Pasco Mkuu,
Umejichanganya sana kwa maneno yako. Kama kweli unaanza kwa kusema kuwa vita ya siasa ni kama vita vingine, basi huko chini umemaliza vibaya sana. Nashindwa kuelewa kama ulipitia JKT na kama ulipitia basi au umesahau au hukupitia mafunzo mazuri ya msituni.
Mrusi VS NATO walikuwa wakishindana kwa kutengeneza silaha. Mrusi akaja na AK-47 na NATO/USA wakaja na Mibunduki yao mikubwaa na risasi za kutisha. Ukipigwa na silaha ya NATO, unakuwa vipandevipande na kufa wakati AK-47 inakupa jelaha kubwa ila kuna uwezekano UKAWA BADO HAI.
Ubaya wa kukufanya uwe bado hai ni kuwa walio wazima itabidi wakubebe. Kama ukifa, wanakuacha na kuendelea mbele. Hivyo basi hakuna mbinu bora vitani kama kutengeneza majeruhi kwa sababu ukiwa na majeruhi wawili, basi askari wanne wanaacha kupigana. Ukiwa na maiti wawili, basi unakuwa na askari wawili zaidi na wenye hasira wakitaka kulipa kisasi kifo cha ndugu zao.
Nafikiri CHADEMA watakuwa wanatengeneza MAJERUHI ndani ya CCM wa kisiasa. CCM itakuwa na maamuzi kadhaa ambayo itabidi iyafanye na nakubaliana kwa upande huo wa shilingi maneno ya Superman:
Code:
CHADEMA wanajua kwa kulitaja hili CCM wana chaguzi 3:
1. Kufuta mpango wao wa kujivua Gamba na kukaa kimya kama hawajui kitu.
2. Kuwatosa mafisadi wa Phase 1 na Phase 2 kitu ambacho hakiwezekani
3. Kuwasamehe mafisadi wote wa Phase 1 na Phase 2 kama ulivyosema.
Nafikiri kilichowasukuma Chadema kufanya hivi si kuwa CCM walikuwa hawachezi Single yao. Ila tatizo ni kuwa mziki uliokuwa ukipigwa na Chadema ulikuwa Reggae na CCM wakaanza kuucheza kama Vijana wa Atlanta yaani CRANK. Beat hazina tofauti ila kucheza kunatofauti. Chadema watakuwa wameshtukia deal kuwa hawa jamaa wanacheza Staili nyingine kwa wimbo unaotakuwa kuchezwa kwa staili nyingine. Sasa dawa yake ni kuwawekea PURE Reggae ili wasitake tena kubadili uchezaji.
Kitendo cha kufukuza watu watatu ndani ya CCM na kuwaita kuwa ndiyo mafisadi, ni kichekesho na tuuite kwa jina KAFARA. Wakishafanya hivyo, watapiga kelele Tanzania nzima kuwa WAMEJIOSHA tayari sasa mnataka nini? German, yule Mzee
Chancellor Helmut Kohl alipokea pesa kutoka kampuni la mafuta la ELF (France) kwa ajili ya chama. Ilipogundulika, alishambuliwa hadi ndani ya chama chake na mmoja ya waliompiga madongo aondoke ni huyu mama Chancellor wa sasa Angela Merkel ambaye walikuwa chama kimoja na ndiyo alimlea ndani ya chama hicho.
Kwenye SIASA nilishasikia maneno haya kuwa "Adui yako ni nyoka, ponda kichwa na tupilia mbali....." Kikwete alifanya hivyo kwa adui zake na wengi wao hadi leo wako HOI kama si Marehemu Ki-Siasa. Sijui Chadema kama pia wanalitumia hilo kuwaponda woote wanaoweza kugombea mwaka 2015 ili kuwamaliza kisiasa mapema kabisa.
Kwa hali ilivyo sasa na Ukorofi wa Lowassa, sidhani kama atataka kuondoka tena na kuwa KAFARA. Sababu ya kutokuondoka kapewa na SLAA. Akigoma kuondoka, Chadema watasema "Magamba ya CCM bado yapo." Kwa sasa ndani ya CCM, wameshapewa mziki mzito sana ambao hadi namhurumia Kikwete.
Huo ufisadi mpya, unasubiri siku yake. Ukiwa unacheza karata, huonyeshi karata zako zote na ukiwa vitani, unatumia kwanza bunduki za kawaida. Mambo yakianza kubadilika, unahamia kwenye bunduki nzito/Kubwa, unakuja mizinga, vifaru, ndege na hadi akina SCUD. Pili kumbuka Slaa hawezi kukurupuka kutumia datas ambazo hana uhakika nazo. Zinaweza kuwa zimepikwa na hata CAG kaingizwa mjini na wewe ukizidandia, unakwenda na maji.
Jibu pekee zuri kwa CCM ni kuondowa watu wengi sana ndani yake jambo ambalo sidhani wako tayari kulifanya. Wakigoma, Chadema ndiyo wanafurahi na kwenda kuwashtaki kwa wananchi. Ngoja tuone/tusubiri kama ambavyo jana Mwenyewe Slaa kaandika kuwa "Mtuachie wenyewe tucheza kama hili jambo hamlifahamu vizuri kwa ndani.........." TIME WILL TELL.