Nimesikitishwa na maneno ya Prof Safari huko Tabora leo,
Pomoja na kujaribu kueleza ukweli kuwa CDM hakuna udini, ukiangalia hoja zake (copy below) zimejaa mambo yale yaleee, eti waislamu wanaonewa, waingie CDM kudai haki zao! haya ni mawazo ya kidini yasiyo na tija kwa taifa, na ni uhongo ule ule kujaribu kuonyesha ni waislamu tu wanaonyimwa haki TZ. Mbona anashindwa kueleza ni vipi waislamu wa Zanzibar wako nyuma kielimu na mambo mengine mengi pamoja na kuwa walitawaliwa na waarabu na si Waingereza anaowasingizia!
Namshauri kama ajenda yake ni kutetea haki za waislamu asichanganye kwenye siasa. Udini ni sumu mbaya sana Prof. wewe ni msomi mkubwa, tunategemea ueleze mambo yanayojenga na si kuleta chuki za kidini. Watanzania wengi bila kuangalia dini wala kabila wana watatizo yanayofanana, hatuwezi kuyaondoa kwa kujenga hoja zenye mwelekeo wa kidini.
*****************************************
Udini.
Wakoloni waliwagawa watu kwa njia za makabila ili wawatawale ,wakagawa watu kwa njia za udini mf.waingereza waliingiza dini na kjuweka watu wao serikalini , na waislamu wengi walikosa nafasi ya kusoma ndio maana hawakuingia serikalini mapema .
Waislamu walipigania uhuru ila , kutokana na waingereza kuwabagua , ndio maana waliamua kupinga ukoloni ili waweza kuweka serikali ambayo haiwabagui, anasema ugomvi wa Nyerere na shehe takadir kuhusu waislamu kubaguliwa , na anasema kuwa ndani ya CDM hakuna udini ila ndani ya nchi kuna tatizo la kihistoria la kidini.
Anasema kuwa ni mbinu ya serikali kuwagawa watanzania ili waweze kuwatawala .
Alipojitoa CUF na kujiunga na CDM alifuatwa na mashehe wakimwambia kuwa yeye ameamua kujiunga na wakristo , yeye akajibu kuwa walitaka yeye aende kwenye chama gani? Mbona CCM sio ya waislamu kwani ukiondoka JK wengi waliopo serikalini ni
Anasema yeye hajabatizwa na pia Slaa sio yohana mbatizaji na amewataka waislamu kuungana pamoja ili kupigania haki za waislamu kwani CCM ndio ambao wanawakandamiza waislamu hivyo ni bora wakajiunga na CDM kwa wingi ili waweze kudai haki zao tangu awali na wasisubiri , waingie cdm tangu mwanzo ili wawe sehemu ya kupigania haki zao na njia nzuri ni kuhakikisha nkuwa wanajiunga ili kuingiza hoja zao kabla ya cdm kuingia serikalini na ni lazima waislamu wakitaka madai yao yasikilizwe wanapaswa kuingia sasa na sio wawasusie cdm kwa hoja za udini halafu baadae waje walalamike .
Kuna haja ya kujiunga na cdm sasa.