lakini si sasa, ulazima wao wa kuwepo ndani ya chama si muhimu kama kipindi kile.

Elewa mpaka sasa move ya EL na timu yake ya kutaka kumwondoa JK kuwa mwenyekiti wa CCM ndiyo iliyowacost sana. Pia wasiwasi wa JK atakapomaliza ngwe yake Nchi amwachie nani na historia itamuhukumu vipi. Ieleweke BWM hana raha hadi leo kwa kelele anazopigiwa.

Wakati wewe unaona move ya CHADEMA ya kutaja mafisadi zaidi ni wrong upande mwingine wa shillingi unaonyesha kuwa hii ni strategy nzuri. Kwa kuwataja "wasafi wa CCM" kuwa mafisadi: Magufuli; Malecela; Mang'ula; na vigogo wa kudumu CC na NEC ya CCM: Sumaye; Mkapa na JK ina maana wao pia wafukuzwe uanachama. je watafukuzwa? RA na sophia simba alisema ndani ya CC kuwa hakuna ushahidi lakini CC safari hii haikukubali na ikawatosa, so suala la ushahidi si issue kwa sasa ila issue ni ushahidi wa kimazingira na kisiasa.

CHADEMA wanajua kwa kulitaja hili CCM wana chaguzi 3:

1. Kufuta mpango wao wa kujivua Gamba na kukaa kimya kama hawajui kitu.

2. Kuwatosa mafisadi wa Phase 1 na Phase 2 kitu ambacho hakiwezekani

3. Kuwasamehe mafisadi wote wa Phase 1 na Phase 2 kama ulivyosema.

Katika hali yoyote CHADEMA wanao mtaji wa kisiasa wa kuendelea kuwapaka CCM kuwa si lolote si chochote na ni Wasanii katika vita vya Ufisadi. hapo bado kuna mafisadi wa 'stimulus package' hawajatajwa.

Nadhani move ya CHADEMA kisiasa inalipa na again kama walivyo prove kwa Phase 1 list na kuwalazimisha CCM kuchukua hatua, I believe also this one will work.

Respect.

QED.
 
Dr. Slaa is a man of principle. There is no way he would have omitted Magufuli or any other corrupt leader from his list out of a vague impression that Magufuli is popular. In fact Magufuli is no longer popular. He was popular when he served under Mkapa, but he seems to have lost the plot. Magufuli, I submit, has lately shown himself to be a person of a very poor reasoning ability.

Magufuli has proposed that the main bus stop for upcountry buses be built in Bagamoyo. That is heartless. How can a person who has travelled from such a long distance be expected to arrive in Bagamoyo and then, with luggage in hand, look for some means of transport to go from Bagamoyo to Magomeni, Ubungo etc? Magufuli does not seem to think before speaking anymore.

Is it not Magufuli who ordered people to tarnish our roads by smearing some paint on all signpost that he considered to be on road reserve? That was a silly way of doing things. The only thing that was achieved was to make Dar ugly.
Dr Slaa has evidence that Magufuli is one of the big, corrupt politicians that are killing our economy. Why shouldn't he mention him?

Bravo Dr. Slaa. The nation is with you. Watatapatapa sana mafisadi na marafiki zao, lakini usijali. Kaza uzi! We, the people, support you!
 
chadema wamefulia

weka magufuli na upande mwingine mbowe. waulize wananchi nani fisadi. jibu kwa asilimia zaidi ya 90 litakuwa mbowe.

kuwataja magufuli na malecela kumemwokoa lowassa kuchukuliwa hatua na ccm.
 
Mkuu Pasco;

Hivyo ni vile ambavyo wewe unaona. Ni chaguo lako kuona ni upande upi wa shillingi unataka kuuona.

Najiuliza maswali mengi una maana gani unaposema "na kuwataja vipenzi vya watu kama kina Magufuli, kutaifanya CCM kuwasamehe hata mafisadi wake kama kina RA, EL na Mzee wa Vijisenti!". Elewa kuwa wakati mbaya wa CCM kuwatosa makada hawa ilikuwa ni kabla ya uchaguzi. Hawakufanya hivyo kwa kuwa chama kingesambaratika. Hawakuweza kufanya hivyo kimikakati na ndiyo maana JK aliwakumbatia na kuwasafisha kipindi hicho. Lakini si sasa, ulazima wao wa kuwepo ndani ya chama si muhimu kama kipindi kile.

Elewa mpaka sasa move ya EL na timu yake ya kutaka kumwondoa JK kuwa mwenyekiti wa CCM ndiyo iliyowacost sana. Pia wasiwasi wa JK atakapomaliza ngwe yake Nchi amwachie nani na historia itamuhukumu vipi. Ieleweke BWM hana raha hadi leo kwa kelele anazopigiwa.

Wakati wewe unaona move ya CHADEMA ya kutaja mafisadi zaidi ni wrong upande mwingine wa shillingi unaonyesha kuwa hii ni strategy nzuri. Kwa kuwataja "wasafi wa CCM" kuwa mafisadi: Magufuli; Malecela; Mang'ula; na vigogo wa kudumu CC na NEC ya CCM: Sumaye; Mkapa na JK ina maana wao pia wafukuzwe uanachama. je watafukuzwa? RA na sophia simba alisema ndani ya CC kuwa hakuna ushahidi lakini CC safari hii haikukubali na ikawatosa, so suala la ushahidi si issue kwa sasa ila issue ni ushahidi wa kimazingira na kisiasa.

CHADEMA wanajua kwa kulitaja hili CCM wana chaguzi 3:

1. Kufuta mpango wao wa kujivua Gamba na kukaa kimya kama hawajui kitu.

2. Kuwatosa mafisadi wa Phase 1 na Phase 2 kitu ambacho hakiwezekani

3. Kuwasamehe mafisadi wote wa Phase 1 na Phase 2 kama ulivyosema.

Katika hali yoyote CHADEMA wanao mtaji wa kisiasa wa kuendelea kuwapaka CCM kuwa si lolote si chochote na ni Wasanii katika vita vya Ufisadi. hapo bado kuna mafisadi wa 'stimulus package' hawajatajwa.

Nadhani move ya CHADEMA kisiasa inalipa na again kama walivyo prove kwa Phase 1 list na kuwalazimisha CCM kuchukua hatua, I believe also this one will work.

Respect.

QED.

wewe sio superman ni propagandist wa chadema.
 
Nyangomboli,

Ndiyo maana kwa watu wanaoangalia tu haraka haraka si rahisi kuelewa na wanavutika na "kuvua Gamba". The Ufisadi issue is much deeper than most people understand. Ukisema hawa wazere hawana kitu ni "safi" basi ni vema mkatueleza Vijinoti "messages" za hawa wazee zilizotoa fedha kwa Balali zilikuwa za nini. Kama mtu haelewi kitu si vema kujitumbukiza kwa utetezi. Kumbukeni nilishaambiwa "nitapelekwa mhakamani" hjadi leo hakuna badala yake wao ndio wako mahakamani japo ni cosmetic tu.

Niliambiwa "nisali" nina dakika chache za kuishi. Nadunda hadi leo lakini mastokeo wao wenyewe wamepeana siku 90 za kujiondoa kwenye uongozi. Ndugu zangu wengi wanajadili kwa ushabiki. Kama mtu haelewi mtuachie tunaoelewa undani na tulio na ushahidi wa kina. Wala usituambie tuweke hapa, kuna mahali tukitakiwa tutapeleka lakini si jamvini na sababu zinajulikana. Ila ieleweke,

i) Wenzetu wanavua Gamba ndani ya CCM. Lakini fedha zilizoibiwa ni za CCM hivyo siyo issue ya CCM tu. Consequences za kuvua Gamba lazima ziende nje ya CCM i.e. kama ni mbunge ajivue, kama ni kiongozi serikalini ajivue.

ii) Watanzania ndio tulioibiwa, hivyo mtu asiojaribu kamwe kutufunga mdomo. Tulianzisha ngoma hii tutaicheza hadi mwisho, nchi itakaporudi kwenye njia sahihi. Wanaoogopa mchezo huu wakae mbali. Lakini Watanzania wasio na hofu na wenye uchungu na nchi yetu kamwe hatutanyamazishwa na yeyote yule, wala na kitendo cha CCM kujivua Gamba.

Asilani, wamekubali sasa wenyewe wanaimba "wimbo wetu" mchezo ndio umefika patamu.

muzee umefulia. magufuli ni msafi kuliko wewe na mbowe.

mbona wewe hujaenda mahakamani kwa kuibiwa kura zako. waambie wa arusha waende mahakamani.

unataka ccm tu ndio waende mahakamani. ni kichekesho
 
Aloo. Mimi nilikuwa hewani kabla hata web browsers hazijagunduliwa: wakati huo Mosaic, Netscape Navigator 1.0 na Internet Explorer 1.0 zilikuwa bado hazijazaliwa. I've been through 'em all since then, kuanzia TANZANET hadi JF and everything in between kama YA, DARHOTBOARDS, BSCTIMES.COM, TANZATL.ORG, you name it. What's more: huyo demi-God wako Slaa pia namfahamu vizuri, at a more or less personal level, kabla hajaenda Italia kusomea madigrii yake ya Sheria za Kanisa, na hata baada ya kurudi Bongo: prior to and after he became Secretary General of TEC. So basically, you got nothing to tell me dude!

Hata zama za Yesu na Muhammmad kulikuwa na mataahira,sembuse zama za Tanzanet,et al!.How early you knew how to browse the net,and how many forums you have so far been a member is immaterial.What matters most is whether you talk sense or just another load of garbage.

Wewe si wa kwanza kubainisha kuwa unamjua Dkt Slaa kuliko wengine.Kuna wenzio waliosadia na chama tawala na serikali kusikika kuhusu "uchafu","maovu","undani",na kila aina ya upuuzi kuhusu Dkt Slaa.Kabla ya kumnyooshea kidole yeye,tueleze how clean you are...though your attitude and crude language zinaweza kutupa clues.

Labda huko kumfahamu kwako ndio kumepelekea hasira zako dhidi yake.Yawezekana ulitarajia kuwa yaliyomtokea kwenye maisha yake ya awali ndio ungekuwa mwisho wa safari yake.Kwa vile Mungu si Athumani au wewe,mwenzio amefika hapo alipo.You can hate him for the rest of your life lakini you'll remain an anonymous nobody while Dkt wa ukweli akituongoza kwenye safari ya ukombozi wa nchi yetu.

Si vigumu kubashiri kiilichokukurupusha ujiunge na JF April 17,2011 -mara baada ya Dkt Slaa ku-update orodha ya mafisadi.Mtanuna sana mwaka huu.Mtatukana sana,na mtatumia kila aina ya maneno machafu lakini mnachopuuza ni ukweli kwamba suala sio Dkt Slaa bali hali halisi inayowakabili Watanzania.
 
chadema wamefulia

weka magufuli na upande mwingine mbowe. waulize wananchi nani fisadi. jibu kwa asilimia zaidi ya 90 litakuwa mbowe.

kuwataja magufuli na malecela kumemwokoa lowassa kuchukuliwa hatua na ccm.

wewe sio superman ni propagandist wa chadema.

muzee umefulia. magufuli ni msafi kuliko wewe na mbowe.

mbona wewe hujaenda mahakamani kwa kuibiwa kura zako. waambie wa arusha waende mahakamani.

unataka ccm tu ndio waende mahakamani. ni kichekesho

Jiskie aibu japo kidogo.Wangekuwa wamefulia ungepoteza muda wako japo kuwataja?Badala ya kupanua vingine,jaripu kupanua upeo wako na kufikiria mbali zaidi ya hapo ofisini kwako.Mwangalie jirani yako,angalia hali katika kijiji ulichozaliwa,ongea na wazazi wako,fanya tathmini mwenyewe.

Ni rahisi kumlaumu Dkt Slaa au Chadema,kwa vile wapo wanaodhani anafanya anayofanya kwa maslahi yake binafsi na ya kisiasa.Lakini hebu jaribu kumwondoa Dkt Slaa kwenye picha,kisha chambua hali halisi ya nchi yako.Weka hisia pembeni bali zingatia facts katika utafiti wako usio rasmi.

Kama una mapenzi ya kweli na nchi yetu ni dhahiri utabaini kuwa tuna matatizo lukuki,huku kubwa likiwa umasikini wa kupindukia miongoni mwa Watanzania wengi japo watawala wetu wanaishi kifalme.Sidhani kama utapata shida kugundua uwepo wa mgao wa umeme, au bei za vyakula zinazozidi kupanda,au hata namna ya kuweza kumudu maisha yako kwa mshahara unaolipwa.

TAFAKARI
 
HTML:
[quote="Mlalahoi, post: 1869091"]Unahitaji ushahidi gani zaidi ya Mzee Malecela kutajwa hadharani kuwa ni fisadi?Mbona ulimpongeza Kikwete kwa maamuzi yake ya kuwatimua mafisadi (japo Kikwete hakuweka ushahidi hadharani) lakini linapokuja suala la babayako unataka ushahidi?Rejea ile post yako kwenye facebook wall yako kuhusu "giving credit where it's due..."
- Ya Facebook yabaki kule kule hapa ya hapa, CCM wametimua mafisadi sio JK, unaposema Malecela anahusika na EPA, unatakiwa kuonyesha evidence za makaratasi aliyoyasaini na kuwezesha kuchotwa kwa hela za wananchi benki, kama huna huo ushahidi na wewe unakua fisadi kwa kusema uongo na kutafuta umaarufu wa kisiasa ambao ni hewa! JF haiwezi kugeuka kijiwe cha walevi mkuu kwa sababu amesema Slaa tu hapana, Sophia Simba hana ushahidi kwamba Chadema wanapewa hela kutoka nje so is Slaa hana ushahidi wa Malecela au Mangula kuhusika na EPA msishushe hadhi ya Forums kwa sababu amesema Slaa tu! ha! ha! ha!

HTML:
Nimejaribu kukushauri umshauri mzee wako aende mahakamani lakini nadhani umeona ushauri huo hauna maana.Sasa badala ya kutetea kwa maneno matupu kuwa Malecela sio fisadi,tupe ushahidi kuwa sio fisadi.Sie kama jamii ushahidi wetu ni kauli ya Dkt Slaa/Chadema.Wewe je?
- Ha! ha! ha! ha! sikutegemea hata siku moja unaweza kushuka this low duh yote nini amesema Slaa basi zidumu! ha! ha! ha!

HTML:
Halafu nahofia utetezi kwa baba yako unaweza kupelekea hasira za wanyonge waliofisadiwa na genge la akina MALECELA.Yaleyale ya Saif Gaddafi kuwakashifu wanaokandamizwa na mfumo dhalimu.Watu wameibiwa kisha watoto wa majambazi hao wanaleta zao za kuleta!!!!!
- Mkuu ninakushuru sana na ushahidi wako wa EPA kuhusika na Malecela, ukweli ni kwamba una ushahidi mzito sana kuliko hata Slaa mwenyewe, UBARIKIWE SANA BRO!

William @ NYC, USA

Kwanini ya Facebook yabaki Facebook wakati aliyeandika hayo ni the same person,on same subject matter,ila tofauti sasa ni imemhusu mzazi.

Uzoefu mwepesi tu unastahili kukuonyesha kuwa jitihada za mafisadi kujisafisha au kusafishwa so far hazijaweza kufanikiwa.Unaweza kuweka kambi hapa kumtetea mzazi (who wouldnt anyway) lakini court of public opinion haihitaji hizo documentary evidence.Watanzania si wajinga wa kuaminishwa kitu kisichopo,na wana uwezo wa kuchambua pumba na mchele.Kwahiyo,laiti tuhuma za ufisadi dhidi ya Mzee Malecela ni uzushi mtupu basi same court of public opinion itamtakasa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom